Habari zenu wanajamvi,
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wanaJF wote, zaidi sana wale walijitokeza nilipotoa tangazo la kutafuta Mr. Right.
Napenda kuwataarifu kuwa tumeendelea na mikakati na taratibu za harusi na my Mr. Right ambaye nilimpata kupitia tangazo langu la mwezi Jan.2016,
binasi sikutarajia kama mambo yatakwenda kwa speed kubwa namna hii lakini ndivyo ilivyokuwa.
Taratibu zote zimekamilika na Jana tu ndo mahari yote imelipwa, kweli nina furaha na amani sana kwa hatua niliyofikia, namshukuru mchumba wangu kwa seriousness alionionesha.
Wandugu tarehe ya harusi imepangwa na Jumapili ya tarehe 6 march 2016 tangazo la kwanza la harusi yangu litatangazwa.
Tarehe ya harusi imeshapangwa na vikao vinaanza kesho, naomba tarehe nisiiweke wazi kwanza, nitaiweka wazi siku tatu kabla ya harusi. Asanteni
sana.
Wewe ambaye umetupia tangazo lako amini tu utampata unae mtaka.Usichoke wala kukata tamaa.