Je, kuna uhusiano gani kati ya kwenda hijja na harakati za uganga ama tiba za kisuna?

Je, kuna uhusiano gani kati ya kwenda hijja na harakati za uganga ama tiba za kisuna?

Mimi nina vitabu vya dini na vya uganga vimejaa begi.
Nilikuwa nanunua pale msikiti wa mtoro kariakoo kwa wahindi.
Hata wewe unaweza kuwa mganga ni ELIMU TU
 
Hulka za Binadamu waliovamiwa na Viumbe hao kutoka Katika Dini hizo ni kwamba Akienda Huko atarudi na Maajabu.

Siyo hao tu hata Wakristo wakienda Kuhiji huko Yerusalemu wanatamani Kujenga kanisa na Kuhubiri kutoa Mapepo

Dini hizi hazina msaada ki utu na Wala Kumtoa Mtu kwenye matatizo bali ni Upigaji wa Kikoloni Uliokuja. Kumbuka Bila Wakoloni usingekuwa unajua Leo Kuna Ukristo wala Uislamu.

Ni Vigumu kuwa Buddha maana Hawakukutawala wenye imani za Kibudha

Mtekwaji Ataongea ya Aliyemteka.
Nakubaliana na wewe. Endapo TANZANIA ingetawaliwa na Wachina leo hii kungekuwa na Wabugha wengi sana na wala tusingekuwa na uelewa wa uislamu na ukristo kama tulivyo sasa! Au tungetawaliwa na Wahindi, ni mwendo wa kuabudu ng'ombe na masanamu.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahii mkuu...wengi wanaoenda kuhijji hawana elimu ya kutosha kuhusu hiyo hijja....mfano yupo ndugu yangu alipata vihela vya kiinua mgongo akawa amekwenda hijja...cha ajabu toka amerudi amekuwa bingwa wa kugombanisha watu.......
Hijja haihitaji elimu kubwa. Usilinganishe Muislam na Uislam. Uislam ni mwepesi sana, walimwengu ndio wazito. Kama wewe hapo, unaoesha wazi ni mzito wa kuelewa. Unauhukumu Uislam kwa makosa ya "Muislam"? Fikiri.

Hijja yake huyo nduguyo haihusiani kabisa na hicho unachosema "kugombanisha waytu". Havana uhusiano wowowte. Hijja yake kaenda na katimiza nguzo ya Uislam na hayo mengine ni yako wewe, si yake, kwa kuwa umsema mtu asiyekuwepo, usengenyaji, (backbiting) hapa. Kiislam hilo ni kama kula nyama ya maiti ya nduguyo. Wacha kabisa. Soma mafundisho ya Uislam kuhusu hilo ulilofanya hapa:

49_12.gif

Qur'an 49:12. Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. 12
 
Mimi nina vitabu vya dini na vya uganga vimejaa begi.
Nilikuwa nanunua pale msikiti wa mtoro kariakoo kwa wahindi.
Hata wewe unaweza kuwa mganga ni ELIMU TU
Rekebisha maandiko yako, Msikiti wa mtoro hawauzi vitabu. Andika jirani na msikiti wa mtoro, Maduka yote yalio karibu na misikiti hayahusiani kabisa na misikiti. Ni biashara za watu binafsi na si za msikiti. Tukumbuke hilo.
 
Wewe umetekwa na nani? Au peke yako ndio hujatekwa, upo huru kushambulia waliotekwa?

Soma Qur'an, imekuja kwa ajili ya watu wote.
Ww ni mtekwa wa wakoloni wa kiarabu. Mimi si mtekwa Wa Watawala hao. Unaongea ya Qur'an maana Ndio waliokutekea akili

Qur'an ya watu wote wakati haijaandika hata haiwatambui wasukuma, wamakonde, wazaneko, wakurya n. K ila inawatambua Manabii wa Waisraeli huko. Malaika n. K Wewe mzanaki,mchaga, mpare, upo wapi kwenye Qur'an hiyo ya watu wote unayoinadi
 
Sheikh Hashim Rusaganya kalijibu vizuri sana kwa mafundisho ya Kiislam hilo la ukabila ulilolileta hapo. Pata faida ya kujuwa mafundisho ya Kiislam:

Ukabila, uzawa sumu ya udugu wa Kiislamu Na Hashim Rusaganya
UKABILA, utaifa, uzawa ni maneno yaliyozoeleka sana masikioni mwa watu. Imefikia hatua ambayo hauangaliwi ufanisi wa kazi inayohitajika au kufanyika bali yanatazamwa haya maeneo matatu kwanza kama yanakubalika kulingana na nafasi yenyewe.

KWA mtazamo wa Uislamu maneno haya matatu hayana nafasi kabisa badala yake uangaliwa ufanisi tu. Bila kujali huyo muhusika ni kutoka kabila lipi au taifa gani wala alipozaliwa.

Uislamu kama mfumo kamili wa maisha umemuweka mwanaadamu katika nafasi nzuri ambayo ni vigumu sana kwa yule atakayeufuata barabara kuingiza matabaka haya ambayo hatima yake ni uadui, chuki za kila namna na hatimaye mauaji ya kinyama.

Hebu na tuangalie Qur'an inatuambia nini juu ya matabaka haya: Kwanza, Mwenyezi Mungu ameanza kwa kututanabaisha kuwa wanaadamu wote asili yetu ni moja na tumetokana na nafsi moja.

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao..." (4:1)

Hapa Mwenyezi Mungu anatufahamisha kuwa baada ya Adam (as) kuumbwa kisha akaumbwa mkewe ambaye ni Hawwa (a.s.) ndipo tukaenea wanaume kwa wanawake wengi duniani kutoka katika wawili hao.

Pia katika Qur'an 49:13 Allah (s.w.) anatufahamisha:

"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanaume (mmoja, Adamu) na yule yule) mwanamke (mmoja Hawaa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane (tu basi, siyo mkejeliane). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule ambaye mcha Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote)". (49:13).

Kumbe Mwenyezi Mungu baada ya kutuumba kutokana na nafsi moja, bado alitugawa katika mataifa na makabila tofauti tofauti, lakini si kwa lingine bali ili tuweze kujuana.

Hebu na turejee katika Hadithi ya Mtume (s.a.w.) iliyosimuliwa na Abi Nadhrah, kwamba alimsimulia mtu aliyesikia khutuba ya Mtume (s.a.w.) aliyoitoa katikati ya siku za Tashriq akisema:

"Sikilizeni, hakika Mola wenu ni mmoja na hakika baba yenu ni mmoja. Hakuna ubora kwa Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu wala hakuna ubora wa mwekundu kwa mweusi wala mweusi ju ya mwekundu. Isipokuwa kwa kumcha Mwenyezi Mungu.

Kisha Mtume (s.a.w.) akauliza nimefikisha ujumbe huu? Maswahaba wakajibu amefikisha mjumbe wa Mwenyezi Mungu".

Pia imesimuliwa toka kwa Ibn Umar (r.a.) kuwa Mtume (s.a.w.) aliwahutubia watu siku ya Fathu Makka akasema:

"Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amekutakaseni kutokana na uchafu wa ukabila na kujifakharisha kwa mababa zao. Watu wako wa namna mbili, wa kwanza ni mtu mwema Mcha Mungu na wa pili ni muovu aliyedhalili kwa Mwenyezi Mungu. Na watu wote ni watoto wa Adamui na Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kutokana na udongo". (Tirmidh)

Pia Hadithi hii imo katika sahihi Sunnah Tirmidh ya Albaan Vol. 3 hadithi ya 2608.

Kwa hiyo utaona kuwa Uislamu ulikuja kuvunja ukabila na kuondoa utabaka.

Historia ya Uislamu inatuonesha kuwa Mtume wa Allah (s.w.) alimpa Usama uongozi wa jeshi kwenda mpakani mwa Sham kupambana na Warumi. Usama alikuwa mtu mweusi akapewa jeshi ambalo limejaa Waarabu mfano Abubakar ni miongoni mwa waliokuwa ndani ya jeshi hilo.

Ipo mifano mingi sana, mfano Sayidina Bilal ambaye alikuwa Muadhini wa Msikiti wa Mtume (s.a.w.) alikuwa mweusi.

Kwa hiyo kinachoangaliwa katika Uislamu ni uwezo wa kufanya kazi inayotakiwa. Kama ni Uimamu au Uamiri au uangalizi wa shughuli yoyote ile inayohusu Uislamu sharti mhusika awe na ujuzi wa yakini juu ya kazi hiyo, ukabila, utaifa na uzawa havitaangaliwa.

Kwa misingi hiyo ndiyo maana Allah (s.w.) akatuunganisha pamoja kwa kutuita ndugu. Soma Qur'an sura ya 49 aya ya 10. Siyo hiyo tu tunaambiwa tupatanishane pale itakapotokea hitilafu baina yetu kisha tumche Mwenyezi Mungu mwingi wa Hekima.

Ndiyo maana Mtume (s.a.w.) kwa kuzingatia hili akasema:

"Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuoneana kwao huruma na kusaidiana kwao ni mfano wa kiwiliwili. Kinapopatwa na maradhi sehemu moja basi mwili wote hukesha kwa maumivu na machovu". (Bukhari na Muslim)

Ninamalizia kwa kuwakumbusha Waislamu wote kwamba tutazame mifano michache ya hapa ulimwenguni juu ya wanaadamu ambao wamethubutu kuweka ukabila mbele zaidi ya utu. Matokeo yake ni nini? Sina haja ya kutoa mifano ni nchi gani au ni jimbo gani hapa duniani lenye mgogoro mkubwa wa kijamii unaotokana na ukabila na utabaka.

Lakini ikumbukwe kwamba maadui wa Uislamu waliutumia ukabila na wanaendelea kuutumia ili kuhakikisha Uislamu unaangamizwa kabisa. Angalia maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur'an 63:7-8.

Chanzo: An-nuur Na. 233
 
Umewahi kujiuliza kwa nini vitabu vya uganga viuzwe karibu na misikiti na sio karibu na makanisa?
Rekebisha maandiko yako, Msikiti wa mtoro hawauzi vitabu. Andika jirani na msikiti wa mtoro, Maduka yote yalio karibu na misikiti hayahusiani kabisa na misikiti. Ni biashara za watu binafsi na si za msikiti. Tukumbuke hilo.
 
Wee Bibi una matatizo.
Rekebisha maandiko yako, Msikiti wa mtoro hawauzi vitabu. Andika jirani na msikiti wa mtoro, Maduka yote yalio karibu na misikiti hayahusiani kabisa na misikiti. Ni biashara za watu binafsi na si za msikiti. Tukumbuke hilo.
 
Hijja haihitaji elimu kubwa. Usilinganishe Muislam na Uislam. Uislam ni mwepesi sana, walimwengu ndio wazito. Kama wewe hapo, unaoesha wazi ni mzito wa kuelewa. Unauhukumu Uislam kwa makosa ya "Muislam"? Fikiri.

Hijja yake huyo nduguyo haihusiani kabisa na hicho unachosema "kugombanisha waytu". Havana uhusiano wowowte. Hijja yake kaenda na katimiza nguzo ya Uislam na hayo mengine ni yako wewe, si yake, kwa kuwa umsema mtu asiyekuwepo, usengenyaji, (backbiting) hapa. Kiislam hilo ni kama kula nyama ya maiti ya nduguyo. Wacha kabisa. Soma mafundisho ya Uislam kuhusu hilo ulilofanya hapa:

49_12.gif

Qur'an 49:12. Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. 12
Huna hoja ya maana wewe...halafu acha kutetea mambo ya hovyo ya mtu kwa kutumia maneno matukufu usilete ushabiki wako hapa na bifu za kipumbavu....
 
ALHAJI MZEE YUSUFU aliyekuwa anaimba taarabu, baada ya kutoka HIJJA, aliachana na MUZIKI kabisa.
Kuna wakati nilisikia TANGAZO kwamba atakuwa HOTEL moja pale DODOMA sambamba na SHEKH SHARIF kwaajili ya kuwaombea dua watu wenye shida mbalimbali pamoja na kutibu Maradhi kwa dawa za kisuna.
KWASASA ALHAJI ANA BEND MPYA YA MUZIKI WA TAARABU.
Nini kinahamasisha baadhi ya watu wakitoka HIJJA kuwa WAGANGA.
AMA KUNA NGUVU ZA UGANGA HUWA ZINAWAPATA WATU KULE MAKKA?
Kwenda hijja siku hizi ni fashion tu

Ova
 
Nimeuliza waislamu wengi mno sipati majibu

Kwa nini mnabusu jiwe?
kila ishara ktk Mambo yahusuyo IMANI, huashiria taarifa fulani.
Kubusu jiwe, ni tendo la imani. Linamaana kubwa ktk Uislamu.
Ngoja kidogo wajuzi wa hili watakupa majibu sahihi.
 
Umeuliza nini kuhusu hii mada ambacho hujajibiwa? kila kitu humu kimejibiwa na kila mmoja kwa uelewa wake.

Unauliza kutaka kuelewa au unauliza kutaka uchokozi? Uliza tutakujibu kwa kadiri ya kuuliza kwako.
Maswali yenye viashiria vya uchokozi, si vema kuyatolea majibu.
hata kukaa kimya ni jibu pia.
 
Back
Top Bottom