Amri ya 6 inasema Usizini. Amri ya 8 inasema Usiseme Uwongo. Amri ya 9 inasema usitamani mwanamke asiye mke wako.
Hizi amri zinavunjwa sana kuliko kawaida. Unatoka kuungama hata masaa mawili yaliyopita ushavunja moja kati ya hizo.
Hivi kwani wanawake hawatamani waume za watu? Kwanin wawe 'exempted' kwenye amri ya 9? Inatakiwa wahusishwe nao.
Hivi kuna haja gani ya kuwa na amri ambazo zinavunjwa mara kwa mara?
Kwanin kusiwe na haja ya kuzipitia upya kuendana na mazingira ya sasa?
Mkuu piga astaghafirullah tafadhari umuombe Mola wako msamaha kwani agizo la Mungu halibadiliki unless tunazungumzia Mungu tofauti. Hata Yesu (Issa ibn Maryam AS) aliwaambia hakuja kuitengua torati ila kuikamilisha na mfano mmoja wapo wa kuikamilisha ni pale walipo mletea mwanamke mzinzi na kusema kwa sheria yetu ya Mussa (AS) huyo ni mawe hadi afe. Majibu yalikua asiyekua na dhambi aanze kurusha jiwe............moral of the lesson
1. Kwa sheria/maoni ya mayahudi mzinzi ni mwanamke
2. Mfumo dume
3. Man is arrogant
4. Sinner is judging a sinner etc etc
Sasa kukamilishwa kwa torati na bwana mkubwa ni;
1. Ni sawa kabisa kumpiga mawe ila je mwanamke huyu amejizini mwenyewe?
2. Kama jibu ni hapana yuko wapi aliezini nae?
3. Je torati insema mwanamke tu ndo auwawe?
4. Je ninyi ni waadilifu wa kutoa hukumu?
Unaweza kuona yule wanaomuita Mungu (Yesu - of course let's not debate on that )lakini hapo unaona haku-review hiyo sheria ila ameifadanua hiyo sheria juu ya utekelezaji wake.
Halafu mwisho juu ya hiyo amri inayosema "usitamani mke wa mwenzako" na unahoji kwani mwanamke hatamani mume wa mwenzake, jibu wanatamani tena mkuu hata hapa kwenye daladala nilipokaa niko nimekaa na mke wa mtu halafu ananishobokea kinoma hivi nafikiri sijui niahirishe kwenda kazini nikampige mikasi [emoji39] [emoji39] . Anyway that's not the point ila mkuu, Mungu katika maandiko yote maagizo amepewa MWANAUME and you can read/find out from injili, torati, quran etc etc etc na hapa usiumize kichwa anglia kutoa uumbaji, Mungu alimfanyiza kwa mikono yake MWANAUME vilivyobakia viliamlishwa viwe vikawa , manabii wote ni wanaume. Hivyo mkuu usitamani wake za watu na kumbuka MWANAUME NDIO CHANZO CHA MABADILIKO