Chaz Joe
Member
- Jul 3, 2019
- 12
- 38
Habari zenu wadau!, nahitaji ufafanuzi kidogo hapa, nilikuwa na Girlfriend wangu ambaye alipata ujauzito na kuniambia kwamba ni ujauzito wangu. Tangu hapo niliamua kwa upendo tu kumhudumia katika kipindi chote cha ujauzito hadi alipojifungua. Japo sikuwa naishi nae lakini nilimpatia mahitaji yote aliyokuwa akiniambia. Baada ya mtoto kuzaliwa, niliendelea kumhudumia hadi akafikisha umri wa miaka 10.
Sasa naona mwanamke huyu amebadilika mno na anatumia hiyo kama fursa ya kunikandamiza, maana anadai matumizi ambayo ni makubwa kiasi cha kunifanya nione kabisa ananitumia kwa masilahi yake kwa kisingizio cha mtoto.
Basi baada ya hayo, nikaona suluhisho ni mimi kumchukua huyo mtoto nikae nae, nimhudumie mimi mwenyewe. Lakini mama yake aligoma, kilichofuata hapo ikawa ni migogoro daily.
Wakati migogoro hiyo ikiendelea, ndipo mama wa mtoto ananiambia kuwa huyu sio mtoto wangu, kitu ambacho kimeniuma sana na kunivunja moyo. Nikapatwa na hasira sana
Sasa nimeleta hili suala kwenu wadau mnisaidie, je kuna sheria yoyote ya kudai fidia kwa gharama zote nilizotoa kumlea huyu mtoto kwa kipindi chote hicho, hadi kufikia hapo ambapo mama yake anadai kuwa sio mtoto wangu?? Na kama ipo sheria ,je utaratibu upoje??