Je, kuna ubaya gani Serikali ikaruhusu sukari iagizwe kwa uhuru kama nguo Kariakoo?

Je, kuna ubaya gani Serikali ikaruhusu sukari iagizwe kwa uhuru kama nguo Kariakoo?

Acha bhana.., kumbe hivi viwanda vinawekewa limit ya kiasi cha kuzalisha?!!!! Huu mbona kama ni Umafia tunafanyiwa na serikali yetu wenyewe dhidi ya walalahoi?!
Nchi za kijinga na zenye viwanda vichache vya sukari wanapata uzalishaji mkubwa kuliko hata Tanzania yenye viwanda vingi vya sukari hapo Uganda, Malawi, Zimbabwe, Zambia na Uganda wanazalisha sana sukari kutuzidi wakati wana viwanda vichache ila Sera zao kwenye sukari sio ukiritimba kama kwetu..
 
Umeandika facts kabisaa,,, tatizo la hii nchi walioko kwenye maamuz akili zilishaganda kwa utamu wa asali na wenye akili timamu hawaruhusiwi kabisaa kupewa mamlaka,,, hii kauli ya sukari ya nje hairuhusiwi kuagizwa kwa soko huru ina ukakasi sana probably inanufaisha sana wachache!
Yan tuna lundi la wapumbavu waliopindukia wako madarakani..thinking zao ni mavi kabisaaa
 
Yani inashangaza
Ukivukuka Hapa Kabanga kwenda Burundi sukari ni 1500
Ila hapa Ngara sukari ni 5200
Rais Samia atunusuru Wananchi
Mbona kama anatukomoa tulimkosea nini
Nauli kufika Dat 1200
Kama unaenda Johannesburg kweli?
Mafuta ya kula bei juu?
Mabando ya simu bei juu
Cement bei juu
Umeme hakuna
Tanzania yetu mbona kama tupo kama wehu aisee
Kuna wananchi wana hali tete vijijini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho ni kituko, hao Burundi wametuzidi nini hasa?
 
Ila hii hujuma ya sukari mbona wanachofanya si ubindamu kabisa?! Sukari ni bora iagizwe kwa mtumdo huru.., huu mfumo wa sasa upo kukandamiza wengi na kuneemesha wachache wizarani, hasa yuke mla rushwa ili kutoa vibali
Tani 500
IMG-20240216-WA0015.jpg
 
Hawa mbwa washenzy ni kwanini miaka nenda miaka rudi wanapewa ulinzi mzito wa kiwango cha SGR, wanahakikishiwa soko la UHAKIKA, wanapewa mashamba bagamoyo na kwingineko bure, vibali vya kuagiza sukari wanapewa wao ili faida waitumie kukuza viwamda, ila viwanda havikui na hawaongezi uzalishaji, NI KWANINI!!!!

Hawa sio kwamba hawawezi kuzalisha ya kutosha, uwezo wanao na DEMAND IPO! , ila wanashirikiana na wahindi wenzao walanguzi na kulimit uzalisha ili kuleta uhaba na hatimae kutoa rushwa na kupewa vibali ili waagize sukari na kuja kuiuza kwa bei mara 5! Mbaya zaidi faida wanaichange kuwa dollar na kuipeleka INDIA, Tunawalinda hawa mbwa kwa faida ya nani kama tunaumizwa hivi?!!!
 
Hii nchi inachezewa sana
Ifike muda tuelezwe faida ya kulinda wahujumu uchumi ni ipi?! Mtu unapewa ukinzi ila hutaki kuongeza uzalishaji kwa makusudi! Kama ni hivyo waondolewe huo ulinzi wakajifie zao huko kuliko kuemdelea kuuziwa sukari 6,000/=
 
Uagizaji na usambazajinwa sukari una siri kubwa sana. Ni sawa kabisa na uagizaji wa mafuta. Kuna network ya walaji hapo kati huwezi amini. Ndio maana huwezi kwenda kichwa kichwa kununua sikari kiwandani. Na hutakaa usikie tangazo la kuomba mfanyabiashara awe msambazaji wa sukari. Gharama ya kutengeneza sukari sio kubwa. Tatizo ni miko ya watu hapo kati.

Ukisema sukari iagizwe kama nguo. Inawezekana na usishangae kilo ikawa shs 1000 pamoja na kulipa kodi kubwa inayotozwa. Kwa bidhaa zinazoingizwa nchini sukari ndio inatozwa kodi kubwa kuliko zote. Huko nje kuna sukari ya kumwaga hasa kutoka Brazil.
Sukari ni mfupa mgumu sana, ulimshinda hata JPM.
 
Tunalinda hivi viwanda vya ndani kwa maumivu na mateso makali hivi kwa faida ya nani? Kama viwanda vinavyolindwa havikuwi wa kuongeza uzalishaji kwa makusudi, faida ya kuwalinda ni ipi kama tunauziwa sukari 6,000/= badlanya 1,000/=?!
 
Kuna nchi ya kufanya hivyo, ila si Tanzania...
Tatizo Serikali ikiruusu Sukari toka nje kelele zinaanza za kulinda viwanda vya ndani hivyo viwanda vikilindwa nao badala ya kujiongeza ndio tunakumbana na mambo kama haya kila mwaka mvua zikianza kuchanganya kunyesha tu Sukari inakuwa ni changamoto
 
Back
Top Bottom