Je, kulikuwa na ulazima wa nchi kuingia vitani na Idd Amin?

Je, kulikuwa na ulazima wa nchi kuingia vitani na Idd Amin?

Mtukudzi

Senior Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
103
Reaction score
408
Nawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?

Je, hatukuwa na diplomacy iliyokuwa matured kuepusha hasara ile?

Je hatukuwa na jeshi imara la kuwafurusha wavamizi wa mipaka yetu kimya kimya bila kutangaza vita?

Nisaidieni wazee wangu
 
Baada ya vita tuliishi maisha magumu sana vitu madukani ilikuwa hamna pia dawa hospitalini zikawa hamna kabisa magonjwa ya kuambukiza tukawa tunapona tu kwa usugu wa miili yetu, ndo maana CORONA haijatusumbua maana hali hiyo inakuja ilikuta tuna corana teyari.

Vita vya kumtoa Idd Amin aliyevamia sehemu ya nchi yetu ilikuwa ni lazima , sema ya kumfukuza na kumnyang`anya Uganda yote ndo haikuwa ya lazima na ndiyo iliyotufirisi. Tuliwezeshwa tu kumshinda na Waganda wenyewe maana waliisha mchoka Idd Amin kabisa,
 
Nawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?...
Unajua Idd Amin alikuwa ni mwanaharakati kama Tundu Lisu na aliingizwa jeshini kwa nguvu na siyo kwa hiyari yake.

Sasa watu wa aina ya Amin hawakomagi uchokozi na dawa yao ni kichapo tu hakuna namna bwana mdogo!
 
Odd amini alikuwa bogus Sana japo alikuwa na speech nzuri Sana Kama intelligent fulani hivi
 
Nawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?...
Uchumi ulishaanguka na viwanda vilishaanza kudorora njia rahisi ya kuepuka mgogoro wa ndani ilikuwa ni kuingia vita za nje ili kuepuka sokomoko. Na baada ya vita ilitarajiwa Obote arejeshe mgawo alau tupunguze machungu na haikuwa hivyo maana nae alikuwa na njaa...
 
Tuliwezeshwa tu kumshinda na Waganda wenyewe maana waliisha mchoka Idd Amin kabisa,
Hii ndiyo hoja ya msingi. Idd Amin alipigwa na waganda. Sisi tulisaidia. Waganda walikuwa wamemchoka, hata wanajeshi wake walikuwa hawana pa kusemea, ilipopatikana opportunity wakaitumia!.............kama picha uliyoiona kwa support ya Lisu kwenye mikutano, it sent a special msg ingawa watu , many of them could not figure out this!
 
kama mzee nyerere alivyosema..
Sababu tunayo, Uwezo tunao na Nia tunayo.

ndo ivyo tukamtia adabu idd dada na kuwakomboa waganda kwa utawala ule, ila yaliyoendelea tusingeweza kuyazuia.
 
Hii ndiyo hoja ya msingi. Idd Amin alipigwa na waganda. Sisi tulisaidia. Waganda walikuwa wamemchoka, hata wanajeshi wake walikuwa hawana pa kusemea, ilipopatikana opportunity wakaitumia!.............kama picha uliyoiona kwa support ya Lisu kwenye mikutano, it sent a special msg ingawa watu , many of them could not figure out this!
Kabisa
 
Back
Top Bottom