Je, kuna siku Zanzibar itajitenga kisa …?

Je, kuna siku Zanzibar itajitenga kisa …?

Wewe sibure una tatizo kichwani ikija issue ya ZANZIBAR daima unakuwa unajifyatu IPO siku utakufa kihoro wewe
Hili haliepukiki rejea Tume mbali mbali zilizoindwa kuhusu sulihisho la Muungano na zote zilikuja na Wazo la Serikali tatu
Hata hawo wenzako G55 walikuja kihivyo hivyo

Mayala Zanzibar itabaki kuwa Mali ya wazanzibar tukiwa hai au tukiwa tumekufa kuna siku Zanzibar itarudi Kwa wazanzibar
Kuna mambo huyajui ndio maana unaota ndoto kama hiyo.
 
Kuna mambo huyajui ndio maana unaota ndoto kama hiyo.
Wewe ndio utakuwa huyajui rejea tumezilizoundwa za kutafuta kero za Muungano zilikuja na sulihisho gani? Za kina Nyalali na wengineo kama huko mbali rejea ya Mapendekezo ya KATIBA YA WARIOBA

Tatizo mna force hili NI tatizo lakutumia akili na si nguvu

kuna siku utanielewa
 
Kama wanajua kuna asiyetakiwa kushinda Uchaguzi, kwanini wanapotezea watu muda na kuingiza nchi kwenye gharama kubwa za uchaguzi?!!!
Uchaguzi ni takwa la kikatiba, hivyo lazima ufanyike, ila matokeo ya uchaguzi sio kwa mujibu wa takwa la kikatiba bali hali halisi iliyopo, ukiona mtu anazungumzia sana muungano wa mkataba, na wewe unajijua muungano wenu ni for life, mtu huyo akishinda uchaguzi utampa?.
Ukisikia muungano tutaulinda kwa gharama yoyote, matokeo ya uchaguzi yatakayo ulinda muungano ni moja ya gharama hizo.
P
 
Wewe sibure una tatizo kichwani ikija issue ya ZANZIBAR
Ni kweli nina tatizo
daima unakuwa unajifyatu IPO siku utakufa kihoro wewe
Naisubiria hiyo siku
Hili haliepukiki rejea Tume mbali mbali zilizoindwa kuhusu sulihisho la Muungano na zote zilikuja na Wazo la Serikali tatu
Hata hawo wenzako G55 walikuja kihivyo hivyo
Kwenye uhuru wa maoni, kila mtu yuko huru, wa serikali moja, mbili na tatu wote wawe huru.
Mayala Zanzibar itabaki kuwa Mali ya wazanzibar tukiwa hai au tukiwa tumekufa kuna siku Zanzibar itarudi Kwa wazanzibar
Zanzibar ni mali halali ya Watanzania wote
Wazanzibar wakiwemo.
P
 
Yugoslavia na Ethiopia zilivunjika, sembuse Tanzania. Pamoja na kuwa na mitandao hatari ya kijasusi, na majeshi imara ya kutisha, Yugoslavia na Ethiopia ziliangukia pua.......

Watanzania huwa wanaamini kwamba huu muungano utalindwa kwa nguvu za kidola lakini siyo makubaliano ya kitaifa (National Consensus). Hili lina hatari sana.....

Ikumbukwe huko nyuma hata wakati Mzee Nyerere yupo, yalishafanyika majaribio makubwa ya kuuvunja muungano, ambayo yalizimwa kwa mauaji, vitisho na nguvu za kijeshi.

Maraisi watatu wa Zanzibar walishakuwa wahanga hadi kupeleka wengine kupoteza maisha na wengine kukweka kizuizini. Haya yote hayakuzuia hizi harakati kuendelea nchini Tanganyika hata wakati bado Nyerere yupo hai.

Ushawishi binafsi wa Nyerere na nguvu ya dola ndiyo ilitumika kuyazima haya makundi ndani ya nchi. Mbali na hivi vitisho vyote, mwaka 2001 ulitokea umwagaji damu mkubwa mno Zanzibar.

Ukiangalia kwa umakini, utafahamu kwamba tukio moja huzaa jingine (A Chain of Dominoes) Kuna siku huko mbele linaweza kutokea jingine, ambalo hata kulizuia haitawezekana.

Jamhuri ya Ireland ilianza hivihivi, dhidi ya Uingereza. Kila wakijaribu, Uingereza inatumia mitandao yake ya kijasusi na kijeshi kupoteza watu. Ila siku ambayo hawategemei waairishi kama Michael Collins walifanya ukatili uliokithiri hadi kupelekea Uingereza kuiachia Ireland.

Hakuna jambo zuri kama uwazi na maridhiano ya kitaifa. Watanganyika wasikilizwe na Wazanzibar wasikilizwe, hili la kikundi cha wanasiasa wachache kutoka chama tawala wakiongozwa na viongozi wa dini fulani, kutaka kutuamulia watanzania wote halikubaliki na litakuja kuleta matatizo huko mbele.
 
Hakuna fyoko fyoko,

Hiyo siku haipo

Mkuu britanicca , hakuna siku Zanzibar itajitenga kwasababu Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Type ya muungano wetu ni very unique, kwa upande mmoja ni fused union, kwa nchi mbili kufa na kuzaliwa nchi moja. Nchi mbili hizo haziwezi kukufuliwa, they are dead and gone, hivyo kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, kuivunja ni uhaini!, ni muungano for life na hakuna room ya kuuvunja!.

Kwa upande wa pili ndani ya muungano, muungano wetu ni federation ya nchi mbili, serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili. Nchi hizi mbili, moja ni dola na nyingine sio dola, nchi ambayo sio dola haiwezi kujitenga kwasababu inaitegemea dola!, hivyo muungano wetu upo sana na tutaulinda kwa gharama yoyote, na ndio maana kwenye kila uchaguzi wa upande ule kuna mtu huwa anashinda lakini hapewi kwa kuhofia hatma ya muungano!. Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano? hivyo lazima fulani ashinde!.

P
But Zanzibar still exist mkuu
 
Nami inabidi niulize swali kama hilo hilo, ila kwa upande wa Tanganyika: Je, kuna siku Tanganyika itajitenga?
Kwa nini swali lisiwe hilo.
Zanzibar wanajielewa kuliko bara,wakati wa uchaguzi utaona vyombo vya usalama vinavyoenda zenji 😀😀
Huku wajukuu wa Nyerere ili mradi kuna Simba na Yanga, Diamond na Ali Kiba utatawala milele
 
Hakuna fyoko fyoko,

Hiyo siku haipo

Mkuu britanicca , hakuna siku Zanzibar itajitenga kwasababu Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Type ya muungano wetu ni very unique, kwa upande mmoja ni fused union, kwa nchi mbili kufa na kuzaliwa nchi moja. Nchi mbili hizo haziwezi kukufuliwa, they are dead and gone, hivyo kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, kuivunja ni uhaini!, ni muungano for life na hakuna room ya kuuvunja!.

Kwa upande wa pili ndani ya muungano, muungano wetu ni federation ya nchi mbili, serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili. Nchi hizi mbili, moja ni dola na nyingine sio dola, nchi ambayo sio dola haiwezi kujitenga kwasababu inaitegemea dola!, hivyo muungano wetu upo sana na tutaulinda kwa gharama yoyote, na ndio maana kwenye kila uchaguzi wa upande ule kuna mtu huwa anashinda lakini hapewi kwa kuhofia hatma ya muungano!. Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano? hivyo lazima fulani ashinde!.

P
Hatima ya muungano inatakiwa kulindwa n katiba na sio hofu ya nani atashinda
Ukiona muungano upo kwa sababu tu fulani atashinda jua huo muungano ni batili.
 
Dr Samia don't mess up , kwa gharama yoyote hakikisha uchagusi wa 2025 unashinda kwa maana haitakuja kutokea tena kwa Mzanzibar kuwa Rais wa JMT mitano inayofuata hakikisha unajenga visiwa unguja ina unaafu kwa sasa elekeza nguvu Pemba hata tukiachana nao tuwe tumejenga nguvu ya kiuchumi ya kuwatawala baadae. tumepigwa pini muda mlefu sana.
 
future impossible tense
 
Zaweza ibuka fyoko fyoko kadhaa je yaweza kusababishwa marais wanaotoka upande wa pili? Maana wanajambo lao kifuani japo hawasemi hadharani ila nadhani there is a day zenji wataamua kukaa pembeni baada ya kuvuna bara bya kutokasha kutokana na awamu ambayo yaweza kuwa ya Bara kuhoji mzenji alowatangulia alokwepesha yaende kwao

Britanicca
Tulishauri Toka enzi za tume ya katiba tuwena serikali 3 mkakataa
Sasa mnalialia Nini?

Wazenji wamejizatiti safari hii wataikamua viliyo Tanganyika then wavunje muungano
 
Zanzibar wanajielewa kuliko bara,wakati wa uchaguzi utaona vyombo vya usalama vinavyoenda zenji 😀😀
Huku wajukuu wa Nyerere ili mradi kuna Simba na Yanga, Diamond na Ali Kiba utatawala milele
Hujui kusoma alama za nyakati mkuu 'Girland'. CCM iko mlangoni, inaaga.
 
Huu Muungano ni mzuri ila pia una ufala mwingi sana kiasi kwamba kadri tunavyozidi kuuendekeza ndivyo unatuoanda kichwani

Kanuni ni moja tu masharti ya kipuuzi yote yaondolewe na watu wawe huru kuishi popote wanapotaka bila kupangiwa wala kuingiliwa

Haiwezekani mtu kutoka zenji amiliki ardhi bara bila kikwazo ila wewe wa bara kumiliki ardhi Zenji ni kipengele

Watu waruhusiwe mahala popote sababu hakuna mtu anelazimishwa kuuza ardhi yake, bali kwa matakwa yake sasa ikiwa mtanganyika anataka kununua ardhi zenji aruhusiwe sababu anayemuuzia karidhia vivyo hivyo bara

Huu utengano ni kwa sababu kama hizo na nyingine nyingii
 
Wengine ni Wasukuma Wajita. Tuna ndugu kule waliokwenda toka vita kuu ya pili.
Nasema waende zao! Inatosha kwa kweli!
Sina hata shida nawo kwa kweli!
 
Hujui kusoma alama za nyakati mkuu 'Girland'. CCM iko mlangoni, inaaga.
Wakiiba kura Kama wanavyofanya kila wakati utafanyaje au unaamini heche alizidiwa kura na CCM au Sugu pale Mbeya town?
 
Back
Top Bottom