Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,996
- 3,950
Nawauliza wazee wangu mliokuwa na ufahamu wakati nchi inaingia kwenye vita vya Kagera. Je, kulikuwepo na ulazima wa kuingiza nchi kwenye vita ya Uganda ambayo tangu wakati huo mpaka sasa madhara yake bado yapo dhahiri?
Je, hatukuwa na diplomacy iliyokuwa matured kuepusha hasara ile?
Je hatukuwa na jeshi imara la kuwafurusha wavamizi wa mipaka yetu kimya kimya bila kutangaza vita?
Nisaidieni wazee wangu
Mjomba, ni ngumu sana kufanya Diplomasia na dikteta. Ukishakuwa Dikteta Maana yake chaguo lake ni USHINDI tu, hivyo diplomasia pekee ilikuwa ni kumuacha Amini afanye anavyotaka yeye.
Hiyo kitu hata mimi nisingeweza kukubali.
Sidhani kama ameshawahi kutokea Rais mwenye Diplomasia kama Mwalimu, Mwalimu was a good listener na alikuwa muelewa sana. Amin alikuwa stupid and ignorant feeding his little ego
Uamuzi wa Mwalimu ulikuwa ni sahihi kwa wakati wake hata kama kwa sasa unaonekana haukuwa sahihi.
Uamuzi wa Azimio la Arusha ulikuwa ni sahihi kwa wakati ule hata kama kwa sasa unaonekana haikuwa sahihi.
Leo Hii ukiangalia Utajiri wa JK na watoto zake, viongozi wakuu wa Serikali, utajiri wa Mkapa na Mke wake , Utajiri wa JPM na viongozi wake utaelewa umuhimu wa Arusha Declaration.
Mwalimu will remain the best ever