Paskali anaweza kutukumbusha majina matatu kwenye kinyang'anyiro cha kugombea uspika 2005.
Nakumbuka CC ya CCM Rais Mkapa akiwa anaondoka madarakani ilipeleka majina 3.
1. Pius Msekwa (Spika alikuwa anatetea nafasi yake)
2. Samuel John Sitta (Mbunge wa Urambo)
3. ............... (nadhani alikuwa Eliab Abihudi kama nimesahau naomba kusahihishwa)
2010 wagombea kiti cha Spika walikuwa 8.
Hii style ya kuja na jina moja tu, haijakaa kidemokrasia hata kidogo.
Maamuzi ya vikao vya CCM ni ya mwisho na hakuna mahakama ya ku-challenge walichoamua. Isipokuwa kuna mahakama ya ndani ya mioyo ya wanadamua na mijadala vijiweni, yaani kati ya watu 70 aliorejesha form, ni mtu mmoja tu ndio ana sifa?
Kwa sasa inaweza kuonekana ndio "demokrasia yetu" ila inapanda mbegu ambayo kuna siku badala ya kupata kiongozi bora kwa merits zake, tutapata bora kiongozi kwa kuwa "tumemwona, anaweza" ila hata hao wanaosema "wanamwona anaweza" angeingia kwenye box la kura say kwenye party caucus, huenda angeangukia pua au kama angeshinda, unaona mchakato aliopitia unlike ile ya mama Makinda kupewa kwenye silver plate kwa kuwa safari hii ni zamu ya akina mama. Kwa maamuzi yake JK yeye kama mkiti wa vikao vya uteuzi ali-set a precedence ambayo inawatuliza watu, ila mioyoni wanabaki na maswali ambayo hayana majibu.
Anyway, acha bendera ipepee.
Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote