Hapa Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%
Umeongea uhalisia kuhusu aljebra
Kwenye ishu za dini nazo soma historia vizuri kama ulivyoelezea aljebra
Naunga mkono na kukupongeza kwenye ishu ya aljebra umesema ukweli kuhusu huyu mgunduzi Bwana Muhhamad Al kwarizim
HONGERA SANA
Kwenye uislam na ukristo Chanzo chake pia Usione Haya sema ukweli uhalisia
Quran ni kitabu kiliunganishwa na Abu Bakr na huyo ndie mtu aliyejua soma na kuandika wakati huo, Acha story kuwa kitabu kilishushwa
Biblia ni kitabu kiliunganishwa pia, Watu Waache story kufikiri biblia ni kitabu cha enzi wakati watu waliunganisha kufanya kitabu biblia
Kasome pia akili za bwana Abu Bakr, Hakika utapata mengi kuhusu uhalisia wa uislam kama ulivyoelezea ishu ya aljebra
Si hao tu. Kuna wengi sana, jiulize kwanini wanabadilishwa majina?
Hawajaishia huko tu, hata hapa kwetu Afrika wametoka mabingwa wa Kiislam, mbona hatuwasomi hapa kwetu? Kuna kina Ibn Batuta, walioiandika Kilwa na pwani ya Afrika Mashariki kabla ya 'akina" Vasco Da Gama.
Kuna bint wa Kiislaam aliyeanziaha chuo kikuu cha kwanza kabisa duniani, anaitwa Fatma Al Fikhri, unalijuwa hilo?
Unafahamu kuwa hii uijuayo sasa kama Tanganyika ilikuwa ni Zanzibar? Mbona hatuyasomi hayo?
Unajuwa kuwa Mbantu kihistoria ni mtu wa kuja tu pwani ya Afrika Mashariki? Mbona hatuyasomi hayo? Aliwakuta kina nani Mbantu alipokuja pwani ya Afrika Mashariki? Ushajiuliza hayo?
Ilikuwaje, utawala wa Kabka na huko Uganda na Kagera vazi la heshima na la asili kwao kuwa ni kanzu? Umeshayasoma hayo? Mbona hayasemwi?
Umeshajiuliza kwanini vazi la heshima kwa wahehe ni kanzu, yes, kanzu hizi za Waislam.
Umeshajiuliza kwanini kuna miji mikubwa chini ya bahari ya Kilwa, hatujulishwi historia yake na wana historia wa Chuo Kikuu cha Dar wapo huko wanafanya tafiti?
Umeshajiuliza kwanini mabaki ya Kilwa yamewekwa kwenye uriti wa dunia na yanalindwa na Umoja wa Mataifa yasiharibiwe? Je ni nani walioacha hayo mabaki na kuna historia ipi hapo?
Umeshajiuliza kama kuna mabaki hapo Kilwa, vipi kuhusu Pwani yote ya Tanzania?
Kuhus Qur'an kama ulivyochomekea mwisho hapa...
Hapana, kitabu hakijaungwa na yeyote zaidi ya aliyeshushiwa aya hizo, akisema aya hii husomwa hivi, kabla ya hii na hii husomea hivi baada ya hii na hii ni aya sura hii na hii ni aya ya sura fulani.
1) Umeisoma Qur'an?
2) Wewe ni wa kanisa lipi?
Qur'an imeshushwa kwa miaka 23 kidogo kidohgo kwa Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam. Utapoisoma na utapo uelewa mpamgilio wake kisayansi ndipo utakapoelewa kuwa si Abubakar (Alayhi Salaam), si Muhammad (Salla Allahu Alayhi Wasalaam) kuwa ndio walioandika au kupanga Qur'an ilivyo. Qur'an ni muujiza unaoishi, ilivyo ni "beyond any human comprehension". Isome usiogope, na ukitaka kufahamu zaidi ntakupa vipande vidogo dogo vya muujiza wake, usiopingika.
Kwa kuanzia, basi haufikirii hata kidogo, vipi hii Qur'an iwe ndicho kitabu pekee duniani kilichohifadhiwa na watu wengi zaidi na ndicho kitabu pekee kipo kwa lugha moja tu lakini kinahifadhiwa na watu wa lugha tofauti tofauti duniani? Huo pekee ni muujiza. Kipi kingine chenye hayo?