haya ni maoni yangu mkuu, leta yako tujadili na ndio essence ya kuwa na JF. Neno 'forum' maana yake ni jukwaa ambalo watu hukutana hapo na kujadili masuala. Leta hoja yako tuijadili, hayo ni maoni yangu halisi!''Kwa kawaida, wanaume wengi huthamini uwazi, haki na mantiki.'' Huu utafiti ni wako au umeupata wapi? Mauaji ya 29/10 wengi ya waliokuwa mitaani wanaua raia walikuwa ni wanaume ''wanaothamini haki'' kwa mujibu wa maelezo yako.
Maadili kwa taifa hilini mzozo unaochemka kwa kasi kubwa mno,sii kwa viongozi ambao walifaa kuliongoza taifa kwa mfano bora wakuliongoza taifa nao kwenye maadili yapo mashaka.Wanabodi katika jamii yetu, taasisi za dini zimekuwa zikitarajiwa kuwa mfano wa maadili mema, uadilifu, uwajibikaji na haki.
Hata hivyo, katika miaka ya karibuni kumekuwepo na malalamiko ya wazi na ya siri kuhusu baadhi ya viongozi wa dini kujihusisha na vitendo vinavyokwenda kinyume na misingi ya imani—ikiwemo kuiba au kutumia vibaya mali za taasisi ya dini, kudanganya waumini, kutoweka wazi matumizi ya rasilimali za taasisi zao kv fedha,magari nk, au kuendeleza migogoro ya ndani kwa sababu ya fedha na rasilimali.
Hali hii imeibua swali nyeti: je, kukosekana kwa uadilifu wa kitaasisi ndani ya taasisi za dini ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wanaume wengi kukwepa kushiriki ibada?
Kwa kawaida, wanaume wengi huthamini uwazi, haki na mantiki.
Wanaposhuhudia migogoro ya mara kwa mara ya uongozi, matumizi mabaya ya fedha za sadaka au michango, au viongozi wanaohubiri mema lakini vitendo vyao ni kinyume na wanachofundisha, huanza kupoteza imani si tu kwa kiongozi bali kwa taasisi nzima.
Matokeo yake, baadhi huamua kujitenga na ibada au dini kwa ujumla, wakiona taasisi imepoteza uhalali wa kuwa mwongozo wa maadili.
Kwa msingi huo, taasisi za dini zinapaswa kuwa mfano bora wa uadilifu wa kitaasisi:
MY TAKE:
- Kuwa na mifumo wazi ya usimamizi wa fedha na mali
- Uwajibikaji wa viongozi kwa waumini
- Kutatua migogoro kwa haki na busara
- Kuishi wanachohubiri
Bila kuboresha uadilifu kama unavyohubiriwa, hatari ya kupoteza uaminifu wa waumini—hasa wanaume—itaendelea kuongezeka.
Tulibaha mwa-n'yadikwa
Ni changamoto sana kaka. Nadhani hata kukosekana kwa maadili kwenye taasisi nyingine kunatokana na mfano usio mzuri kutoka kwenye baadhi ya taasisi zetu za dini ambazo zilifaa kuwa mfano...binafsi nimeshuhudia zaidi ya mara tatu fedha zilizochangwa kwa ajili ya mradi husika ndani ya taasisi fulani ya kidini zikipigwa waziwazi na hakuna lililofanyika na hakuna mtu wa kuhoji, ukihoji unapewa mfano wa Miriam na Haruni against Musa kwamba unawakosea viongozi wa dini!!!Maadili kwa taifa hilini mzozo unaochemka kwa kasi kubwa mno,sii kwa viongozi ambao walifaa kuliongoza taifa kwa mfano bora wakuliongoza taifa nao kwenye maadili yapo mashaka.
Don't generalize things! Be specific about that religious institution.Wanabodi katika jamii yetu, taasisi za dini zimekuwa zikitarajiwa kuwa mfano wa maadili mema, uadilifu, uwajibikaji na haki.
Hata hivyo, katika miaka ya karibuni kumekuwepo na malalamiko ya wazi na ya siri kuhusu baadhi ya viongozi wa dini kujihusisha na vitendo vinavyokwenda kinyume na misingi ya imani—ikiwemo kuiba au kutumia vibaya mali za taasisi ya dini, kudanganya waumini, kutoweka wazi matumizi ya rasilimali za taasisi zao kv fedha,magari nk, au kuendeleza migogoro ya ndani kwa sababu ya fedha na rasilimali.
Hali hii imeibua swali nyeti: je, kukosekana kwa uadilifu wa kitaasisi ndani ya taasisi za dini ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wanaume wengi kukwepa kushiriki ibada?
Kwa kawaida, wanaume wengi huthamini uwazi, haki na mantiki.
Wanaposhuhudia migogoro ya mara kwa mara ya uongozi, matumizi mabaya ya fedha za sadaka au michango, au viongozi wanaohubiri mema lakini vitendo vyao ni kinyume na wanachofundisha, huanza kupoteza imani si tu kwa kiongozi bali kwa taasisi nzima.
Matokeo yake, baadhi huamua kujitenga na ibada au dini kwa ujumla, wakiona taasisi imepoteza uhalali wa kuwa mwongozo wa maadili.
Kwa msingi huo, taasisi za dini zinapaswa kuwa mfano bora wa uadilifu wa kitaasisi:
MY TAKE:
- Kuwa na mifumo wazi ya usimamizi wa fedha na mali
- Uwajibikaji wa viongozi kwa waumini
- Kutatua migogoro kwa haki na busara
- Kuishi wanachohubiri
Bila kuboresha uadilifu kama unavyohubiriwa, hatari ya kupoteza uaminifu wa waumini—hasa wanaume—itaendelea kuongezeka.
Tulibaha mwa-n'yadikwa
MODS NIREKEBISHIENI TITLE NENO 'KITAALUMA' LIONDOKE MKONO ULITELEZA
Mkuu nimekuelewa. Kmbe siyo utafiti ila ni maoni yako. Na mimi ndiyo nimetoa maoni yangu kuwa sikubali kuwa wanaume wanapenda haki kuliko eg . wanawake.haya ni maoni yangu mkuu, leta yako tujadili na ndio essence ya kuwa na JF. Neno 'forum' maana yake ni jukwaa ambalo watu hukutana hapo na kujadili masuala. Leta hoja yako tuijadili, hayo ni maoni yangu halisi!
Kamuulize mwamposa atakuambia anaingiza milion ngapi kwa mwezi.kumbe dini imekuwa biashara mkuu