Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani hakukuwa na ulazima maana kilichomfanya Idd Amini avamie nchi yetu ni hofu ya Obote ambae baada ya kupinduliwa alikimbilia kwetu tzNawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?
Je, hatukuwa na diplomacy iliyokuwa matured kuepusha hasara ile?
Je hatukuwa na jeshi imara la kuwafurusha wavamizi wa mipaka yetu kimya kimya bila kutangaza vita?
Nisaidieni wazee wangu.
There you are!!Ilikuwa sio lzm kuingiza nchi kwa interest ya Nyerere na Obote
Haaa wapi!Odd amini alikuwa bogus Sana japo alikuwa na speech nzuri Sana Kama intelligent fulani hivi
Mwana kulitafuta mwana kulipata.
Tuliingia vitani kwa sababu tulitengeneza mazingira ya kukwaruzana na Field Marshall Iddi Amin Dadah
1.Amini Alimpindua Milton Obbote akiwa kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola.
2.Mwalimu Nyerere akamkaribisha Obbote aishi Tanzania.
3.Nyerere aliapa kutoitambua serikali ya Iddi Amin.
4.Wafuasi wa Obbote wakaanzisha Vita ya msituni wakiwa Tanzania.
5.Amin akashtukia mipango hiyo ndio mwanzo wa border crash za 1971 na 1972.
6.Iddi Amin alijaribu njia zote kumshawishi Mwl.Nyerere wafanye mahusiano mema lakini Mwl.Nyerere hakuwa na nia dhati ya kushirikiana na Amin.
7.Mauaji ya halaiki na ya kikatili ubakaji,kufukuza wahindi zaidi ya elfu 70 ulilaaniwa na mataifa mengi na kumpa Mwl.Nyerere sababu ya kumuodoa Amin kwa Nguvu.
8.Kilichofuata ni vita vya Kagera, Majeshi ya Amin yalivamia maeneo ya Mkoa wa Kagera na kuyatwaa.Mwl Nyerere alitangaza vita akayadunda na kuyasambaratisha Majeshi ya Amin yaliokuwa yanasaidiwa na Gaddafi.
9.Majeshi ya Amin yalisalim amri,Amin akatoroka kupitia mpaka wa Kenya.
10.Baada ya vita IMF,World Bank walitaka Mwl.Nyerere abadirishe sera za biashara, viwanda,Uchumi na Utawala bora Mwl.Nyerere aliyakataa mapendekezo hayo tukawekewa vikwazo vya kiuchumi .
11.Nchi iliyumba kiuchumi,hali ngumu ikakumba wananchi,ukosekana wa vyakula,petrol, Sabuni,nguo,madawa, upatikanaji wa vipuli uilikuwa vya shida viwandani,njaa ilikuwa shida kweli kweli.
12.Ilifika vitendo vya kumuondoa Mwl.Nyerere madarakani valipata kasi kubwa.
13.Mwisho Mwl.Nyerere akasalim amri,akangatuka uraisi 1985.
Hatukuwa na ulazima wowote na wala Amin hakuwa na makosa yeyote bali ni Mwalimu kutaka tu kumrudisha rafikiye Obote. Vita ilikuwa na maslai ya kirafiki kati ya Nyerere na Obote. Na watawala wengi duniani wamezigharimu nchi zao kwa masilai yao binafisi. Ndo maana baada kumtoa Amin waliwekwa maraisi takribani 3 na baadaye Obote akarudishwa kutawala uganda. Sema tu walikosana tena na mwalimu wanadai eti alilipa visasi.
Mtu anachukua sehemu ya ardhi yetu na kutaka kuitawala Kijeshi halafu wewe huchukui hatuna yeyote? Fashisti na Dikteta Idd Amin Dada alipata alichokitafuta. Kwa hili sisi Wahenga hatukua na simile. Tulimfuata hadi ndani ya nchi yake na kumfurusha hadi akatokomea na kufia huko Uarabuni.Ni ngumu sana kufikiria kufanya diplomasia na dikteta, diplomasia pekee ilikuwa kuichukua uganda mazima
Mtu anaingia ndani ya nyumba yako anaua watoto wako na ku baka mkeo, halafu wataka diplomasia?Nawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?
Je, hatukuwa na diplomacy iliyokuwa matured kuepusha hasara ile?
Je hatukuwa na jeshi imara la kuwafurusha wavamizi wa mipaka yetu kimya kimya bila kutangaza vita?
Nisaidieni wazee wangu.
Hiyo Diplomasia itatokea wapi wakati tayari Idi Amin Dada kwa Kusaidiwa na Libya walishaelekeza 'Makombora' yao katika Hospitali ya Bugando Mwanza huku wakiwa wameshawauwa baadhi ya Watanzania wenzetu hasa Mkoa wa Kagera ( Bukoba ) kwa Watani zangu Wahaya?Nawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?
Je, hatukuwa na diplomacy iliyokuwa matured kuepusha hasara ile?
Je hatukuwa na jeshi imara la kuwafurusha wavamizi wa mipaka yetu kimya kimya bila kutangaza vita?
Nisaidieni wazee wangu.
Bwashee, Idd Amin aliingia jeshi la mkoloni kwa hiari yake Kama mpishi.Unajua Idd Amin alikuwa ni mwanaharakati kama Tundu Lisu na aliingizwa jeshini kwa nguvu na siyo kwa hiyari yake.
Sasa watu wa aina ya Amin hawakomagi uchokozi na dawa yao ni kichapo tu hakuna namna bwana mdogo!
Ni paradoxical!Haaa wapi!
Huwezi kuwa bogus kisha ukawa na speech nzuri sana!
Aise hiyo isingekubalika na OAU/UN kwa sababu tayari Uganda ilikuwa ni nchi huru, hivyo ingepelekea kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.Walikosea strategy, uganda ilitakiwa kufanywa jimbo chini ya Tanzania kwa miaka angalau 30 kabla ya kupewa uhuru.