Je, kwa Tsh Milioni 40 tu GENTAMYCINE 'nikijibanabana' naweza Kuitumia Kukamilisha yafuatayo?

Je, kwa Tsh Milioni 40 tu GENTAMYCINE 'nikijibanabana' naweza Kuitumia Kukamilisha yafuatayo?

1. Kununua Uwanja wa Ujenzi wa Tsh Milioni 4 na Laki Saba na Elfu Hamsini ( Tsh 4,750,000/= ) maeneo ya ndani ndani kiasi Kinondo, Mingoyo, Vikawe na Mapinga.

2. Kununua Ramani ya Nyumba Shilingi Laki Mbili na Elfu Hamsini ( Tsh 250,000/= )

3. Kujenga Nyumba ya Vyumba Vitatu kwa Tsh Milioni 25 huku na Gharama ya Ufundi / Mafundi ( Labour Charge ) ikiwemo

4. Kuiwekea Madirisha ya Kawaida na Kununulia Makochi, Vitanda, Jiko la Gesi, Masufuria, Ndoo, Vjiko, Umma, Upawa, Mabeseni, Friji, Makabati, Meza ya Chakula kwa Tsh Milioni 8.

5. Kuvuta Umeme na Maji kisha kuweka Taa ( Bulbs ) pamoja na Kuweka Feni za Kawaida tu kila Chumba ili wakati wa Joto Kali la Dar es Salaam nisibanikwe nalo.

Ukweli ni kwamba Kiasi nilichonacho / kilichopo ni Tsh Milioni 50 ila nataka Kujibana kwa Tsh Milioni 40 tu ya kufanya yote hayo niliyoyataja hapa juu ili hii Tsh Milioni 10 itakayobakia niitumie kwa Kununulia Pikjpiki ( Bodaboda ) zangu Nne ( 4 ) tu au niiweke katika Mfumo wa UTT AMIS ili niwe napata Interest ( Faida ) ya kila baada ya Miezi Minne au Miezi Sita au kwa Mwaka ( Miezi Kumi na Mbili ) tu.

Tafadhali karibuni nyote katika Kuniongoza na Kunishauri vyema katika hili Jambo langu la Kimaendeleo baada ya Kuzichangachanga Kiubishi.

Pia kuwa Huru kabisa nawe pia kuja na Mtiririko wako ( kama ambao Mimi nimeutoa ) hapa juu ila hakikisha tu hutoki ndani ya Kiasi hicho cha Pesa cha Shilingi Milioni Arobaini ( Tsh 40,000,000/= )

Karibuni na Nitawashukuruni mno. Na tambueni Nyumba niitakayo ni ya Kawaida ( ya Maisha yangu tu ya Kawaida ) na si ile ya Kitajiri ( Kifahari ) kama mlizonazo wana JamiiForums wote hapa.

Ninaungana na TEC 100% kwa Tamko.
Kuna mhuni atakuja kuropoka hapa kuwa hela hiyo haitoshi hata msingi.

Huku kalala kwenye godoro kuukuu nyumbani kwa baba yake pembeni na choo cha shimo cha kutapisha
 
Asante ila Ungenifafanulia zaidi Kimtiritiko ningeshukuru.
Mimi si mtaalamu wa ujenzi ila nimetumia uzoefu wangu wa kujenga jenga vijumba vya saizi hiyo tena mikoani ambako vifaa vya ujenzi ni bei juu kuliko huko unakotaka kujenga.
 
Unaweza tumia hata 20m ....ukapata nyumba nzuri sana....halafu 20 nyingine ukaweka kwenye biashara....ambazo wengi wanaona za kiduanzi....genge...pombe za kienyeji...supu...mishkaki....au voop.
 
Inategemea ukubwa wa nyumba. Ila kwa nyumba ya vyumba vitatu sebule jiko na dining, Hiyo hela utaishia kwenye kukamilisha boma lililoezekwa, kuwekwa magrili, kuwekwa mfumo wa awali wa umeme na maji. Kwenda zaidi ya hapo, sidhani.
 
1. Kununua Uwanja wa Ujenzi wa Tsh Milioni 4 na Laki Saba na Elfu Hamsini ( Tsh 4,750,000/= ) maeneo ya ndani ndani kiasi Kinondo, Mingoyo, Vikawe na Mapinga.

2. Kununua Ramani ya Nyumba Shilingi Laki Mbili na Elfu Hamsini ( Tsh 250,000/= )

3. Kujenga Nyumba ya Vyumba Vitatu kwa Tsh Milioni 25 huku na Gharama ya Ufundi / Mafundi ( Labour Charge ) ikiwemo

4. Kuiwekea Madirisha ya Kawaida na Kununulia Makochi, Vitanda, Jiko la Gesi, Masufuria, Ndoo, Vjiko, Umma, Upawa, Mabeseni, Friji, Makabati, Meza ya Chakula kwa Tsh Milioni 8.

5. Kuvuta Umeme na Maji kisha kuweka Taa ( Bulbs ) pamoja na Kuweka Feni za Kawaida tu kila Chumba ili wakati wa Joto Kali la Dar es Salaam nisibanikwe nalo.

Ukweli ni kwamba Kiasi nilichonacho / kilichopo ni Tsh Milioni 50 ila nataka Kujibana kwa Tsh Milioni 40 tu ya kufanya yote hayo niliyoyataja hapa juu ili hii Tsh Milioni 10 itakayobakia niitumie kwa Kununulia Pikjpiki ( Bodaboda ) zangu Nne ( 4 ) tu au niiweke katika Mfumo wa UTT AMIS ili niwe napata Interest ( Faida ) ya kila baada ya Miezi Minne au Miezi Sita au kwa Mwaka (Miezi Kumi na Mbili ) tu.

Tafadhali karibuni nyote katika Kuniongoza na Kunishauri vyema katika hili Jambo langu la Kimaendeleo baada ya Kuzichangachanga Kiubishi.

Pia kuwa Huru kabisa nawe pia kuja na Mtiririko wako (kama ambao Mimi nimeutoa) hapa juu ila hakikisha tu hutoki ndani ya Kiasi hicho cha Pesa cha Shilingi Milioni Arobaini ( Tsh 40,000,000/= )

Karibuni na Nitawashukuruni mno. Na tambueni Nyumba niitakayo ni ya Kawaida ( ya Maisha yangu tu ya Kawaida ) na si ile ya Kitajiri ( Kifahari ) kama mlizonazo wana JamiiForums wote hapa.
Hongera sana mkuu.

Binafsi naamini inawezekana.

Cha msingi ni kutoruhusu kutoka nje ya bajeti naalengo yako.
 
Kiwanja cha mil 4 utauziwa makaburini labda uende porini kabisa.

Na kujenga kwa mil 25 hapa tena vyumba 3 angalau uwe na 50 nje ya kiwanja
..Halafu kwa nn ukajenge nje ya mji sana huko nunua eneo kubwa sana kwa baadae maana usafiri kama unapiga mishe huko town utakugharimu sana.
 
Unaweza tumia hata 20m ....ukapata nyumba nzuri sana....halafu 20 nyingine ukaweka kwenye biashara....ambazo wengi wanaona za kiduanzi....genge...pombe za kienyeji...supu...mishkaki....au voop.
😅😅😅
 
Mkuu nauza kiwanja Vikawe! Seven kilometers from "bawbaw" secondary school"
 
Hivi hiyo pesa ukizunguka zunguka huwezi kupata nyumba ya kununua hata kama utamaalizia baadhi ya finishing? Mbona naziona sana mitandaoni
 
Back
Top Bottom