Je, Kuna shida surname ya mtoto na baba zikitofautiana?

Unajua, hili swala la kutumia majina naonaga pia yamekaa kama spiritual sana
Usihadaike na hayo mauongo ya waongo. Jina ni utambulisho wa mtu. Jina halina spirit.
Wazungu waliwadanganya mababu eti Majina yao yatawaletea mabalaa na bahati mbaya.
Leo hii watu Wana majina ya kizungu na bado wana mabalaa na bahati mbaya!
Sisi wa leo, tunapaswa kuwa ana akili na kuthamini urithi wa tamaduni zetu badala ya kuendeleza ulaghai wa wazungu, hasa kupitia dini.
 
Ok kwa mfano, Mimi ukoo wangu ni maarufu huko itinga. Niliskiaga kitambo ukoo wa wetu ulkuwa na ugomvi na ukoo gan sijui wakaanza kuuana kwa majina, lakin baadae inasemekana wazee wakakaa kumaliza tofauti zao, chain ya vifo kwa majina ya ukoo ikastop. Lakin pia nikaja kuskia Tena ikatokea Tena scenario kama hiyo kwenye jina hili Tena ila uzao wa kuanzia kwa Babu yangu.
 
Na hii ndio kasumba inayowafanya wengi waachane na matumizi ya majina ya koo zao, kuna ule uhasama wa koo na koo tangu zamani, upo na unaendelea kizazi hadi kizazi vita ni kubwa usipokuwa smart n ngumu sana kulitambua hilo.

Watu wanapatana na kusuluhisha ila hiyo haitoshi kumaliza vita na tofauti bado kuna wanaobaki na vinyongo na wanavirithisha kwa vizazi vyao na inakuwa endelevu.

Kuna kisa kimoja nilihadithiwa nikapewa sababu kwanini ndugu zangu fulani hawakupewa jina la ukoo wao, baadhi waliopewa vita yao ilikuwa kubwa sana. Kwa kifupi ambao hawakupewa iliwasaidia sana kuanzia shule, ajira na hata kwenye jamii.
 
Unajua, hili swala la kutumia majina naonaga pia yamekaa kama spiritual sana
Mkuu nakuonea huruma kwa sababu hujui ulitendalo. Katika sehemu zote ambazo zinahitaji kujaza majina huwaga kuna jina la kwanza, jina la pili na jina la ukoo, hiyo hata kitumishi kama kijana wako anahitajika kushika nyadhifa serikalini basi vetting yake inaanzia kwenye ukoo wake ili kujua chimbuko lake halisi. Sasa wewe unasema limekaa spiritual wakati huo ukoo ndo umekuweka hadi hapo ulipo kiumri.
 
Usihadaike na hayo mauongo ya waongo. Jina ni utambulisho wa mtu. Jina halina spirit.
Wazungu waliwadanganya mababu eti Majina yao yatawaletea mabalaa na bahati mbaya.
Leo hii watu Wana majina ya kizungu na bado wana mabalaa na bahati mbaya!
Sisi wa leo, tunapaswa kuwa ana akili na kuthamini urithi wa tamaduni zetu badala ya kuendeleza ulaghai wa wazungu, hasa kupitia dini.
Bila kwenda europe au arabia. Wazazi wengi huwezi waambia kitu 😁
 
Hakuna Shida
Hiyo ipo kwetu.....
Baba anaitwa Klop Joseph Mbilinyi
Mimi naitwa Liverpool Klop Mbilinyi
Mdogo angu/Dada anaitwa Chelsea Klop Joseph

Na HAIJAWAHI KUWA SHIDA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kwanini mbilinyi lakini, lazima utuweke wakinga,,,,, enewei msamehe mzee wako alchokosea ad kutaka kujitenga nae(ukoo).
 
Nini inakufanya ugeuzegeuze jina namna hiyo
 
Hakuna Shida
Hiyo ipo kwetu.....
Baba anaitwa Klop Joseph Mbilinyi
Mimi naitwa Liverpool Klop Mbilinyi
Mdogo angu/Dada anaitwa Chelsea Klop Joseph

Na HAIJAWAHI KUWA SHIDA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Mkuu mbona Mimi immigration walinibania passport kisa jina la babu wa kwenye birt certificate halifanani na langu la nida walikaza kbs ikabidi nikarekebishe upya Rita
 
Habari wakuu, naomba kujua kama inaweza leta shida kwenye mambo ya utambulisho ikiwa baba akaamua kulitoa jina la ukoo kwa majina ya mwanae. Mfano Mimi naitwa Joseph John Mbilinyi, ila mtoto wangu nikaamua nimwite Tony Joseph John kama full name yake.
Haina shida mkuu, mimi mwenyewe nilivyo fika darasa la nne nilibadili jina. Jina la mdingi lilikuwa limekaa ki-mizi mizi nikaamua kuachana nalo.
 
Habari wakuu, naomba kujua kama inaweza leta shida kwenye mambo ya utambulisho ikiwa baba akaamua kulitoa jina la ukoo kwa majina ya mwanae. Mfano Mimi naitwa Joseph John Mbilinyi, ila mtoto wangu nikaamua nimwite Tony Joseph John kama full name yake.
Haya majina matatu ya utambulisho wa mtu ni mfumo wa kisasa.

Kumbuka kuna mila mtoto akizaliwa hupewa jina la bibi au babu wa ukoo kwa mume na atakayefuata kuzaliwa hupewa jina la bibi au babu kwa mke.

Kwa utaratibu huu wa sasa unamnyima haki mtoto kuitwa jina lake la uji( jina la bibi au babu).

Mfumo uliopo sasa jina la kwanza ndiyo jina la mhusika, liwe la ubatizo au la kimila, jina ka pili ni la baba yake, jina la tatu ni la babu yake(la ukoo).

Ukitaka kulitoa jina la ukoo, unaanza kumuita:
Jina la kwanza ni la ubatizo/kiislam.
Jina la pili ni lile la kimila.
Jina la tatu ni la baba yake.
Ukiyaarange namna hiyo, jina la ukoo linapotea hapo.
 
Mkuu mbona Mimi immigration walinibania passport kisa jina la babu wa kwenye birt certificate halifanani na langu la nida walikaza kbs ikabidi nikarekebishe upya Rita
Kwangu haijawahi kutokea shida kokote.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Back
Top Bottom