Exorcist
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 1,243
- 1,279
Msaada. Tuseme kiwango cha mwisho cha miamala cha line yangu ya Airtel ni 5mil. Halafu nikatuma 4.5mil. kwenda mtandao mwingine, halafu kutokana na shida ya mtandao hiyo pesa ikarudishwa kwangu.
Kisha nikajaribu kuituma kwa namba ya mtandao mwingine, lakini naambiwa kwamba umefikia kiwango cha mwisho cha miamala, je, inamaanisha pesa ile iliyorudishwa kwa ukamilifu kwangu badi inahesabika kama muamala uliofanyika kwa ukamilifu na hivyo kiwango cha miamala nilichobakiza ni laki tano tu ndio naruhusiwa kutoa?
Sasa cha kushangaza, kupiga huduma kwa wateja mara ya kwanza, akaniambia kwa kuwa pesa imerudishwa kwako , kikomo chako cha miamala bado ni 5mil, hivyo jaribu kumuuliza huyo unaemtumia kama line yake imefika kikomo, lakini haikuwa hivyo; nikajaribu kutoa hicho kiwango direct kwa wakala wa airtel , lakini jibu ni lile lile, ‘UMEFIKIA KIWANGO CHA MWISHO CHA MIAMALA’.
Nikapiga tena mara ya pili, huyu wa mara ya pili akaniambia kwamba ule muamala uliorudishwa unahesabika kama muamala, hata kama haukufanikiwa na pesa imerudishwa kwako, hivyo kikomo cha miamala cha siku kimepungua, hivyo nisubiri hadi kesho. Wahudumu wawili wa kampuni hiyo hiyo wananipa majibu tofauti ndani ya nusu saa.
SWALI: Kikomo cha miamala cha siku ni ‘MIAMALA ILIYOFANIKIWA’ au hata ile iliyorudishwa?
Sasa kama muamala haukufanikiwa mimi inanisaidia nini hiyo pesa niliyorudishiwa na siwezi kuitoa wala kuituma?
Hivi wakitufanyia hivi watu milioni 1, na wakahodhi pesa za watu, lets say bilioni 100 hata masaa 24 tu, kwenye kausha damu zao zile za Bustisha nakadhalika, hiyi si inaingiza hata bilioni 10 za ziada?
Lakini pia kwa upande wa mteja hata ni maumivu, hata kama ni biashara ndio imeshakwama, au unaweza ukaitwa hata tapeli kwa hutaki kulipa unasingizia kikomo…,
Inaumiza sana