Uchaguzi 2020 Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Watu wamelisoma bandiko lote kweli ama wamuamua tu kumpa za uso jamaa! Nimesoma hapa "...Au ndio wanatangaza nia ya kugombea urais kupitia Chadema ili kuutumia ugombea huo kama ngazi ya kujisuru kipigo cha CCM kwa kuwaonyeshea wapiga kura kuwa wao ni presidential materials, hivyo kama wangeweza kuwa rais wa JMT kupitia Chadema, then ubunge ni nini compared?, hivyo kuwapa mileage zaidi ya kuchaguliwa ubunge?...." na kuona mambo mawili ambayo muandishi ameyaandika. Mosi, kujinusuru na kipigo na mbili kupata mileage zaidi ya kuchaguliwa. Wala hajahitimisha moja kwa moja kuwa wanakwepa kutogombea ubunge!!
Alipoharibu muandishi ni kumung'unya maneno kwenye aya ya kwanza, pale aliposhindwa kuwa muwazi kuhusu sababu ya upinzani kushindwa uchaguzi mkuu ujao!
 
Uchaguzi ni namba, aache kuaminishwa kitu ambacho hakipo...kwn kushindwa kwenye uchaguzi ndo nn?? Ukishindwa maisha lazima yaendelee
 
UNAFIKI wa Pascal NJAA Mayalla


 
Bora hata wewe bado ulikuwa unamheshimu huyu MPUMBAVU mimi nilishamdharau siku nyingi sana. Hajitambui kabisa ni mmoja wa waandishi wa habari Nchini ambaye AMEIDHARAULISHA sana taaluma ya wanahabari kwa UNDUMILAKUWILI na NJAA ZAKE. Anajirusha huku na kule yule dikteta amuone ili ampe ULAJI lakini wapi! Mpumbavu sana huyu jamaa.

Natangaza hadharani kumdharau Pascal Mayalla katika kipindi chake chote kifupi alichobakiwa nacho hapa duniani
 
Samahani ndugu pachal waeleze wabunge wa ccm nao wachukuwe fomu ya uraisi kupitia ccm kwani kuna kosa lolote
 
Hivi ulisema utagombea jimbo gani kupitia CCM, maana toka umesema utuambii unagombea jumbo gani
 
Mayala huchoki tu kupambania teuzi yaani unajipendekeza kama wale wabunge wa viti maalumu walioasi KUB
 
Nikizingatia utangulizi wa bandiko lako nitajikita kidogo tu na aya yako ya mwisho. Dhana kuwa walio na shaka ya kurejeshwa kwenye Uheshimiwa, na wapiga kura, dio hao wametia nia ya kugombea Urais ina, kwa kiasi fulani, na ukweli.

Hakuna ubishi, labda kwa sababu ya kubishana tu, Rais Magufuli amebadilisha maisha ya wanasiasa kimawazo na kimatendo. Anaishi na kutenda ndani ya nadharia ya "utashi wa kisiasa" (political will). Nadharia ya kisiasa ambayo wengi wameshindwa au hawana uwezo wa kuitafsiri kwa vitendo. Nitarejea baadaye kueleza ni kwa nini wengi wa waheshimiwa hawatarudi mjengoni.

Hebu nitoe tafsiri fupi ya nadharia ya"Utashi wa kisiasa" kama azimio binafsi la mwanasiasa kufanya na kusema mambo ambayo yatakuwa na matokeo yanayotarajiwa. Ufafanuzi huu una maana kadhaa muhimu. Kwanza, unaondoa mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa uwezo mdogo wa kisiasa au vyombo vya kiusimamizi ili kufikia malengo tarajiwa.

Kiutendaji, "utashi wa kisiasa" ni nia ya kisiasa au dhamira ya mwanasiasa aliye na madaraka ya kiserikali kutekeleza, kwa vitendo, Sera, hasa ambayo uwezakano wa kufanikiwa mara moja ni mdogo au hakuna kabisa. Mwanasiasa wa aina hiyo yuko tayari kubeba lawama zote iwapo atashindwa kufikia malengo yake. Kwa misingi hiyo, mwanasiasa huyo hutafsiri sera kwa umakini wakati wa utekelezaji wake.

Rais Magufuli ameitafsiri Ilani ya Uchaguzi ya CCM, 2015 kwa umakini sana na kuitekeleza akiamini matokeo yatakuwa yenye kugusa maisha ya wengi.

Wanasiasa wenye kutambua hilo na/au ambao uwezo wao kutafsiri nadharia ya "utashi wa kisiasa" kwa vitendo ni mdogo au hawana kabisa, aidha hawatagombea ama watahamia chama cha Rais Magufuli, wakitegemea huruma yake. Wachache ni hao waliotia nia ya kugombea Urais kwa imani kuwa wanaweza kuwaaminisha wapiga kura kuwa Sera anazotekeleza Magufuli haziwezi kuleta mabadiliko chanya ya maendeleo (Rejea hotuba zao za kutangaza nia ya kugombea Urais zilivyojaa shutuma na lawama tele dhidi ya Rais Magufuli)

Nawaita WAFA MAJI.
 
Naunga mkono hapo kwenye siasa ni sayansi... Lakini pia CCM walifanya jambo la kufanana na hili wanalofanya chadema sasa la watu wengi kujitokeza na kuchukua fomu ingawa malengo yanaweza kutofautiana ila mantiki ni kucheza na akili ya mwananchi (mpiga kura)
 
1) Chama cha siasa kusimamisha mgombea, hata kama mna uhakika hamtashinda, ni jambo muhimu kimkakati. Linaimarisha nguvu ya chama.
2) Magufuli amefanya mengi mazuri, lakini kwa hesabu zangu, ana mengi zaidi ya kuudhi na kukera. Inaonekana na yeye amalijua, ndio maana Magu siyo mshabiki wa chaguzi huru
 
Anajua kabisa kwa ccm haina tena mvuto mbele ya watanzania
 
Wewe nani asiye kujua kuwa ni mpigania ugali? Haitatokea wewe ukatoa mchango wa kulijenga taifa.

Hakuna mtu wa ku kusikiliza huo ugoro wako
 
Aliyepo madarakani ndiye kasababisha wafanye hivyo ndiyo maana wanaeleza weaknesses utawala huu ambao umeshindwa kwelikweli kwenye nyanja zote

Ishu za ulegelege wa vyama vya upinzani umeonesha wazi unafiki maana mimi binafsi naona wapinzani wapo imara ila wale tawala wametumia nguvu ya ziada isiyo ya kisiasa kuwazimisha wapinzani ili wasionekane tena hata katika chaguzi mbalimbali na sasa huu mkuu.

Sema ulegelege wa upinzani niseme ulegelege wa hao unaodai wanaogopwa.
 
Wewe nani asiye kujua kuwa ni mpigania ugali? Haitatokea wewe ukatoa mchango wa kulijenga taifa.

Hakuna mtu wa ku kusikiliza huo ugoro wako
Bila shaka na amini nimekuelewa na nadhani pia umeeleweka na jamii ya JF kuhusu kiwango chako cha kujadili mada. HONGERA SANA - keep it up[emoji111]
 
umeanza kwa mbwembwenikajua nitakutana na uchambuzi makini ndan ya comment hahaha nimeona ni mbwembwe na uchambuzi usio na tija yoyote hata hujui ulichochambua kama unabisha njoo nikuulize swali kutokana na comment yako .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…