Je, kuna mwanaume asiyechepuka?

Je, kuna mwanaume asiyechepuka?

Musa Meizon

Member
Joined
Aug 3, 2021
Posts
13
Reaction score
53
Habari yako ndugu msomaji.

Hili ni swali la kizazi cha leo, watu wengi wamelijibu kutokana na hisia zao na sababu mbali mbali zisizo na ukweli. Leo tulijibu katika uhalisia wake.

Kabla hujajibu lazima ujue hili, nini kinapelekea wanaume kuwasaliti wapenzi wao? Tuanze na mzizi.

Ukweli ni kwamba, japokuwa wapo wanaume waliojengewa au kujijengea tabia hii, kinachomfanya mwanaume achepuka ni kukosa CONTROL dhidi ya asili yake ambayo ni HUNTERS/WAWINDAJI. Hii ni asili yetu kama wanaume, kuwawinda wanawake kwa kila namna ili kuwapata kimapenzi.

Baada ya kuelewa chanzo, sasa utanielewa nikisema SWALI halitakiwi kuwa NI KWELI HAKUNA MWANAUME ASIE CHEPUKA? bali linatakiwa liwe JE, INAWEZEKANA MWANAUME ASICHEPUKE?. Ukweli ni kwamba WAPO WANAUME WASIO CHEPUKA na INAWEZEKANA KABISA.

Yafuatayo ni mambo matatu yanayoweza mfanya mwanaume aitawale asili yake na hatimae kutochepuka kabisa:

KUWA NA MALENGO:

Hapa simaanishi zile ndoto zisizo na kichwa wala mkia, mfano unasema malengo yako ni kuwa na pesa nyingi! Sasa Ukiwa na hela ndio utafahamika kama nani? Ninaposema malengo namaanisha lile kusudi la wewe kuwepo duniani. Usiniambie ulizaliwa ili tu uwe na pesa.

Hakuna kiumbe hatari zaidi duniani kama mwanaume asie na malengo. Huyu ni sawa na risasi iliyokosa muelekeo.

Ukiwa na malengo, utakuwa na muelekeo katika maisha na hutakuwa na muda wa kupoteza kuwinda winda wanawake.

2. MARAFIKI:

Huji kukuta swala anatembea msafara mmoja na Simba, labda ajichanganye na nyumbu. Wazungu wanasema,

"Show me your friends and I will tell you who you are."

Ukiwa na mke au mpenzi basi kaa na rafiki wenye wake/wapenzi pia. Ukikaa na nyumbu au wanaokula majani wakati wewe unakula nyama mwisho wa siku utajikuta unakuwa kama wao. Mwanaume mwenye malengo hakai vijiweni kupiga soga hata sikumoja. Vijiwe wanakaaga swala na nyumbu sio masimba dume embu jiheshimu. Asilimia kubwa vijiwe vinamfanya mwanaume atamani kufanana au kuwazidi wenzake ambao wanatembea na wanawake wanne kwa wiki! Maranyingi hizi ndio story za vijiweni, story zinazohamasisha kuwatumia wanawake kimapenzi; ukikaa nao utaishia kuingia kwenye hii ligi tu!

3. TAFUTA ROLE MODEL/MENTOR:

Hili ndio kosa wanalolifanya wanaume wengi sana. Hakuna kitu muhimu kama kuwa na mtu unaejifunza toka kwake na anaeweza kukushauri. Wanaume wengi hawajui kuchagua mentors/role models hivyo unakuta mtu anauwezo wa kibiashara lakini role model wake ni CHRIS BROWN! wapi na wapi???

Tafuta role model anaeweza kufanya lile unalofanya wewe. Na awe kafanikiwa katika hilo. Sio lazima awe perfect lakini katika yale unayovutiwa kuyafanya awe ameyamudu.

Namna ya kumchagua role model:

Usiangalie umri wakeHakikisha haishi maisha ya kuigizaAwe na uwezo wa kukusaidia katika unalojifunza toka kwakeAwe na mafanikio katika unalojifunza toka kwakeAwe na sifa ya uongoziSio lazima awe ndugu au mtu wa karibu. Hata akiwa taifa tofauti ni sawa.
IMG_20210804_203225_812.jpg
 
Wapo wanaume wasiochepuka ila wengi ni wenye umri kuanzia miaka 40 na kupanda hao ndo wanatosha kwenye hii mada yako, ambapo ni kwamba chini ya umri huo anakuwa amefanya uwindaji wa aina zote halali na haramu akiamua kutulia na mwanamke mmoja wengi wao hutulia kabisa, ila ndo sio wote wengine huendeleza kujitutumua mpaka uzeeni na wengi wao huzeeka kwa aibu sana.

Hakuna tuzo kwenye kubadili wanawake, watajisifia ndo uanaume lakini waliofanya hizi mambo ukiongea nao katika umri wao wa uzee wanajutia sana muda waliopoteza.
 
Mimi nimeacha kuchepuka lakini kitu nimeshindwa kuacha ni nyeto aisee.

Nitakaza weeee labda miezi miwili ila sasa nikiwa naoga najikuta tu najisemea ngoja leo nipige kwa mara mwisho lakini waaapi.

Ila nyeto tamu jamani tuacheni masikhara.
 
Kutochepuka ni mpaka uamue aisee na ujifunge mkanda kweli kweli kwakua opportunities zinatokea sana inalulazimu tu kusuuza rungu kama nature inavyotaka

Mimi binafsi bado sijafikia kuamua kujitesa. Ila kama wacheza mpira wanavyosemaga wanatundika daluga/kustaafu na mimi siku moja ntatundika penis. Kwa sasa Mungu nisamehe😂😂
 
Ukiona mwanaume anakwambia hawez chepuka ata itokee nn kwa kigezo kua anajiheshimu hyo ni ana matatizo ambayo ataki yajulikane popote zaidi ya yeye na mke wake.

Kiukweli sisemi kama kujizuia hatuwezi ila uwezi niambia upo kwenye ndoa miaka 5 na hujawai kuruka ukuta labda uwe umeolewa au umetengenezwa.
 
Back
Top Bottom