Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Zamani wakati dola ya Rumi ni jamuhuri, walikuwa wanafanya uchaguzi kila mwaka. Kila mwaka walikuwa wanachagua viongozi(consulars) wawili kuwaongoza.
Hawa walikuwa ni watu walioonyesha uwezo wa kiuongozi na kivita na walipitia ngazi kadhaa hadi kufaa kuchaguliwa uconsular. Maconsular hawa walikuwa wanaangaliwa kwa ukaribu sana na senate.
Sasa basi, ikitokea dharura, hasa vita kubwa. Maconsular hawa walikuwa wanapewa nguvu ya kidikteta. Walipewa nguvu za kufanya watakavyo kwa manufaa ya nchi, na hata kipindi cha mwaka mmoja ilivyo kawaida kingeweza kuongezwa.
Shule tulikaririshwa tu kuwa demokrasia ni nzuri na udikteta mbaya. Bila ya kujulishwa faida na hasara ya kila moja(Elimu ya mchongo tulipewa).
Sasa, kuna faida zozote za utawala wa kidikteta? ni wakati gani utawala wa kidikteta unafaa zaidi?