mafiakisiwani
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 833
- 616
Pesa ndio sabuni ya roho
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mhhhPesa inaweza kukupa ngono tu kwa mwanamke malaya na sio penzi la dhati. Upo hapo baba?
Anaona sifa mwenyewe, wakati alikua anahongwa buku ten, alafu anasema nayo ni pesaKwa maneno rahisi unatuambia kwamba umeto.mbwa sana,au sio??
Huyu ndio nani mkuu?Adui mmoja ila siku ya jumapili anashinda na jezi za polisi.
Acha kujiona unajua kila kitu USA sio mjinga anajua nini anafanya ndio maana akamuaa aingie kwenye deal la hela na wanamgambo....sasa wewe uko huku wami dakawa unaona usa kafeli hebu jitafakali mkuu mbona unatatalika sana kama mahindi yapo kwenye motoGood evening jamiiforums
Je, kinachoendelea sasa katika nchi tajiri ya Marekani ni uthibitisho kwamba pesa sio kila kitu (Money can't buy everything)?
Marekani ana-sign peace deal na wanamgambo? How comes? Americans have enough cash, fully equipped military/intelligence machinery plus overwhelming political influence lakini bado wanaomba poo?
View attachment 1801477
Marekani (USA) ndio nchi yenye pesa nyingi, teknolojia ya kutisha pamoja na mifumo imara ya ulinzi na usalama hapa duniani ikufuatiwa na mataifa kama China, Uingereza na Ufaransa.
Kwa namna Marekani ilivyo na "assets" za kila namna sikutegemea kabisa kama wange-sign peace agreement na wanamgambo wa Taliban ambao hata ndege vita moja hawana.
Taliban wanapigana kwa kujificha, silaha duni, pesa za kuungaunga na Intelligence gathering mbovu leo wanaingia makubaliano ya kusitisha vita na nchi yenye mihela?
HATA MIMI BADO NINAPENDA SANA PESA
=====
Pesa ni kitu kimoja muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ukosefu wa pesa umefanya watoto kufa mapema sana kwa sababu ya kukosa matibabu stahiki ambayo laiti kama wazazi wao wangekuwa na pesa ya kutosha, wangeweza kuishi muda mrefu zaidi na kufika hata miaka 80.
Umuhimu wa pesa unaweza pia kuonekana linapokuja suala zima la elimu. Mimi ni mmoja wapo wa wahanga wa suala zima la kusoma pasipo kuwa na pesa za kutosha. Ningekuwa na uwezo wangu wa ku-upload vyeti vyangu vya kidato cha nne na sita humu JF mngeshangaa sana.
Matokeo yangu ya mitihani ya vidato hivyo viwili yanatofautiana kwa mbali mno. Nilifaulu kwa alamu za juu kidato cha nne kwa maana shule niliyopangiwa ilikuwa na walimu wazuri waliofundisha kwa juhudi pasipo mtoto kuhitaji kusoma masomo ya ziada.
Kidato cha tano na sita, nilienda kusoma katika shule ambayo ilikuwa ni lazima mwanafunzi asome masomo ya ziada (tuition) ili aweze kufaulu.
Sasa mimi baba yangu atapata wapi pesa ya kunipa nikasoma tuition wakati nguo/t-shirts tu za kuvaa nikiwa nyumbani nilikuwa nazo mbili mpaka watu wamenikariri wakawa wananiita "yule jamaa anayevaaga t-shirt nyekundu".
Kuna kipindi niliacha kabisa hata kwenda kanisani kwa maana nguo ni hizo hizo tu kila jumapili mpaka wasichana wakawa wananicheka.
Siku moja nikiwa kidato cha tano nilienda ofisini kwa mwalimu wa taaluma nililia saaana kama dakika 10 mbele ya yule mama nikamsimulia shida nilizokuwa ninapitia nyumbani kesho yake akaniletea nguo kadhaa za mtoto wake wa kiume.
Keep resting in peace madam Rosemary, sitakuja kukusahau shujaa wangu. Hakika umasikini ni mbaya sana.
Juzi hapa kuna watoto waliuawa wakiwa wameenda kuiba kuku. Just imagine mtoto anauwawa kisa kuku wa 15,000/= tu?
Ndugu zangu madhila ya umasikini ni mengi sana na ninaweza kuandika hata kurasa 1000 zinazohusiana na kadhika ya kutoka katika familia fukara. Nimeishi katika umasikini hivyo ninaujua from A to Z.
Kwa kipindi kirefu sana watu wamekuwa wakihusisha matukio ya uhalifu na viwango vya umasikini huku reference kubwa ikifanywa kutoka katika nchi zilizomo ndani ya bara la Afrika kama vile Tanzania.
Kwa namna nyingine tunaweza kusema kwamba "the higher the the poverty level, the higher the crime rate".
View attachment 1801505
Katika page ya Facebook ya kaka/mdogo wangu Millard Ayo nimekutana na taarifa hii inayohusu maamuzi ya bunge la huko kuruhusu watu kutembea na silaha hata kama hawana vibali kutokana na matukio ya "random shooting" ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika majimbo mbalimbali huko nchini USA;
"Wabunge wa Texas Marekani wamepitisha muswada utakaoruhusu Wakazi wa Jimbo hilo kubeba bunduki na kutembea nazo mtaani hata kama hawana vibali vya kubeba silaha tofauti na sasa ambapo sheria inataka yeyote anaebeba bunduki kuwa na leseni, awe pia na mafunzo ya kuitumia lakini pia historia yake lazima ichunguzwe.
Wanaounga mkono sheria hiyo mpya wanasema itaruhusu Raia wa Texas kujilinda wenyewe huko mitaani na huenda ikasaidia Raia kujibu mashambulizi pale Mtu mwenye silaha anapofyetua risasi bila sababu kwenye eneo la umma kama ambavyo imetokea Watu kuua Watu kanisani, super market na sehemu nyingine za umma"
SWALI: Je, kinachoendelea katika nchi tajiri ya Marekani kwa sasa ni uthibitisho kwamba pesa sio kila kitu (Money can't buy everything)?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kushindwa wameshindwa. Tangu 2001 mpaka sasa hakuna kinachoeleweka? Walifikiri akina Osama waliwashinda Urusi kwa bahati mbaya.Rais wa sasa wa Marekani anapenda suluhu yeye ni Democratic hivyo anaona ni bora kuongea kwanza na sio kuchukua hatua kabla. Sio kwamba wameshindwa hawajwahi kushindwa.
Kuna sehemu nimesema kwamba ninajua kila kitu? Una wivu? Punguza inferiority complex zitakuua mdogo wangu. Acha utoto, man up bro.Acha kujiona unajua kila kitu
Mbona umeandika kwa ku-panic? Hao USA wanakulipa pesa? Au unafanya kazi ubalozini kwako unaogopa kufukuzwa ajira?USA sio mjinga anajua nini anafanya ndio maana akamuaa aingie kwenye deal la hela na wanamgambo....sasa wewe uko huku wami dakawa unaona usa kafeli hebu jitafakali mkuu mbona unatatalika sana kama mahindi yapo kwenye moto
Osama na kundi lake la MujahideenKushindwa wameshindwa. Tangu 2001 mpaka sasa hakuna kinachoeleweka? Walifikiri akina Osama waliwashinda Urusi kwa bahati mbaya.
Hapa ulikuwa unamaanisha nini mkuu?But happiness can't buy yo' ass
Hapo nilikuwa nimequote mistari ya J Cole kuhusu fedha .Wimbo unaitwa " Spark will fly".Hapa ulikuwa unamaanisha nini mkuu?
Biden ana hulka kama ya Rais Samia, wote ni waungwana. Republicans ndio watata sana akina JPM na Trump.Rais wa sasa wa Marekani anapenda suluhu yeye ni Democratic
Poa mkuuHapo nilikuwa nimequote mistari ya J Cole kuhusu fedha .Wimbo unaitwa " Spark will fly".
Thanks bro.Kuna scenatio flani hivi
Tajiri anapokutana na maskini aliyekata tamaa huwa na woga juu ya maskini kwa sababu maskini yeye hajali aidha kama atakufa au la hasa kukitokea mgongano na tajiri
Tajiri yeye sio kwamba anapenda amini hapana bali ni uoga anapotathimini juu ya kuzitumia mali zake kujistarehesha na hapo ndipo anapoogopa kuumia(kimwili)au hata mauti
Nawasilisha