DOKEZO Je, kuna nini kinaendelea JNIA Terminal 3? Ndege hazitui wala kuondoka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Abiria wote wa KLM iliyotakiwa kuwasili jana usiku Dar es Salaam kutokea Amsterdam kupitia Kilimanjaro wamekwama KIA, na wako Mount Meru Hotel.

Mpaka sasa (saa sita na robo mchana leo) hakuna taarifa ni saa ngapi wataendelea na safari yao ya Dar es Salaam.

Abiria waliambiwa runway ya Dar ina mashimo makubwa na hivyo ndege kubwa zote haziwezi kutua. Only ndege ndogo ndogo zinaweza kutua kwa sababu haziitaji runway ndefu.

Hatma ya abiria waliokwamba KIA itajulikana leo saa kumi jioni kama watasafiri leo ama vipi.
 

Utaambiwa ni chama pinzani
 
Kutokana na hii hali labda ipo haja ya kufikiria kujenga 2nd runway
Inaweza kuwa;
1. Tuongeze iliyopo ifike labda 3.5kms ili iweze kutumika hata nusu
2. tuongeze nyingine across kama eneo linatosha
3. Kama upepo haubadiliki badiliki, tuongeze nyingine parallel

Kwa mitandao inaonekana Chato ina runway ya 3kms ina maana ni ndefu kuliko Dar?
Sioni kwa nini tusiboreshe hata zikawa mbili
 
Mambo mengi yameharibika hakuna uwajibikaji wala taarifa rasmi. Mtamkumbuka yule baba
 
Hahaha.........hapa msimuhusishe Shujaa tafadhali
 
Maji na umeme kwanza.
Mishahara hatimae umetoka. Ngoja tupambane na umeme kwanza. Maji wananchi wamekinga ya mvua.
Hivi punde taanza vikao vya kusikiliza kero nyingine
 
Nasikia pia kadi za maegesho ya magari zimeisha watu wamezuiwa kuingia! Uzembe umerudi kwa kasi kubwa kuliko kawaida!

Mama Samia awe mkali kidogo otherwise tutarudi kwenye damage beyond repair! Hii ngozi nyeusi bila kufukuzana na ukali wanakutia kidole machoni taifa linaingia hasara.
 
Makampuni ya ndege yanaingia gharama zisizo na ulazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…