Mungu atusimamie kwa Kweli, umeongea yaliyo ya kweli na Hakika!Mpendwa Mwafrika mwenzangu,
Leo nakuandikia tafakri yangu binafsi, lakini pia kwa tumaini. Uchungu kwa sababu kuna jambo linaloendelea kwenye jamii zetu ambalo linatufanya tusisonge mbele kama tunavyopaswa. Tumekuwa watu wa kutafuta, lakini si watu wa kuendeleza. Tumekuwa hodari wa jasho, lakini si wa maono. Tumekuwa wakali katika kujenga, lakini dhaifu katika kurithisha.
Tuna tatizo kubwa.
Na tatizo hili ni kutojua maana ya urithi. Tunajua kutafuta mali , mashamba, nyumba, biashara ,lakini hatujui kuiweka katika misingi ya kudumu. Mara nyingi, mtu anahangaika maisha yake yote, anajenga kitu kizuri, halafu akifariki, mali zile zinatafunwa na migogoro ya kifamilia, tamaa, na hata uchawi. Mali inatafunwa na moto wa hasira, chuki, na ubinafsi. Haipiti muda, yale yote yaliyotafutwa kwa miaka mingi yanayeyuka kama barafu kwenye jua.
Kwa nini inatokea hivi?
Kwa sababu hatuna utamaduni wa kuweka msingi wa mali kuwa mali ya vizazi. Hatufundishi watoto wetu thamani ya juhudi. Hatuna maono ya mbele. Tunafikiria ‘leo’ tu , kula, kuvaa, kujionesha ,lakini hatufikirii ‘baada ya mimi’, hatufikirii urithi. Tumezoea kusema, "watatafuta wao wenyewe kama mimi nilivyotafuta." Lakini huo si utamaduni wa maendeleo ni utamaduni wa kurudia umasikini kizazi hadi kizazi.
Sasa tuangalie jamii nyingine:
Waarabu, Wahindi, Wayahudi hawa hawachezi na mali za familia. Mtoto analelewa tangu mdogo kujua biashara ya familia, anajua utaratibu wa mirathi, anapewa elimu ya kusimamia mali, na kuna mfumo wa kuhakikisha utajiri unadumu kizazi hadi kizazi. Mtoto hufundishwa, "hii si yako pekee ni ya ukoo, na ukoo ni wa vizazi vijavyo." Huu ni msingi wa fikra za kizazi, si fikra za mtu mmoja mmoja.
Sisi je?
Badala ya kushirikiana, tunagombana. Badala ya kuwekeza, tunafuja. Badala ya kushirikisha watoto katika ujenzi wa familia, tunawaficha kila kitu hadi tunapokufa, halafu wanarithi mali bila maarifa na wanaiangusha kwa mikono yao. Na kibaya zaidi, tunaanza kulogana. Tunaona maendeleo ya ndugu si baraka ni tishio. Tunalogana, tunaombea mabaya, tunatamani waanguke , halafu tunabaki tunashangaa kwa nini hatuendelei kama jamii.
Ni wakati wa kuamka.
Ni lazima tubadilishe fikra zetu. Tusifurahie kuwa na mali, tukose mipango ya urithi. Tunahitaji,
Mali inapaswa kuwa ya kizazi na si ya mtu mmoja.
- Kuweka maandishi ya mirathi,
- Kuwekeza kwa ajili ya watoto wetu,
- Kuwashirikisha watoto katika kujifunza biashara na mali,
- Kuacha chuki, husuda, na uchawi,
- Kujifunza kushirikiana badala ya kugombana.
Maendeleo ya kweli ni yale yanayoishi hata baada yetu kuondoka.
Tuamke,tujenge msingi,tuweke urithi imara. Kizazi kijacho kitatushukuru ama kitakulaani kwa sababu ya uamuzi wako leo.
Usikubali mali uliyojenga kwa mateso ipotee kwa sababu hukuweka msingi wa kuendeleza.
Kwa upendo, wasiwasi, na msisitizo wa dhati,
~Mwanenu Chavalikungu!.
Laana ni nini?Mpendwa Mwafrika mwenzangu,

Hongera ,hope na wajukuu zako wataziendeleza mali zako ,nawengine wenye mtazamo watajitafutia zakwao na hivyo koo zenu hazitakabiliwa na umasikini!Hakuna cha laana babu yangu alitafuta pesa huko Kenya ,watoto wake 9 wakiume wote wameziendeleza , halafu kuna mimi mjukuu wake sikutaka mambo ya ukoo , now najaribu kukimbiza ukoo wote , usichukulie poa watu weusi wa humu kaka.
Yaani jamii zetu tunahitaji sana kujikomboa, makabila mengine hata kurudi kujenga kwao n kosa wanaogopa kuuwawa kiushirikina !,hii inadumaza sana akiliUko kwenye akili yangu, ndio ninacho zungumza kila ninapopata nafasi, tunashinda kuondoa minyororo ya umasikini kwa namna hii
Hizi ni njia potofu,kule Mbeya kuna Muhindi ana maroli yameandikwa kanji lalji miaka ya 1985,Nilidhani Yuko hai Kumbe alifariki kitambo! Kampuni hiyo ipo hadi Sasa,2025,Wanaoiendeleza ni vitukuu!Naam mkuu haya yapo kwenye jamii zetu kabisa ,Vijana wanaachiwa nyumba wanagombana mpaka wanauza kila mtu afe na chake 😆,halafu wanarudi kupanga nyumba tena
Hilo nalo Neno,ila hizo za bank,zinaendelezwaje?Laana - ni nadharia isiyo halisi .
Kuhusu mali
Babu yangu before hajafariki alisema hakuna kurithi Mali na hakuna kugawanya Mali na hakuna kuuza.
Na hela alizokuwa nazo zilibaki bank kwa maagizo maalumu kuwa zitumike kusomesha watoto na hela italipwa Shule direct na sio MTU kupewa mikononi.
Ili uendeleze Mali zako baada ya wewe kuondoka ondoa swala la kuzigawa Ila weka mfumo wa kuzifanya Mali ziwe za familia na sio watoto fulani au MTU Fulani.
Kwahiyo mpaka Leo zile Mali Kama Mashamba makubwa ya miti , Nyumba n.k bado zipo na zimefanyia maintenance nzuri.
Asilimia kubwa ni asilimia ngapi na uliipataje?narekebisha nilizungumza kwa mtazamo katika asilimia kubwa mkuu naomba unielewe hivyo🙏,
Hizo za bank hazikuisha tulitumia hadi wajukuu .Hilo nalo Neno,ila hizo za bank,zinaendelezwaje?
Mno mkuuHongera ,hope na wajukuu zako wataziendeleza mali zako ,nawengine wenye mtazamo watajitafutia zakwao na hivyo koo zenu hazitakabiliwa na umasikini!