N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Wanabodi katika jamii yetu, taasisi za dini zimekuwa zikitarajiwa kuwa mfano wa maadili mema, uadilifu, uwajibikaji na haki.
Hata hivyo, katika miaka ya karibuni kumekuwepo na malalamiko ya wazi na ya siri kuhusu baadhi ya viongozi wa dini kujihusisha na vitendo vinavyokwenda kinyume na misingi ya imani—ikiwemo kuiba au kutumia vibaya mali za taasisi ya dini, kudanganya waumini, kutoweka wazi matumizi ya rasilimali za taasisi zao kv fedha,magari nk, au kuendeleza migogoro ya ndani kwa sababu ya fedha na rasilimali.
Hali hii imeibua swali nyeti: je, kukosekana kwa uadilifu wa kitaasisi ndani ya taasisi za dini ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wanaume wengi kukwepa kushiriki ibada?
Kwa kawaida, wanaume wengi huthamini uwazi, haki na mantiki.
Wanaposhuhudia migogoro ya mara kwa mara ya uongozi, matumizi mabaya ya fedha za sadaka au michango, au viongozi wanaohubiri mema lakini vitendo vyao ni kinyume na wanachofundisha, huanza kupoteza imani si tu kwa kiongozi bali kwa taasisi nzima.
Matokeo yake, baadhi huamua kujitenga na ibada au dini kwa ujumla, wakiona taasisi imepoteza uhalali wa kuwa mwongozo wa maadili.
Kwa msingi huo, taasisi za dini zinapaswa kuwa mfano bora wa uadilifu wa kitaasisi:
Bila kuboresha uadilifu kama unavyohubiriwa, hatari ya kupoteza uaminifu wa waumini—hasa wanaume—itaendelea kuongezeka.
Tulibaha mwa-n'yadikwa
MODS NIREKEBISHIENI TITLE NENO 'KITAALUMA' LIONDOKE MKONO ULITELEZA

- Kuwa na mifumo wazi ya usimamizi wa fedha na mali
- Uwajibikaji wa viongozi kwa waumini
- Kutatua migogoro kwa haki na busara
- Kuishi wanachohubiri