Je Kuna Sheria kuhusu jinsi ya kupaki gari kwenye parking lot ya Bank?

Je Kuna Sheria kuhusu jinsi ya kupaki gari kwenye parking lot ya Bank?

Grand Canyon

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2020
Posts
545
Reaction score
1,191
Nimefika bank nikageuza gari na kupaki. Nikashuka na kwenda ATM Mlinzi akaniambia ni kosa kugeuza gari kabla ya kuingia Bank. Kwamba gari ikae mwelekeo wa bank, baada ya kupata huduma ndipo nigeuze gari. Sikuwa na muda wa kuhoji nilikuwa na haraka.
Naomba ufafanuzi mwenye kujua.
 
Yuko sahihi huyo mlinzi

Mia kwa mia
Muende shule za udereva achananeni na leseni za kuletewa majumbani na bar
 
Sheria ya zamani iliyopitwa na wakati
Mjinga wewe jambazi akivamia counter akapora pesa counter na wateja kumpata inakuwa ngumu kama kageuza gari kukimbia

Sheria imewekwa kuchelewesha na raisi ku block gari hiyo ya majambazi tena ashukuru kakuta mlinzi mpole ingekuwa Kenya angetwangwa risasi

Vituo kama vya mafuta gesi nk ndio unatakiwa gari ugeuze mwendo wa kutoka
 
Yuko sahihi huyo mlinzi

Mia kwa mia
Muende shule za udereva achananeni na leseni za kuletewa majumbani na bar

Mimi ni mhitimu wa Shule ya udereva. Ila hili sikufundishwa. Mara nyingi napata huduma ATM ya vituo vya mafuta, Huwa Kuna exit mbili na hakuna shida
 
Mjinga wewe ambazi akivamia counter akapora pesa counter na wateja kumpata inakuwa ngumu kama kageuza gari kukimbia

Sheria imewekwa kuchelewesha ns raisi ku block gari hiyo ya majambazi tena ashukuru kakuta mlinzi mpole ingekuwa Kenya angetwangwa risasi

Vituo kama vya mafuta gesi nk ndio unatakiwa gari ugeuze mwendo wa kutoka
Vipi ATM za kwenye vituo vya mafuta zenye njia mbili za kutokea?
 
Tuelekeze hizo shule za udereva zinazofundisha namna ya kupaki kwenye ma bank tafadhali.
Zinafundisha vizuri tu sio hayo ya benki tu wanafundisha pia ikiwemo polisi ,mahakamani ,hospitali nk kipi ufanye na kipi usifanye
 
Tuelekeze hizo shule za udereva zinazofundisha namna ya kupaki kwenye ma bank tafadhali.
Nenda chuo chochote cha VETA cha serikali hata refresher course hata uwe na leseni hawana shida watakupa refresher course kwa gharama ndogo
 
Tukiwa wadogo tulidanganyana kuwa range rover haziruhusiwi kupaki bank kisa zinakimbia sana,tukiwa wakubwa tukadanganywa eti pikipiki boxer marufuku bank,ujinga mtupu
 
Tukiwa wadogo tulidanganyana kuwa range rover haziruhusiwi kupaki bank kisa zinakimbia sana,tukiwa wakubwa tukadanganywa eti pikipiki boxer marufuku bank,ujinga mtupu
Sahivi tunaambiwa kuna direction ya kupark.
 
Nenda chuo chochote cha VETA cha serikali hata refresher course hata uwe na leseni hawana shida watakupa refresher course kwa gharama ndogo
Huko VETA ndipo tulipotokea mkuu hakuna hiyo elimu unayo isemea
Tena mbaya zaidi kwa sasa idadi ya wanafunzi imekua kubwa ndio wanafanya bora liende na kuna asilimia kubwa kama unasomea basic ukatoka mweupe kama ulivyo enda.
 
Back
Top Bottom