theprogrammer C++
Senior Member
- May 17, 2013
- 150
- 385
Kwa juu juu, story inaeleweka kabisa. Shekilango imekuwa ndogo, magari mengi, traffic inakuwa balaa na katikati ya Dar tunajibana . Kwa hiyo RC akaamua: "Wote Magufuli Stand!" Lakin je kuna lolote nyuma ya pazia?
Kuna angle nyingine nimeiwaza
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kampuni ndogo ndogo za mabasi zikikua kwa kasi. Kampuni ambazo zamani zilikuwa zinaonekana kama "wadogo" zimeanza kuleta huduma za kisasa, mabasi mazuri, VIP/luxury services, booking za online, ofisi zao wenyewe na kadhalika.
Kwa kifupi, wadogo wameanza kuwafuata wakubwa kwenye mchezo wao wenyewe.
Kampuni kubwa ambazo kwa miaka mingi zimekuwa na dominance kwenye luxury transport zikaanza kuona ushindani ukiongezeka. Yaani zamani ukitaka luxury bus unaangalia wale wale watu.
Leo hii?
Unakuta kampuni ambayo juzi tu ulikuwa huijui imeleta basi jipya, limejaa charging ports, AC, Wi-Fi, viti vya kulalia, uniform kali na dereva anaongea kama captain wa ndege.
Na mbaya zaidi, hawa wadogo wameanza kuwa na ofisi zao Shekilango, wanakusanya abiria pale pale, wanauza tickets, wanajenga customer base yao na taratibu wanakuwa brand.
Kama Shekilango imefungwa kama kituo cha mabasi, nani anaumia zaidi?
Kampuni kubwa ambazo tayari zina jina, routes, customers na uwezo mkubwa wa kuhamia Magufuli?
Au kampuni ndogo ambazo zilikuwa zimejenga biashara zao taratibu kuzunguka eneo la Shekilango?
Hapo ndipo unaweza kuanza kujiuliza kama hii movement ina athari ya pili ambayo haizungumzwi sana.
Kwa sababu Magufuli Bus Stand si sawa na kuwa na ofisi yako pale Shekilango.
Kampuni kubwa zina uwezo wa ku-adapt haraka. Zina resources, branding, booking systems, fleet kubwa na customer base iliyokwisha jengwa.
Lakini kampuni ndogo?
Mteja ambaye alikuwa anapita Shekilango, anaingia ofisini, anaona basi, ana-book ticket, anaondoka...
Sasa anapaswa kwenda Magufuli.
Na Magufuli Stand ni battlefield nyingine kabisa.
Hapo ndipo wale wenye jina kubwa, mabasi mengi na network kubwa wanaweza kuwa na advantage.
Kwa hiyo, bila hata kusema kwamba kuna mtu alisukuma agizo hili na sina ushahidi wa kusema hivyo lakini commercially, hii movement inaweza kuwa na matokeo ambayo yanafanana sana na kile ambacho kampuni kubwa zingependa kuona:
ushindani mdogo.
Ni kama ligi imehamishwa kutoka uwanja mdogo kwenda uwanja mkubwa, halafu ukigundua kwamba kwenye uwanja mkubwa wale wenye timu kubwa ndio wenye uwezo wa kukaa dakika 90 bila kuchoka.
Na kitu kingine kinachonifanya nicheke ni kwamba....Wakati mwingine regulatory decision inaweza kuwa na sababu halali kabisa... lakini unintended consequences zake zikawa nzuri sana kwa mtu mwingine.
Sasa sijui kama hii ni coincidence tu, au ni "business chess" iliyochezwa vizuri sana.
Jamii Forum wenyewe mnaonaje?