Je, kipaumbele cha CCM ni kuendelea kusalia madarakani au ni kuwaletea maendeleo Watanzania?

Wewe kumbe hupo sawasawa kichwani.

Hivi unaelewa Tume ya Kisheria ya Jaji Warioba ilikuja na jibu gani kutoja kwa wananchi kuhusiana na katiba.

JF inaonekana sasa hivi imekusanya hata watu wenye uelewa duni wakati halikuwa lengo la jukwaa hili.

Ni mwendawazimu pekee ndiye anaweza kuhoji uwepo wa katiba mpya wakati uamuzi ulimwishafanywa na wananchi.
 
Katika mkutano mkuu wa hivi karibuni, uliofanyika kipindi nchi ikiwa na ukosefu wa maji na umeme, hawakuzingumzia kabisa mambo hayo zaidi ya kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao. Uko sahihi
 
Sasa kwa nini huwa hawafanyi huo uchaguzi halali??!
Jibu liko wazi.

Wanajua kuwa Katiba iliyopo, ndiyo inayowapa wao CCM uhakika wa kuendelea kubaki madarakani, kinyume Cha hapo Taifa litakapopata Katiba mpya, ambayo pia itaweka utaratibu wa kupata Tume huru ya uchaguzi, itakuwa ndiyo mwisho wa utawala wao
 
Ilo jina likitajwa linatusaidiaje?.Hizo ni vibe tu wala hakuna cha maana.Inaonekana ata wewe hujielewi.
 
Thumuni kuu la chama cha siasa ni kuingia ikulu! Mengine baadaye! Hivyo dhumuni kuu la chama cha siasa kinapokuwa madarakani ni kubakia madarakani
 
Mlamba asali wewe. Nyie ndio watu wazuri ambao hamtakufa.
 
Haya yote ni matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere
 
Hebu tujiulize ni kwanini serikali ya CCM inapata "kigugumizi" kikubwa Sana kutengeneza Katiba mpya itakayoendana na mfumo wa vyama vingi?
Inajua wazi kuwa kwa uovu na ukatili wao ikiwepo katiba mpya ccm haichukui round kuwa chama cha upinzani!
 
Thumuni kuu la chama cha siasa ni kuingia ikulu! Mengine baadaye! Hivyo dhumuni kuu la chama cha siasa kinapokuwa madarakani ni kubakia madarakani
Siyo kweli........

Dhumuni kuu la chama kinachotawala duniani kote, ni kuwatumikia wananchi wake Kwa ufanisi mkubwa, hayo mengine yanafuatia
 
Siyo kweli........

Dhumuni kuu la chama kinachotawala duniani kote, ni kuwatumikia wananchi wake Kwa ufanisi mkubwa, hayo mengine yanafuatia
Tatizo lenu nyie ni wabishi. Mnalazimisha njozi zenu ziwe ni uhalisia. Uanaharakati unawazidi nguvu.

Narudia dhumuni Kuu la chama cha siasa ni kuingia Ikulu. Kikishaingia Ikulu ni kuhakikisha kinaendelea kutawala. Watu wenye mawazo mgando kama wewe ndiyo wanaangusha upinzani Tanzania. Huwezi kumshinda adui bila kumfahamu! Chadema inaangushwa na nyie wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…