Sajo
Platinum Member
- Nov 8, 2010
- 4,540
- 8,256
Jibu ambalo utalisikia mara nyingi si kwamba wanachukia sheria, bali wanahisi wanaweza kubambikiwa makosa au kutozwa faini hata pale wanapoamini hawajakosea.
Badala ya askari kuonekana kama walinzi wa usalama, kwa baadhi ya madereva wamekuwa ishara ya usumbufu na hofu kila wanapoanza safari.
Kisheria, utaratibu uko wazi. Kwa mujibu wa Jedwali la 1 la The Road Traffic (Specified Offences) Order ya 1985 Government Notice 339 of 1985 ambapo haijafutwa mpaka sasa, ikisomwa pamoja na kifungu cha 109 cha THE ROAD TRAFFIC ACT, CHAPTER 168. R.E 2023, inaonesha uwepo wa FOMU YA POLISI Na. 101 (NOTIFICATION) ambayo kazi yake ni kutoa taarifa kwa dereva iwapo anatuhumiwa kutenda kosa la barabarani. Fomu inaelekeza kuwa kama dereva atakiri kutenda kosa hilo basi atatakiwa kujaza SEHEMU B ya fomu na kulipa faini (kwa sasa kiwango ni Tshs. 30,000/=), au kama hatakubali kosa, ajaze SEHEMU A na jeshi la polisi litamfikisha mahakamani kujibu mashtaka kuhusu kosa alilotenda.
Kupitia Police Form No. 101 (PF.101), dereva anayeshukiwa kutenda kosa ana haki ya kulikubali au kulikataa. Akikubali hulipa faini, lakini akilikataa anatakiwa kufikishwa mahakamani, kwa kuwa mahakama ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kumtia mtu hatiani. Askari anatakiwa kuwa mtekelezaji wa sheria, si mwamuzi wa hatia.
Tatizo linalolalamikiwa ni kwamba, baada ya kuanzishwa kwa matumizi ya mashine za POS, madereva wengi hudai hawapewi tena nafasi ya kukataa kosa na kupelekwa mahakamani. Mara nyingi huandikiwa faini papo hapo, huku wengine wakichagua kutoa rushwa ndogo ili kuepuka faini kubwa.
Mfumo huu umeibua malalamiko kuwa umeongeza mianya ya rushwa badala ya kuimarisha utekelezaji wa sheria.
Iwapo hali hiyo ipo, basi athari yake ni kupungua kwa imani ya wananchi kwa vyombo vya dola na kudhoofisha dhana ya utawala wa sheria.
Mtu anayeshutumiwa anapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa na mahakama, si kuonekana amehukumiwa papo hapo na anayemkamata, isipokuwa yeye mwenyewe mtuhumiwa akiamua kukiri kosa papo hapo alipokamatwa. Hiyo ndiyo haki ambayo sheria ilikusudia kuilinda.
Sasa, suluhisho la hili, halipo katika kuondoa askari barabarani, bali katika kuboresha mfumo. PF. 101 itumike kama sheria inavyoelekeza, na kwa mazingira ya sasa, askari wavae body cameras kuongeza uwajibikaji.
Pia kuhusu kudhibiti spidi barabarani kamera za kudumu zitumike kupima mwendokasi badala ya zile za mkononi (tochi), na Jeshi la Polisi liweke nguvu zaidi kwenye elimu ya usalama barabarani. Hatua hizi zinaweza kurejesha imani ya wananchi na kufanya sheria itekelezwe kwa haki kwa kila upande.
Ukiwa mtumiaji wa barabara, ni kero zipi umewahi kukumbana nazo kutoka kwa askari polisi wa usalama barabarani?
Lusajo Mwakasege - 0713368153