Je, Kobe Bryant alikuwa sahihi kumkiss mdomoni mwanae wa kike?

Je, Kobe Bryant alikuwa sahihi kumkiss mdomoni mwanae wa kike?

Haya mambo magumu sana lakini pia mepesi sana. Inategemea unayachukuliaje maisha. Unaweza kujikuta haufanyi lolote la maana kwa kuwaogopa watu.

Cha msingi ishi maisha unayoyataka wewe ilimradi usikwaze wrngine au kuvunja taratibu za nchi. Haitakaa mtu awaridhishe watu wote kwa wakati mmoja, haiatokea.
Watu tunamalezi yanatofautiana na tumepitia maisha tofauti, usitegemee tutaona mambo kwa mtizamo sawa, haitatokea.

Kama huyo mnigeria anasema kifo ni adhabu kwa hilo kosa la kubusiana, na hao wengine waliokuwapo kwenye ndege je?
Ikiwa hilo kosa limeondoa uhai wao, inamaana wao ndio wamefanya dhambi kubwa kabisa ikabidi waondolewe wabaki watakatifu duniani?
 
Nawashangaa sana watu wanaokurupuka na kusema jambo ni sahihi eti kisa wale wanaofanya vile ni watu wenye utamaduni wa kizungu,na wakati huo huo utamaduni wa muafrika ukapitwa na wakati.
Kinachoonekana katika picha ni ujinga,nasema kwa suati kubwa NI UJINGA.
 
Kobe hakuwa na tabia nzuri, alikuwa na tabia mbaya sana, mzinzi wa kutupwa, alishawahi kushtakiwa kwa kubaka, hata mkewe alitaka kumuacha kwa umalaya wake.

Kushtakiwa kwa kubaka ni kigezo cha kua na tabia mbaya? What if kasingiziwa?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Desturi mkuu. Ukikutana na demu wa kijapan anaweza funguka sana kwako hadi ukadhani kakupenda, kibongobongo utataka kumtokea. Kumbe yeye wala hana hisia zako za kibongo.
Inawezekana kweli hilo jambo?
 
Sijasikia kuwa marehemu kaacha mjane na watoto kadhaa. Hata picha ya mkewe akiwa kwenye majonzi sijaiona mitandaoni, jambo ambalo si kawaida kwa watu maarufu kama kobe.

Zipo mnyampaa, inategemea unazitafutia wapi. Lakini pia misiba ya wenzetu iko tofauti na yetu tunavyoomboleza.
 
mtoto mwisho kumkiss hivyo ni miaka 4, lakin akishafikisha miaka 10 tayar ameshavunja ungo, hiyo ni tabia chafu, unamfundisha uhuni

Nafikiri haifai kabisa kumkisi mtoto mdomoni kwani tuna bacteria wengi mdomoni ambao wanaweza kumpa maradhi mtoto
Pia sio vizuri kuanza kumfundisha mtoto hivyo halafu baadae ukimkuta analiwa denda unaanza kulalama wakati chanzo ni wewe
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hahaha yupo sahihi mno Sema ma Mila na destuli ya Africa yaliyo tufanya tukawa wajinga weusi mpaka ubongo hayakuruhusu iyo kitu imagine Leo hii huwez Ata kumkiss mke wako mbele za watu Sasa je uyo mtoto unaanzaje? [emoji848][emoji848]

Kuna maradhi ambayo unaweza kumuambukiza mtoto
Halafu kuna njia nyingi za kuonyesha upendo kwa mtoto na kiss ya mdomoni sio moja wapo


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom