Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Kuna watu wametengwa kwenye jamii, na ndugu jamaa na marafiki kwa sababu hizo hizo za madai ya uchawi , Binafsi kabisa yalikwishawahi nikuta nikaitwa mshirikina , nimetoa msukule baada ya katoto kangu kadogo kufariki na pneumonia, na maujinga ujinga mengi ya kipumbavu tu.
 
Kumbe ndio maana
 
Duh pole sana mkuu jamii yetu inawatu wajinga mno. Jamii zilizofunguka haziwezi waza mambo ya kipuuzi.
 
Uchawi upo.

Hauoni athari zake kwakuwa hakuna kinachowavutia kwako.

Au
Walishachukua vinavyowahusu kwako bila bughudha hivyo wanajilia au kuvitumia kwa raha zao.
Pia unatumia mbinu na njia tofauti na inavyopaswa ili uwajue, hivyo unajikuta unaishia kusema hawapo kitu ambacho wao wanapenda watu wengi wahisi hivyo kwamba hawapo, ili shughuli zao zisiwe zinakwamishwa.
 
Zamani watu walikua wana amini magonjwa yanatokana na hewa chafu wanayoivuta( Miasma theory) na waliamin kwa mamia ya miaka.


Germ theory ikaja batilisha na kutoa sababu za magonjwa mbalimbali.
na baadhi ya magonjwa yalikuwa yanasambazwa kwa hewa, hawakujua chanzo chake au njia ipi hasa ya hewa ila waliona watu wakizidi kuambukizwa kwa kuvuta hewa, hivyo sio kila kinachosemwa kiwe na uongo moja kwa moja huenda uchawi upo ila njia ya kuwasilisha ili ueleweke ndio kuna changamoto
 
Inaweza kuwa ni story tu, ila pale jamii zaidi ya moja ambazo hazina historia ya kukutana aidha kwa biashara au sababu yoyote zinapo ongelea hicho kitu unaanza kuwaza huenda kukawa na ukweli maana kwa nini wawe na wazo moja
Dini ipo je? Imani za kishirikina zipo je na zinasambaa aje?

Watu wanajifunza kutokana na interaction that's why.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…