Aziz Ki Mayele
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 899
- 1,955
Imekua kawaida kila mechi unapoibuka mjadala wa Feisal Yanga imekua ikipata ushindi wa kishindo
Mechi ya Azam na mechi za CAFCC zote zilizotanguliwa na mijadala hii zimekua za neema nyingi kunako club hii ya jangwani
Sasa mjadala huu umeibuka tena kuelekea mechi ya dabi baina ya Simba na Yanga, na kwa mujibu wa vyanzo vyangu timu ya Yanga inayafurahia sana mazingira haya especially kwa wachezaji wao wa kutumainiwa Mayele na Aziz
Baada ya Simba kupata dokezo hili kutoka kwa mnajibu nyota maarufu huko Morogoro, kumekua hakukaliki huko msimbazi na wasiwasi umetanda huku ikitanabaishwa baadhi ya wachezaji wamejifanya kuumia ili kuepuka dhahama inayokuja
Simba pia wamejitahidi sana kuuzima mjadala huu kwa kuweka press conferences na kuibua mada nyingine mbalimbali lakini Yanga wamekomaa kuuendeleza mjadala mpaka hapo mechi ya dabi itakapoisha.
Hii ni nyota njema imewaka kwa Yanga na ushindi sasa ni wazi na hakika kutokana na ishara hizi za wazi
Kongole za awali Yanga Afrika kwa ushindi mtakaoupata hapo jumapili
Wasalaam