Je, kuna fidia yoyote ya kulea mtoto wa kusingiziwa?

Mtoa mada zingatia hili.
 
Sina risiti, lakini miamala niliyokuwa nikimtumia kwenye namba yake nina uhakika nikienda kwenye ofisi za mtandao ninaotumia nitapata statement ya miamala yote niliyokuwa nikiituma kwenda kwenye namba yake. Uzuri namba yake hajawahi kubadilisha, na mimi pia sijawahi kubadilisha
 
Utadai vingapi hapa duniani ndugu?Futa mawazo hayo.Jidai tajiri.
 
Uchumi wake unahakika unaweza kukulipa hizo gharama kwa muda gani...??
 
Kiislam mtoto wa nje ya ndoa ni ntoto wa uzinzi ankuwa ni wa mama tu.

Uislam mwema sana. Simple.
 
Hiyo sheria ya Daktari kuruhusiwa kudanganya majibu ikoje. Toa ufafanunuzi kidogo
 
Hiyo sheria ya Daktari kuruhusiwa kudanganya majibu ikoje. Toa ufafanunuzi kidogo
haipo mkuu!, nani akuwekee wazi ili msiamini..?
serikali haitaki watoto wa mitaani huko mitaani inajiepushia mizigo,majambazi na vibaka wanajua wakikupea wewe utamlea kama mwanao na kwa asilimia nyingi malezi yake yatakuwa kwa usahihi kuliko kumuachaniza!.. hii inaitwa akili kichwani si kila kitu uwekewe uchi..😂
 
Dah umeshusha SoMo Pana sana, huo ndo uhalisia wa mwanaume ktk familia na jamii. Ukitegemea furaha kutoka Kwa familia au jamii utapata shida sana, vita ya mwanamke na mwanaume ktk mahusiano mara nyingi mwanamke hupatiwa udhindi hata kama yeye ndo mwenye makosa, maaumizi sahihi ya mwanaume ni mhimu sana vinginevyo unawezajikuta ama unapoteza uhai wako au wa mtu mwingine na ikagharimu maisha Yako yote. Ushauri mzuri kwa mleta mada aachane na hiyo vita na mwanamke huyo na mtoto wake aendelee na maisha yake.
 
Mkuu hii kitu inatia hasira sana, usipojizuia unaweza jikuta hata umeua mtu. Imagine nimehudumia kwa kipindi chote hicho, alaf sasahivi anakuja kuniambia kuwa mtoto sio wangu, tena ananijibu kwa nyodo kabisa😡😡
Panga jipya pamoja na kulinoa, haizidi 15,000/-
 
Ukienda mahakamani watakuuliza je una risiti zinazoonyesha gharama za matunzo ya mtoto?kama huna basi utakosa ushahidi na uthibitisho na kesi itatupiliwa mbali na kuonekana haina mashiko.
Cha msingi potezea tu huyo mtoto yeye hajui lolote na ugomvi wenu yeye haumuhusu
 
Hiyo bado siyo uhakika, anawez kusema hivyo ikawa ni wako. Labda hakutaki tena katika maisha yake. Komaa kapime DNA uwe na amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…