Haya, twende kazi.
Kama baba alikuwa genius kuna kila uwezekano akawa amerithi kwa baba. Bado hujaonyesha ushahidi wowote ule kwamba mtoto hawezi kurithi akili kutoka kwa baba. Bado hujaonyesha.
Si unadai umesikiliza? Sasa kama umesikiliza kwa nini unaniuliza tena? Wewe ulichosikia ni nini? Halafu umesikiliza au umetazama?
Is this a rhetorical questions?
What's this got to do with what we are discussing about?
Haya, soma hiki kipande kwa umakini (hususan hicho cha pili) na ikiwezekana rudia kusoma hata mara tatu na ambapo hutaelewa niulize nikueleweshe. Sawa? Haya soma sasa.
Intelligence inapimwaje kwani?
Na kwanza wao wala hawakutakiwa wawe ma geniuses kama ilivyokuwa kwa ma sperm donors. Kwa akili ya kawaida tu naweza kusema walitakiwa wasiwe wendawazimu among other things lakini si kuwa extremely intelligent au "genius square".
Hii kauli yako inapingana na madai yako kuwa watoto wanarithi akili za mama zao.
Kama ana akili alizozirithi kutoka kwa mama yake kwa nini a-behave hivyo ilhali yeye si mjinga? Hizo akili alizorithi hazimtoshi kubaini kuwa ulivyomwita mjinga hayuko hivyo?
Kwa taarifa yako hao watoto walikuwa observed kuanzia wakiwa wachanga. Na sijui kama umewahi kupeleka wanao (nasadiki unao kadhaa, kama huna niwie radhi) kwa pediatrician? Pediatrcian hakuwa ana track development yao na kukupa percentile ranking?
Mara nyingi watoto wenye akili nyingi huwa wanaonyesha uwezo mkubwa tokea wakiwa wadogo sana. I have one so I know what I'm talking about. Mtoto wa miaka 2 akiwa na verbal skills za mtoto wa miaka 7 au 8 si sawa na mtoto wa miaka 2 aliye na verbal skills za mtoto wa miaka 3 au 4.
Ku behave kama genius hakumfanyi mtu awe genius. Nakubali kwamba kutia mtu moyo huwa kunaleta matokeo chanya lakini pia ili hayo matokeo chanya yatokee ni lazima kuwepo na fundamentals. Kwa hiyo hata uambiwe una maakili kumzidi Einstein wewe kama hesabu hazipandi ni hazipandi tu.
Haikuwa study. Ilikuwa ni project. Na sidhani hata unasoma vizuri ninayoyaandika.
Kwa kifupi, watoto waliozaliwa kwenye hiyo project bado wapo hai. Na miezi kama miwili iliyopita CNN walirusha documentary kuhusu hiyo project na matokeo (watoto) yake.
Story highlights za hiyo documentary hizi hapa:
Sasa bonyeza
hapa uende moja kwa moja kwenye tovuti ya CNN ilipo hiyo makala ambako pia kuna clips kadhaa za hiyo documentary.
Haya niliyaongelea jana na inavyoonekana hata hukuyasoma. Kama uliyasoma basi ni ama umeyasahau au hukuyaelewa.