Mh Rais, amesema mwenge uliowekwa katika daraja la Tanzanite uondolewe, na iwekwe alama ya Tanzanite,
Ukiachana na ukweli kwamba Mh Rais akiwa Makamu wa Rais aliona michoro ya daraja hili kabla halijaanza kujengwa, na mwenge ulikuwepo katika michoro, hivyo angeweza kutoa maoni yake na kuzuia mwenge kutengenezwa .
Lakini ukiachana na ukweli kwamba wakati Mh Rais anakabidhiwa kiti cha Urais alijua daraja litakuwa na mwenge, lakini ulikuwa haujawekwa wala kutengenezwa hivyo angeweza kutoa mapendekezo wakati huo na kuzuia mwenge kutengenezwa na kuwekwa.
Pia ukiachana na ukweli kwamba Mh Rais si Mhandisi wa Madaraja , hivyo hajui ule mwenge pale juu kwa sasa baada ya kukamilika kwa daraja , kuondolewa kwake kama kunaweza kuathiri mlinganyo na uzania wa daraja,
Laini pia ukiacha ukweli kuwa gharama zimetumika kuutengeneza ule mwenge na kuuweka juu ya daraja, na anaagiza gharama mpya za kutengeneza jiwe la Tanzanite
HOJA YANGU NI, kwa kauli hii ya Mh Rais, je ni kweli kuwa umuhimu wa mwenge umeanza kupotea machoni mwa wakuu wanchi,?
Je ni wakati muafaka sasa kuuweka mwenge wa uhuru katika JUMBA LA MAKUMBUSHO na kuepuka gharama kubwa ya kuukimbiza nchi nzima.?
Hoja ya mwenge wa uhuru kuwekwa makumbusho imekuwepo kwa muda mrefu sana, hasa gharama zinazoendana na shughuli za kukimbiza mwenge, zinapolinganishwa na matokea ya kuukimbiza.
Je kwa Mh Rais kutaka uondolewe katika daraja la Tanzanite ni ishara kuwa mwenge si tena kielelezo cha kupewa kipaumbele?
#songoka
Vatican katika kwaresma