Je, kuna uhusiano wotote kati ya nyumba unayoishi na kufunguka mambo yako?

Je, kuna uhusiano wotote kati ya nyumba unayoishi na kufunguka mambo yako?

Hii ni kweli, kuna nyumba nimewahi ishi dom kwa miaka sio pungufu ya minne na nilikua wakwanza kuingia baada ya kukamilika. Nikiwa kwenye ile nyumba sikufanya kitu chochote cha maana zaidi ya kulipa kodi na kula, majanga ndio usiseme ukipata hela tatizo linatokea linafyeka ela yote nikawa najiuliza au ni mimi tu kumbe sikuwa napitia hali hiyo peke yangu na baadhi ya majirani nao ni hivyo hivyo. Tukashauriana na jirani mmoja tukahama baada ya hapo unafuu ukawepo.
 
Nyamba nyingi zimezindikwa, wenye nyumba wana imani za kishirikina huchimbia ushirikina maeneo ya nyumba ndani na nje ya nyumba. Binafsi nimeshafukua vitu vya kishirikina nyumba kadhaa nilizoishi. Mambo ni mengi kwa kweli na yanaathiri wapangaji. Kikubwa ni kugundua na kuhama
 
Hii ni kweli, kuna nyumba nimewahi ishi dom kwa miaka sio pungufu ya minne na nilikua wakwanza kuingia baada ya kukamilika. Nikiwa kwenye ile nyumba sikufanya kitu chochote cha maana zaidi ya kulipa kodi na kula, majanga ndio usiseme ukipata hela tatizo linatokea linafyeka ela yote nikawa najiuliza au ni mimi tu kumbe sikuwa napitia hali hiyo peke yangu na baadhi ya majirani nao ni hivyo hivyo. Tukashauriana na jirani mmoja tukahama baada ya hapo unafuu ukawepo.
Mie nmekuja kuunganisha dots leo
 
Habari,

Dah leo nimekumbuka jambo ambalo lilishawahi nitokea miaka 7 nyuma sasa katika kuunganisha kwangu dot naona kuna kitu ambacho naweza kuwa sahihi ama la hasa kwenye swala la nyumba zetu hizi za kupanga na upatikanaji wetu wa ridhiki. Na hizi ndo historia ya nyumba nlizokaa kwa upande wa ridhiki

1: Hii nilikuwa nakaa magomeni mapipa dah bwana hii nyumba ilikuwa ukipata hela nyingi kwa week basi ni elfu 50 na kuumwa kila siku kama ni chuo basi ilifikia kipindi nkawa na sapu mpaka 3 dah sema nlihama kwa mbinde mno full uswahili nyumbani mpka mtaa mzima

2: Kinondoni
Hapa nlihamia nkiwa chuo mwaka wa kwanza semester ya 2 hapa nili clear sapu zangu zote na mwishoni wa semester nilifanikiwa kununua gari nikiwa mwanafunzi na siku na ajira rasmi bali mission town tu.

Mpaka kufikia mwaka wa pili semester ya pili nlikuwa na gari zangu mbili huku mitikasi yangu ikienda vizuri mno mpaka nikaamua kuchange kutoka full time kwenda night chuoni.

Mungu si athumani ile nyumba ikauzwa so ikabidi nitafute nyumba nyingine ilala.

3 ILALA
Hapo ndo kimbembe kilipoanzia kwani niliingia nikiwa na gari tatu mambo yalikuwa yanakwenda hovyo mno, ilikuwa inafikia kipindi mpaka hela ya kula huna gari zote zikauzwa kwa hasara ikawa ni mtu wa daladala hela haipatikani kabisa ukipata tu hela ujue kesho ni siku ya kodi au ya kula tu ila maendeleo zero.

Kila ukitaka kuhama misuko suko au unakosa kabisa hela hela yani ukitoka tu kwenye kazi zako unamkuta mwenye nyumba kibarazani hali hyo ilidumu kwa miaka 3 kila nikisema niondoke inashindikana lakini mungu si athumani nikahama .

Ajabu baada tu ya kuhama mambo yakaanza kurudi tena vizuri walau ya kupata maendeleo inapatikana.

Je hii ni kwangu tu au kuna wenzangu ilishawahi watokea?
Chukuaudongokachanganye na wamposa tupia kwakoo njoo unianbiee
 
Ni kweli kabisa kuna nyumba zingine zina maagano mabaya au zipo kwenye mitaa yenye maagano. Kwa mfano usikae kabisa kwenye nyumba ambayo ipo kwenye mtaa ambao barabara haitoki
Mkuu nimejenga nyumba kwenye close, maana yake nini kwamba nisiishi hapo? ata kama ni nje ya TZ?
 
mimi nimefiwa mpaka na mtoto na nimefilisika biashara kariakoo nyumba ilikuwa kigogo luhanga nishakula sana makofi ndani anayekupiga humwoni kila nikitaka kuhama hela hamna ukija kupata mwenye nyumba huyu hapa anataka hela yake acha tuu hizi nyumba zina mengi.
Duh hatari pole sana mzee
 
mwenza sawa lakini nyumba ina uhusiano gani na uchumi wako? Maana shughuli zako hufanyii nyumbani!
Zina negative energy zinafukuza baraka zako.
Ni kama ilivyo uswahili utoboi kama wewe sio mwanga.
Sababu ya chief satanists au mkuu wa wachawi wa eneo Hilo kaset standard mstari Fulani wa maisha wakazi wa eneo Hilo wasivuke.Mfano hakuna atakaemilki gari,kufika chuo kikuu,olewa nk.
Kuyashinda maagano ni either uwe na nguvu kuzidi wao.
 
Mbaraka mwinshee aliimba kitu halisi.
Mtaa WA Saba.
Mswahili kwa bidii anachoweza ni ngono na uchawi.
Uchawi na ngono ni pacha,maana ngono ni ibada katika uchawi
 
Nyumba zina maagano, kuna nyumba wahusika wamezindika vitu, or alikua anaishi kaacha mambo yake. So ukihamia ardhi hakukubali unasota. Nyingine inakukubali mambo yananyooka. Ni kuomba Mungu tu
Nyumba zinajengwa kwa damu za watu.
 
Hatuswali
Hatusali
hatuna hata mda yaani ni kuamka kuendelea na shughuli zetu ukirudi usiku unalala tutaacha kuwa na mikosi kweli
 
Back
Top Bottom