Je, kuna fidia yoyote ya kulea mtoto wa kusingiziwa?

Je, kuna fidia yoyote ya kulea mtoto wa kusingiziwa?

kazaa roho tu mjomba mbona tunafuga mbwa na tunamhudumia na watoto wake sembuse mtu
 
Panga jipya pamoja na kulinoa, haizidi 15,000/-
Kwa hiyo wwe unataka watu wagawane majengo ya serekali!? Mmoja Mortuary na mwingine gerezani ndiyo utafurahi!!??
 
Hii dunia utadai vingapi? Kuna vitu unasema swala then unapotezea
 
Kapime DNA, halafu kadai fidia. Hii itakuwa fundisho kwa wale wote wenye tabia Kama yake pia itasaidia wale wanaojichukulia Sheria mkononi kujua njia mbadala.
 
Sina uhakika, wala sio kama nina shida saana na hizo pesa, ila nilitaka apate fundisho tu , mana ana dharau na kiburi sana huyu mwanamke
basi ngoja nikeambie....kaa nae mbali kaa kimya mshukuru Mungu.
mtoto kadiri anavyokua na matumizi yanaongezeka flani hivi hasa ada za shule...hata kama Binti anafanya kazi atakurudia tu.

na hata akikupeleka ustawi, zingatia ushahidi wa kwamba huyo mtoto si wako.

Tulia Lea watoto wengine au huna???
 
ukweli umekuweka huru,
si kwamba wema wako umekuponza, bali umejiwekea hazina mbinguni,

umetekeleza wajibu wako ipasavyo kama baba mwema, bora sana muwajibikaji.

Hujapoteza kitu gentleman kwa malaika huyo japo ni kwa hadaa za Delilah, huo ni uwekezaji wa Neema, kwa ukarimu. Unayo hazina mbinguni.

Huna haja ya kubababika,
Umetenda wema, sasa nenda zako kwa amani.

Neema na Baraka za Mungu ziambatane na kuandamana nawe daima,
aimen🐒
Umepata ushauri wa kikubwa hili ndo uishi nalo hakuna la zaidi wala hakuna cha fidia!!! Kaa kwenye ushauri huu wa mdau.
 
Mkuu hii kitu inatia hasira sana, usipojizuia unaweza jikuta hata umeua mtu. Imagine nimehudumia kwa kipindi chote hicho, alaf sasahivi anakuja kuniambia kuwa mtoto sio wangu, tena ananijibu kwa nyodo kabisa😡😡
Fata ushauri uliopewa, kapime DNA kuepuka kuwa ATM/mgodi. Ukijua ni wako fata utaratibu wa kisheria wa kumchukua na hana uwezo kukataa. Kama sio wako samehe na anza upya. Hapo bado mambo ya secondary na chuo yanakusubiri.
 
Nimeacha baada ya yeye kunitamkia hayo maneno.. sasa nikipiga hesabu gharama zangu zote nilizotoa kipindi chote hicho kiukweli inaniuma sana
Ameshapata mwekezaji mpya atakayemtunza mtoto au baba yake mzazi amepata maokoto ya kutosha. Sikiliza na zingatia wimbo uliosema kwani kuachana sh ngapi. Na wewe sema kwani kuacha sh ngapi. Usihesabu pesa, angalia amani ya moyo wako. Huyo danga anajiletea laana kwa kizazi chake.
 
Hakuna fidia wazaz washez hua wana wabaka tu utasikia baba kabaka mwanae wa miaka 3
 
Mkuu - Kama ulikuwa unaweka ushahidi wakati unamtumia hizo pesa (e.g. Bank Slip etc), unaweza kabisa kudai fidia. Tafuta mwanasheria mpe hiyo kazi, tena udai na usumbufu na interest juu ya pesa yako, bila kusahau msongo wa mawazo na kuathirika kwa akili alikokusababishia kwa kukudanganya kuwa mtoto ni wako, wakati akijua sio wako..
 
Wanawake vichaa mnawakutaga wapi?
Huyo ni Asha ngedere Pro kabisa..

Wewe cha kufanya mpe huyo mtoto kisha mpotezee… pambana na maisha.!!
 
Back
Top Bottom