Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo:
Hili ni bandiko la swali, kuhusu ideas ya watangaza nia wa urais Chadema. Kama una majibu, karibu uchangie. Nimeanza na angalizo hili kwasababu humu jf tumevamiwa na ma simple minds ambao kazi yao ni kujadili watu badala ya kujadili ideas!. Kumezuka mtindo wa watu kutokujadili hoja iliyo mezani na badala yake kumjadili mtoa hoja!. Tujifunze kujadili mada iliyo mezani na sio kumjadili mtoa mada.
Kuelekea uchaguzi wa 2020, imetabiriwa kuwa kwa huku Tanzania Bara, Wabunge wote wa upinzani hata wakigombea tena, wataishia kupigwa chini na CCM, kufuatia kukubalika kwa CCM kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwaletea maendeleo Watanzania inayofanywa na rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano. Imetabiriwa CCM itashinda uchaguzi Mkuu ujao kwa ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%.
Hivyo ili kuepuka kushindwa kwa aibu, jee kunauwezekano, huku kutangaza nia ya kuwania kuteuliwa na vyama kugombea urais kupitia tiketi ya chadema, kwa baadhi ya wagombea, sio kweli kuwa wanataka kugombea urais kwa dhati, bali kunatumika tuu kama kichaka cha kujifichia aibu ya kugombea na kushindwa Ubunge?, hivyo kuutumia huo ugombea urais wa kupitia Chadema as an excuse ya kutogombea ubunge?.
Au ndio wanatangaza nia ya kugombea urais kupitia Chadema ili kuutumia ugombea huo kama ngazi ya kujisuru kipigo cha CCM kwa kuwaonyeshea wapiga kura kuwa wao ni presidential materials, hivyo kama wangeweza kuwa rais wa JMT kupitia Chadema, then ubunge ni nini compared?, hivyo kuwapa mileage zaidi ya kuchaguliwa ubunge?.
Lengo la kuuliza hivi, ni kufuatia watia nia wakizidi kumiminika Chadema licha ya kumjua mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ni mtu wa namna gani, na amefanya nini, na wewe unajijua ni mtu wa namna gani, unawezaje kathubutu kuchukua fomu kuomba kuteuliwa Chadema kumkabili Magufuli?.
Nilidhani wana Chadema, baada tuu ya kumsikia Tundu Lissu ametangaza nia, then haikutarajiwa kama kuna mtu mwingine yoyote Chadema angethubutu kuchukua fomu kwa upinzani kufutia upinzani legelege uliopo nchini Tanzania kiasi kwamba kwa maoni yangu, ndani ya kambi nzima ya upinzani, watu pekee ambao wanaweza kumkabili rais Magufuli na aka feel angalau ka joto joto cha uchaguzi, ni Tundu Lissu na Zitto Kabwe pekee, hivyo hawa wagombea wengine wanao omba kuteuliwa Chadema, are they serious kweli au wanagombea tuu ili na wao kuonyeshea ni presidential materiale?!.
NB. Leo ninapozungumza haya, sii wengi wanajua kuwa kuna baadhi ya wabunge wa majimbo wa Chadema, hawatagombea tena uchaguzi wa 2020, hivyo namna nzuri ya kutogombea kwa heshima ni kugombea urais!. Lakini kwa wale ambao hawatapitishwa kwenye urais na kuendelea kugombea ubunge, then bandiko hili haliwahusu!.
Jumatatu Njema.
Paskali
Rejea
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!.
Elections 2020 - Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!