Je, kuna ubaya gani Serikali ikaruhusu sukari iagizwe kwa uhuru kama nguo Kariakoo?

Hii ni kulinda Viwanda vya ndani na kivijengea uwezo

kiuchumi inaitwa Protectionisim Policy

Wazalishaji wa ndani wanalindwa kwa kutoruhusu au kuruhusu kidogo bidhaa inayo zalishwa na wazalishaji wa ndani kuingia nchini.

Kuna aina mbili

Kwa kutoza kodi juu bidhaa inayoingizwa hivyo kuifanya iwe na bei juu kuliko ile iliyozalishwa ndani

Kutoruhusu kabisa au kwa uchache bidhaa hiyo kutoka nje.
 
Nani kabisha?

Unarudia nilichosema, nimeuliza, kama wanalindwa na hawakui wala kuongeza uzalishaji, badala yake wanashirikiana na walanguzi kulimit uzalishaji iki wapewe vibali vya kuagiza sukari na kuja kuuza bei mara nne huku wananchi wakiumia, ni kwanini sukari isiagizwe kwa uhuru ili watu wapone na mateso haya?
 

Hasara zakuagiza sukari hovyo na kito vilinda viwanda vya ndani ni kubwa kuliko.

Fikiriria kuhusu

1.Kodi
2.Ajira
3.Huduma za kijamii
 
Huu ni mradi wa watu wazito (viongozi na wafanyabiashara) Kipindi wewe unalalamika bei ya sukari ndivyo watu wanavyopiga hela
 
Hasara zakuagiza sukari hovyo na kito vilinda viwanda vya ndani ni kubwa kuliko.

Fikiriria kuhusu

1.Kodi
2.Ajira
3.Huduma za kijamii
Wakiagiza sukari nje.
1. Kodi gani itakosekana?
2. Ajira zipi zitakosekana?
3. Huduma gani za kijamii zitakosekana?
Siku zote uzalishaji wa sukari hapa nchi upo chini sana na ndiyo maana kila siku sukari inapanda bei.
Kikwete sukari ilikuwa shilingi ngapi? Magufuli je? Juzi hapa sukari ilikuwa 2800 kilo ila sasa ni 4,000 mpk 5500.
Kwa viwanda hivi vya ovyo Tanzania sukari itakuwa ni 7000 kilo 1. Time will tell
Endelea kulinda ujinga wakati watanzania wanalia
 
Bora umenisaidia, Mimi sikuona hata haja ya kumjibu, sina muda wa kuchezea
 
 
 
Kwa jinsi hii nchi inavyotamaniwa tutalishwa sumu tupukutike
 
Sukari iagizwe kwa mtindo wa soko huria, umeme sasa ni wa kutosha na wa uhakika, wenye viwanda wajisimamie wenyewe sasa..
 
Mkuu hizo ndio moja ya dili kubwa za CCM, ili upewe kibali lazima uwe unakula nao, usikute mtu anatakiwa alipe B 2 kila kwaka ili aendelee kuwa na kibali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…