DOKEZO Je, kuna nini kinaendelea JNIA Terminal 3? Ndege hazitui wala kuondoka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) inautangazia Umma kuwa kufuatia maelekezo ya Serikali kuhamia Dodoma, imehamishia baadhi ya shughuli zake za Makao Makuu jijini Dodoma kuanzia tarehe 30 Septemba 2022.

Ofisi za Mamlaka zitakuwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.

Wasiliana nasi kupitia anuani ifuatayo;
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,
S. L. P 250, Dodoma,
Simu: +255262354418
Barua Pepe: tcaa@tcaa.go.tz
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCCA)
Source : TCAA : Tanzania Civil Aviation Authority

Habari za ziada:

MANDHARI YA UWANJA WA DODOMA

Uwanja wa ndege jijini Dodoma wapokea dege kubwa la jeshi la Marekani aina ya C-17. Ripoti ya tarehe 31 August 2022 Boeing C-17 Globemaster

 
Apo aliedesign na kujenga runway lazima wataftwe kwa ajili ya kueleza shida Ni nini
 
Duh; hiyo ni airport au shamba? Mbona vumbi limefunika kila kitu hadi majengo during take off? Wali risk sana kushusha huo mdege hapo Dodoma.
 
mama anaupiga mwingi
 
Wale tu bata wanagalamiwa kila kitu hao watasafiri j4 asubuhi.

Suala ni kupotezewa muda, una tiketi ya ndege kutokea JNIA na unawahi kikao cha kikazi, shule, una likizo ya wiki n.k hadi hapo ushapotezewa ratiba yote...
 
Huu uwanja una eneo kubwa la kujenga Runway nyingine upande wa mashariki-upande wa reli ya TAZARA. Eneo hilo linatosha hata kuweka terminal nyingine tatu. Sijui kwa nini hili halikufanyika wakati wa maboresho ya Runway hiyo hiyo moja? 🤔
 

Mainzi yako yanazurura
 
Huu uwanja una eneo kubwa la kujenga Runway nyingine upande wa mashariki-upande wa reli ya TAZARA. Eneo hilo linatosha hata kuweka terminal nyingine tatu. Sijui kwa nini hili halikufanyika wakati wa maboresho ya Runway hiyo hiyo moja? 🤔
CC TAA
 
Nan anawalipia hotel au wanajilipia
 

26 November 2022​

| UONGOZI WATOA UFAFANUZI SABABU YA FOLENI UWANJA WA NDEGE JNIA DAR ES SALAAM

26 November 2022
Na Lovin Kefa,
Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere JNIA, Mhandisi Rehema Myeya amesema tatizo la msongamano ambalo lilitokea Novemba 22, 2022 katika geti la kupitia magari lilisababishwa na kuisha kwa kadi katika geti husika ambazo hutumika kuruhusu geti kufunguka.

Mhandisi Myeya ametoa ufafanuzi huo jijini DSM na kueleza kuwa tatizo hilo lilidumu kwa dakika thelathini na kupatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo ameomba radhi kwa niaba ya uongozi kwa usumbufu uliojitokeza siku hiyo na kuahidi kuwachukulia hatua wote waliohusika na uzembe huo.
 
Ehh ehhh hizo fidia nani analipa!

Mana mtu km una connection yako mbelez inakua ishakula kwako

Walipeleka watu kulala hotelini ama?
 
Sio basi lile ndugu hio gharama ya kukodi ndege nipesa mingi sana hafu kibongo bongo utakodi ndege gani mana kama I Ababa abiriq wengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…