Je, kila kinachofanyika "kinalenga kufuta Legacy" ya Magufuli?

Inafaa tusikie kwa sasa tunapiga hatua zipi kimaendeleo na kutatua kero za Wananchi.
Legacy ya Magufuli haifutiki,sasa mjikite kutengeneza yenu.
Au kumsema hayati vibaya ndio legacy?
 
Mbona mnatumia nguvu nyingi kumshambulia JPM. Yaani uzembe wenu mnamhusishaje JPM.

Pambaneni na hali zenu. Maana kwa dalili hizi mnazoonyesha hata SSH akitoka story zitakuwa ziezile dhidi yake!
 


Mkuu Bwana PGO,

Vumilia nikushirikishe jambo hivi:-

Unapotoa mada usiwe judgmental yaani usilete mada ambayo tayari umeishakuwa hakimu kwa kuwa unaileta tayari umeishaihukumu, nakunukuu bila ku-edit isimu "Magufuli alipendwa kwakua aliudanganya umma...." pia usiwe mwepesi wa kutangulia kuchafua mada yako mwenyewe kwa maneno ya kejeli, nakunukuu "Tusiwe wajinga kiasi hiki ndugu zangu" aidha epuka kuwa inciteful (usijihalifu mwenyewe kwa uchochezi) acha watu wajihalifu au waihalifu mada alafu wewe uchukuwe nafasi ya Mwalimu uwasahihishe/uwasaidie kwa kuwatengenezea uvumilivu wa hoja mbadala kupitia responses zako kwenye uzi.

Wachangiaji wa mada wanapenda kupewa room ili wao ndiyo watoe mawazo na suluhisho, hivyo unapotaka mada ipate uzi mrefu iweke bila kutangulia kuhukumu wala kukejeli maana GTs walio wengi sana wanajaribu kukwepa sana mada zenye sura na mwelekeo huo. Wewe jiwekee maneno ya akiba ambayo utayatumia kusahihisha mwelekeo wa mjadala pale wachangiaji watakapotaka kupotosha mantiki na muktadha. Mwishoni kule utatumia akiba yako ya dondoo/maneno ya hekima na busara kuhitimisha kwa ama kukubaliana au kupingana na audience yako. Kwa staili hii mkuu utatukosha nyoyo kwelikweli.

Ila mada iko very sensitive, up-to-date, contextual, educative only structure yake ndiyo imeteleza. Kama nimeenda kinyume na matarajio yako basi tuchukuliane mizigo tusonge mbele pamoja mkuu.
 
Hivi Nyerere hana legacy? Mwinyi je? Mkapa nae? Jk je? Acheni masihara. Legacy pekee ya Magufuli ni WATU WASIOJULIKANA, Azory Gwanda na Ben Saanane, Bashite na kugeuka kituko dunia nzima kwa kuaminisha watu kuwa Korona imeisha.
Ficha upumbavu wako
 
Nawezaje kukataa ushauri wa kiistaarabu namna hii? Asante sana, nimelichukua jambo hili kwa uzito unaostahili na Leo ni Siku ya Bwana, barikiwa
 
Mbona mnatumia nguvu nyingi kumshambulia JPM. Yaani uzembe wenu mnamhusishaje JPM.

Pambaneni na hali zenu. Maana kwa dalili hizi mnazoonyesha hata SSH akitoka story zitakuwa ziezile dhidi yake!
Mpwa, acha mahaba, soma uelewe
 
Mkuu una haki ya kumponda hayati Magufuli,kwa miaka nenda rudi tumeshuhudia hakuna mtawala wala kiongozi ameshawahi kupendwa na watu wote kuna watu watamuona shujaa wao,huyo huyo kuna watakaomuona gaidi au jambazi,mtu ka Xi Jiping rais wa china pamoja na kufanya yote china lakini kuna watu wengi tu wanamchukulia kama mkandamizaji wa demokrasia,Vladimir Putin pamoja na effort zake zote nae hajawahi kosa tuhuma nyingi tu za ukandamizaji wa demokrasia na mauaji ya ajabu kwa wahasimu wake.Che guevera wakati katika dunia anaonekana kama symbol ya mapinduzi ya ukandamizaji kwa wamarekani wanamuona kama alikuwa gaidi.Hyo inakwenda mpaka kwa akina Indira Gandhi,Mwal Nyerere (kumbuka kuna watu hawakumkubali na walijaribu kumpindua sio mara moja).Kwa ufupi hakuna kiongozi aliyekuwa mzuri kwa watu wote lazima kuna kundi liliumia katika utawala wake.Saddam Hussein alifanya mengi Iraq lakini uadui wake na wakurd ulipelekea anguko lake so kila mtu atamuenzi kivyake.Yesu mwenyewe hakukubaliwa na wote na ndo maana hata baada ya kifo chake kuna watu palepale hawakukubali kama alifufuka bali wanafunzi wake walimuiba.Mtume mwenyewe hakukubaliwa na kila mtu ndo maana alipigana vita nyingi kuueneza uislam.Namalizia kwa kusema usiwabeze wanaoyashuhudia na kuyasifia mazuri ya Magufuli sababu wao sio vipofu au vichaa wameona kwa macho na akili zao,hvyohvyo hatutawabeza wanaokashfu Magufuli sababu nao wana machungu yao.
 
Yule jamaa alikua anatupeleka wapi sijui,yaani Mwigulu aliapishiwa pale hotelini kwa mkuu,JS hotel.
 
Hivi Nyerere hana legacy? Mwinyi je? Mkapa nae? Jk je? Acheni masihara. Legacy pekee ya Magufuli ni WATU WASIOJULIKANA, Azory Gwanda na Ben Saanane, Bashite na kugeuka kituko dunia nzima kwa kuaminisha watu kuwa Korona imeisha.
Asante Sana Kaka Mkubwa
 
Mpwa, nimeshafanya editing, karibu kwa mjadala huru
 
Inafaa tusikie kwa sasa tunapiga hatua zipi kimaendeleo na kutatua kero za Wananchi.
Legacy ya Magufuli haifutiki,sasa mjikite kutengeneza yenu.
Au kumsema hayati vibaya ndio legacy?
Duniani kote ni ngumu kufuta legacy za mtangulizi wako kwa 100% hata kama alikuwa wa chama cha upinzani. Bado Mhe. SSH anaendeleza kazi kwenye maeneo yafuatayo ambayo yalianzishwa na Magufuli:-
1. Elimu bure (ujenzi wa madarasa pia kwa ela za corona)
2. Afya (ujenzi wa vituo vya afya na zahanati kwa ela za Corona)
3. Usambazaji wa maji.
4. Udhibiti wa demokrasia.
5. Usambazaji wa umeme vijijini.
6. Ukamilishaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo e.g. mabarabara (ikiwemo BRT), madaraja ya nchi kavu na majini, ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa SGR na ukarabati wa MGR kwa upande wa Kigoma.
7. Uendelezaji wa ujenzi wa JNHEPP.
8. Uendelezaji wa ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo mkubwa wa Mbeya-Namanga.
9. Uongezaji wa idadi ya udahili taasisi za elimu ya juu na upanuzi wa kasma ya mikopo ya elimu ya juu.
10. Mabadiliko katika safu ya chama yanayolenga kukiimarisha zaidi.
11. Uendelezaji wa ujenzi wa makao makuu ya nchi ikiwemo Ikulu mpya.
12. Ongezeko la makusanyo ya mapato ya nchi. nk nk nk...

Rais anaongoza nchi kwa Katiba, Sheria, Sera, Kanuni, Miongozo, Itifaki za Kimataifa nk hivyo hayo tunayoona yanabadilishwa, siyo kufuta legacy bali ni ku-plug gaps za utekelezaji wa tools hizo za Katiba, Sheria, Sera, Kanuni, Miongozo na Itifaki za Kimataifa. Kama ni legacy basi ni legacy ya serikali na chama kinachoongoza na siyo legacy ya individual person kwasababu hakuna anayejiweka Ikulu kutawala.
 
Ukweli ni kwamba kuna mambo yalifanyika kwa kutumia mbinu za kibabe na kila unapowauliza watu kuhusu awamu ile unazidi kuwa pandisha hasira zao. Wema hujisemea wenyewe hauhitaji nguvu nyingi kuelezea.

Watu wana huzuni kwa vifo vilivyotokea bila kutolewa ufafanuzi: Azori Ngwanda, Ben Saanane, Alfred Mawazo, Leijabe na wengine wengi waliopotea. Mazingira kama haya yanafuta mazuri yote aliyofanya mtu. Sababu ni ndogo tu ambayo amezalisha yatima na wajane wengi bila sababu ya msingi.
 
Nawezaje kukataa ushauri wa kiistaarabu namna hii? Asante sana, nimelichukua jambo hili kwa uzito unaostahili na Leo ni Siku ya Bwana, barikiwa
Mkuu,
Umeurithi uzima wa milele kwa kuja na mada hii ambayo inaogopeka na wengi, wewe jasiri kama JPM. Keep it up!
Yule jamaa alikua anatupeleka wapi sijui,yaani Mwigulu aliapishiwa pale hotelini kwa mkuu,JS hotel.
Si bora yeye hotelini (a.k.a Ikulu ndogo). Think of mere RC kuapishwa Ikulu na Rais kuapishwa stadium, Ikulu na stadium wapi ni wakfu zaidi? Kibaki aliapishwa usiku wa manane (bendera nchi nzima zikiwa zimeshushwa) Ikulu bila mgeni wa kimataifa hata mmoja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…