Je kuna uwezekano yaliyosemwa kwenye Biblia na manabii wa Mungu yanatimia kwa sasa?

Je kuna uwezekano yaliyosemwa kwenye Biblia na manabii wa Mungu yanatimia kwa sasa?

IIS

Member
Joined
Jun 11, 2024
Posts
89
Reaction score
171
Habari za wakati huu popote ulipo.Je yaliyosemwa kwenye biblia yanatimia kwa sasa?

Katika biblia kuna ujumbe juu ya ishara na matukio mbali mbali yatakayo tokea kipindi tunaelekea wakati wa ujio wa mwana wa Adam.

Biblia imetaja juu ya vita kati ya taifa na taifa,falme na falme na kuendelea.Ukiangalia mpaka sasa unaweza kuona kama nyakati zinaweza kuwa hizi(nani ajuaye).Tutafakari kwa pamoja.

Wakati huu tuna siku ya pili Thailand na Cambodia kimenuka,tumetoka kuona machache kati ya Israel na Iran,Israel na Gaza , Lebanon akijumulishwa ndani yake.DRC kidogo aingie mkenge kwa Rwanda,Urusi na Ukraine mpaka sasa hakuna suluhu,Taiwan na China waliingia mitini baada ya kutangaza pambano,India na Pakistan walipasha kidogo misuli na kwingineko huko duniani.

Matukio yanazidi kuwa mengi ambayo yanafanya kuona kama unabii unatimia wa siku za mwana wa Adamu kuja.Chukua hatua,ombea amani ya dunia na taifa lako pia
 
Hata tukiombea hatuwezi kubadilisha,ili maandiko yatimie!
Cha muhimu tujitakatifuze ili tujaaliwe kuwa na mwisho mwema!
 
  • Thanks
Reactions: IIS
Hata tukiombea hatuwezi kubadilisha,ili maandiko yatimie!
Cha muhimu tujitakatifuze ili tujaaliwe kuwa na mwisho mwema!
Kutumia kama yalipangwa lazima iwe hivyo lakini kuna kitu huwa wanasema kuombea mwisho mwema ndio jambo la msingi.Maana unabii kama kutumia lazima utumie(muda na wapi hakuna ajuaye)
 
Back
Top Bottom