Je, kauli ya Rais Samia inathibitisha kuwa ni wakati wa Mwenge wa Uhuru kuwekwa kando?

Je, kauli ya Rais Samia inathibitisha kuwa ni wakati wa Mwenge wa Uhuru kuwekwa kando?

Mh Rais, amesema mwenge uliowekwa katika daraja la Tanzanite uondolewe, na iwekwe alama ya Tanzanite,

Ukiachana na ukweli kwamba Mh Rais akiwa Makamu wa Rais aliona michoro ya daraja hili kabla halijaanza kujengwa, na mwenge ulikuwepo katika michoro, hivyo angeweza kutoa maoni yake na kuzuia mwenge kutengenezwa .

Lakini ukiachana na ukweli kwamba wakati Mh Rais anakabidhiwa kiti cha Urais alijua daraja litakuwa na mwenge, lakini ulikuwa haujawekwa wala kutengenezwa hivyo angeweza kutoa mapendekezo wakati huo na kuzuia mwenge kutengenezwa na kuwekwa.

Pia ukiachana na ukweli kwamba Mh Rais si Mhandisi wa Madaraja , hivyo hajui ule mwenge pale juu kwa sasa baada ya kukamilika kwa daraja , kuondolewa kwake kama kunaweza kuathiri mlinganyo na uzania wa daraja,

Laini pia ukiacha ukweli kuwa gharama zimetumika kuutengeneza ule mwenge na kuuweka juu ya daraja, na anaagiza gharama mpya za kutengeneza jiwe la Tanzanite

HOJA YANGU NI, kwa kauli hii ya Mh Rais, je ni kweli kuwa umuhimu wa mwenge umeanza kupotea machoni mwa wakuu wanchi,?
Je ni wakati muafaka sasa kuuweka mwenge wa uhuru katika JUMBA LA MAKUMBUSHO na kuepuka gharama kubwa ya kuukimbiza nchi nzima.?

Hoja ya mwenge wa uhuru kuwekwa makumbusho imekuwepo kwa muda mrefu sana, hasa gharama zinazoendana na shughuli za kukimbiza mwenge, zinapolinganishwa na matokea ya kuukimbiza.

Je kwa Mh Rais kutaka uondolewe katika daraja la Tanzanite ni ishara kuwa mwenge si tena kielelezo cha kupewa kipaumbele?

#songoka Vatican katika kwaresma
 
Tatizo kubwa Wanasiasa na Walokole wa Taifa hili WANAFIKIRI Matatizo yao yote Yanasababishwa na Mwenge.
 
Tz cheo Cha Makam wa Rais kwa katiba Hii ni Kama bahasha tu , barua ni Rais mwenyewe basi,
 
Mwenge wa uhuru una mazuri yake na mabaya yake, moja ya zuri miradi ya maendeleo huzimduliwa na mingine kukaguliwa, baya mikesha yake huchochea maambukizi ya ukimwi na kupunguza nguvu kazi ya taifa.

Sasa muamue huo mwenge uendelee kuwepo au uondolewe.
 
Mwenge wa uhuru una mazuri yake na mabaya yake, moja ya zuri miradi ya maendeleo huzimduliwa na mingine kukaguliwa, baya mikesha yake huchochea maambukizi ya ukimwi na kupunguza nguvu kazi ya taifa.

Sasa muamue huo mwenge uendelee kuwepo au uondolewe.
hiyo miradi haiwezi kuzinduliwa bila mwenge??
 
Sasa mwenge una umhimu gani? Na uliwahi kuwa na umhimu gani?

Tuanzie hapo?
 
Upotevu wa pesa.. Ina maana kweli hakuliona hilo tangu picha za ujenzi mpaka uzinduziView attachment 2163093
Ana mambo mengi mno makubwa ya kushughulikia, na hivyo haiwezekani kuwa ana notice hadi vitu vingine vidogo vidogo kama hivi ambavyo kiuhalisia, hata watu wengi wa kawaida wanaopita njia hiyo hawawezi kuvi-notice.

Kuna watu wa kawaida tu ambao wanapita njia hiyo kila siku lakini ungewauliza leo kama walishawahi kuona bango la mwenge kwenye daraja hilo, wangeweza kukujibu kuwa hawajawahi kuliona.

Sasa ije iwe Rais? Yaani hata nembo za kwenye mabango nazo awe anakuwa anazijua Rais kuwa zimewekwa mahali fulani?
 
Mwenge ni zindiko na maagano Kati ya nchi na shetani. Ili kuondoa nchi kwenye umiliki wa shetani ni kuanza kung'oa mikabata na maagano yaliyofanywa na wazee ikiwemo shehe Yahya, forozo ganze, Mwalimu na wenzake.
Huyu ganze ni nani
 
Back
Top Bottom