Je, kwanini ndoa imekuwa ngumu kufikiwa?

Masharti ya ndoa ndo magumu, yamekaa kiuonevu sana..kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuvumilia.

Labda utaratibu wa ndoa ubadilishwe.
Watu wanaingia kwenye ndoa kwasababu jamii imewataka wafanye hivyo.
Unadhani ni masharti gani ya ndoa yanayofanya iwe ngumu na ya kibaguzi? Je, ndoa inaweza kufanikiwa bila masharti yoyote au bado inahitaji mwongozo fulani ili iwe imara?
 
Tafiti yangu ndogo japo sio uhakika 100% , wazazi wetu wanajua kuchagulia watoto wao wenza wanaoendana nao kwa sana .

Unaweza kwenda mji mwingine kwa ajili ya kusoma ,ukakutana na mtu mnapendana ila kwenye uwanja wa ndoa hamuendani kutokana na asili yenu ...Arranged marriages ndiyo mfumo wa India .Sasa angalia divorce rate yao ni ndogo hakuna duniani..​
Je, unadhani sababu kuu ya divorce rate ndogo kwenye ndoa za kupangwa ni kweli watu wanaendana, au ni kwa sababu tamaduni zao haziwapi nafasi ya kutoka kwenye ndoa hata kama mambo hayaendi vizuri?
 
kwanza feminism imemwamimisha mwanamke ku-play role yake ya submissive ni utumwa kwaiyo moja kwa moja nguzo kuu ya maelewano haipo tena hapo

SIo mbaya mwanamke kujitegemea au kuwa na chanzo cha kipato. Lakini iyo haiendani na zile kanuni zilitumika kutengeneza msingi wa ndoa. Katika muundo wa ndoa mwanaume anaangiliwa kama provider kwaiyo anawajibika kwenda kutafuta ugali wa familia, mwanamke anaangaliwa kama receiver hivyo anabaki nyumbani kuangalia familia.

Sasa tukitumia kanuni ya 50/50 kwamba wote waende kutafuta maana yake inabidi tufanye marekebisho ya mfumo wa ndoa kwa kumwondolea mwanamke ile privilege ya reciever na kugawana mali za mwanaume, kwa sababu mwanamke nae kapewa access ya kutafuta kama mwanaume ivyo hakuna sababu ya kuwa twgemezi au kuwa na entitled kwenye pesa na mali za mwanaume.

Kosa lililofanyika tumemwondolea mwanamke boundaries na limitation katika wajibu wake wakati hatujamwondolea mwanaume risk na mzigo anaoubeba. Ndio maana mwanaume akijipata anaogopa ndoa jqasababu haiingii akilini kugawana mali na mwanamke ambaye ajachangia chochote
Kosa si feminism, bali ni watu kushindwa kujadiliana kuhusu matarajio yao. Kama mwanaume hapendi kugawana mali, basi aongee hilo kabla ya ndoa na atafute mwanamke anayekubaliana na mtazamo wake. Vivyo hivyo, mwanamke akitaka mwanaume amuhudumie kabisa, naye aseme mapema. Ndoa inapaswa kuwa maelewano, si vita.
 
Je, unadhani sababu kuu ya divorce rate ndogo kwenye ndoa za kupangwa ni kweli watu wanaendana, au ni kwa sababu tamaduni zao haziwapi nafasi ya kutoka kwenye ndoa hata kama mambo hayaendi vizuri?
Misingi ya kuheshimu ndoa ikiwa ni kuheshimu maamuzi ya wazazi wao ,pamoja na tamaduni..

Bongo hatuheshimu ndoa ,mke wa mtu anatongwa kama kawaida ,wahindi wanaweka mpaka alama kweny paji la uso ili ajulikane yuko kwenye ndoa .

Jamii nyingi ndoa ni heshima inahitaji kulindwa na kutumikiwa ,kwa sasa tuna ishi kwa mfumo wa demokrasia kwamba mtu anaweza kuamua atakacho ..Kuna kipindi ndoa inakuwa ngumu ila unatakiwa kushikilia ili kuvuka Mtihani.

Magumu yapo sana ila ukiachika sio suluhu labda kama hautaki tena ndoa.​
 
Zamani wanawake hawakuwa na nguvu za kiuchumi, ndio maana ndoa nyingi zilidumu hata kama hakukuwa na furaha. Sasa wanawake wanataka kuheshimiwa, na wanaume pia wanataka wake wenye maadili ya zamani. Swali ni: Tunapataje balance kati ya zamani na sasa? Bila hivyo, ndoa nyingi zitazidi kuwa ngumu.
Kwasasa mwanamke ananyanyasika sana asipokuwa na kitu chochote chakumwingizia kipato, unakuta mzazi anamwambia kijana wake oa mke mwenye kazi, unategemea nini toka kwa mwanamke? Wanaume wa siku hizi wavivu wakuhudumia wake zao.
 
kwanza feminism imemwamimisha mwanamke ku-play role yake ya submissive ni utumwa kwaiyo moja kwa moja nguzo kuu ya maelewano haipo tena hapo

SIo mbaya mwanamke kujitegemea au kuwa na chanzo cha kipato. Lakini iyo haiendani na zile kanuni zilitumika kutengeneza msingi wa ndoa. Katika muundo wa ndoa mwanaume anaangiliwa kama provider kwaiyo anawajibika kwenda kutafuta ugali wa familia, mwanamke anaangaliwa kama receiver hivyo anabaki nyumbani kuangalia familia.

Sasa tukitumia kanuni ya 50/50 kwamba wote waende kutafuta maana yake inabidi tufanye marekebisho ya mfumo wa ndoa kwa kumwondolea mwanamke ile privilege ya reciever na kugawana mali za mwanaume, kwa sababu mwanamke nae kapewa access ya kutafuta kama mwanaume ivyo hakuna sababu ya kuwa twgemezi au kuwa na entitled kwenye pesa na mali za mwanaume.

Kosa lililofanyika tumemwondolea mwanamke boundaries na limitation katika wajibu wake wakati hatujamwondolea mwanaume risk na mzigo anaoubeba. Ndio maana mwanaume akijipata anaogopa ndoa jqasababu haiingii akilini kugawana mali na mwanamke ambaye ajachangia chochote​
Sio tatizo ,hauwezi kuingia kwenye ndoa kwa kuhofia matokeo yake bora usiingie kabisa.

Kufikiria ishu kama mali baada ya kuachana na mambo ya kuachana ni utapeli wa kujidanganya ni vyema usingeoa kabisa ..Usifungwe na mtego wa kupata watoto ambao ni matokeo ya ndoa .

Katika ndoa angalia kama jambo la ibada , heshima ,takwa la kibinadamu,utayari wako ilq usiangalie matokeo ya ndoa utafeli.​
 
Kosa si feminism, bali ni watu kushindwa kujadiliana kuhusu matarajio yao. Kama mwanaume hapendi kugawana mali, basi aongee hilo kabla ya ndoa na atafute mwanamke anayekubaliana na mtazamo wake. Vivyo hivyo, mwanamke akitaka mwanaume amuhudumie kabisa, naye aseme mapema. Ndoa inapaswa kuwa maelewano, si vita.
Hayo ni maelewano binafsi tu lakini sheria mama ina miongozo yake. Wewe unafikiri mwanamke anaelenga mali za mwanaume atakuja moja kwa moja kumwambia mwanaume kwamba anataka mali zake?

Feminism ndio iliyovuliga taasisi ya ndoa, imepachika miongozo ambayo haiendani na taasisi ya ndoa. Tuchague kimoja kipi cha muhimu kati ya feminism na ndoa.

Kama feminism ni muhimu basi taasisi ya ndoa iondolewe au ifanyiwe marekebisho kuendana na feminism, na kama ndoa ni muhimu basi tuachane na feminism au tuifanyie marekebisho iingie kwenye mfumo wa ndoa bila kuvuluga misingi yake.

Lakini feminism kwa namna inavyoenezwa na inavyotendeka kwenye jamii, tukitaka kuiingiza kwenye ndoa ni lazima mambo yavulugige.

We can't have feminist society without abolishing the marriage institute
 
Siri ya kupenda ni tofaut na Hali ya kuishi na mtu.
Ndyo maana Kuna mahusiano yanadumu zaid ya miaka 4 ila wakiona tuuh ndoa inavunjika ndan ya mwaka
Kuni Siri katka kuchagua mke au mume
 
Sio tatizo ,hauwezi kuingia kwenye ndoa kwa kuhofia matokeo yake bora usiingie kabisa.

Kufikiria ishu kama mali baada ya kuachana na mambo ya kuachana ni utapeli wa kujidanganya ni vyema usingeoa kabisa ..Usifungwe na mtego wa kupata watoto ambao ni matokeo ya ndoa .

Katika ndoa angalia kama jambo la ibada , heshima ,takwa la kibinadamu,utayari wako ilq usiangalie matokeo ya ndoa utafeli.​
Dunia imekua kijiji mikasa ya wake za watu kuchepuka, wanaume kufilisika baada ya talaka vijana wanaona. Uwezi kuwaokota akili kirahisi rahisi tu na izo blah blah za ibada
 
Si kweli kwamba ndoa ni biashara yenye faida kwa mwanamke pekee. Kila ndoa inategemea watu waliomo ndani yake. Kama mwanaume anaingia kwenye ndoa bila kuchagua mwenza sahihi, basi ni kweli atapata hasara. Lakini ndoa nzuri inaweza kumpa mwanaume utulivu wa maisha, familia, na mtu wa kushirikiana naye kufanikisha malengo.
Bwanamkubwa ukiona ndoa ipo na inaendelea ujue mwanaume amekubali yaishe.Chunguza ndoa nyingi wanaume hawakai kwenye nyumba zao zaidi ya masaa ya kulala pekee tena hiyo inakuwa ni usiku wa saa tano kwenda mbele.
 
Misingi ya kuheshimu ndoa ikiwa ni kuheshimu maamuzi ya wazazi wao ,pamoja na tamaduni..

Bongo hatuheshimu ndoa ,mke wa mtu anatongwa kama kawaida ,wahindi wanaweka mpaka alama kweny paji la uso ili ajulikane yuko kwenye ndoa .

Jamii nyingi ndoa ni heshima inahitaji kulindwa na kutumikiwa ,kwa sasa tuna ishi kwa mfumo wa demokrasia kwamba mtu anaweza kuamua atakacho ..Kuna kipindi ndoa inakuwa ngumu ila unatakiwa kushikilia ili kuvuka Mtihani.

Magumu yapo sana ila ukiachika sio suluhu labda kama hautaki tena ndoa.​
Heshima ya ndoa haipaswi kutoka kwa wanandoa pekee, bali pia kwa jamii inayowazunguka. Kama mke wa mtu anatongozwa na wanaume wengine au mume wa mtu anafanya usaliti, basi ni ishara kuwa jamii nzima haijaheshimu ndoa. Suluhisho siyo tu kuvumilia matatizo, bali kujenga mazingira yanayosaidia ndoa kudumu kwa heshima.
 
Kwasasa mwanamke ananyanyasika sana asipokuwa na kitu chochote chakumwingizia kipato, unakuta mzazi anamwambia kijana wake oa mke mwenye kazi, unategemea nini toka kwa mwanamke? Wanaume wa siku hizi wavivu wakuhudumia wake zao.
Je, unadhani wanawake wanapaswa kuingia kwenye ndoa wakijua kabisa kwamba hawatahitaji kumtegemea mwanaume, au bado mwanaume anapaswa kuwa provider hata kama mwanamke ana kipato chake?
 
Heshima ya ndoa haipaswi kutoka kwa wanandoa pekee, bali pia kwa jamii inayowazunguka. Kama mke wa mtu anatongozwa na wanaume wengine au mume wa mtu anafanya usaliti, basi ni ishara kuwa jamii nzima haijaheshimu ndoa. Suluhisho siyo tu kuvumilia matatizo, bali kujenga mazingira yanayosaidia ndoa kudumu kwa heshima.
Vijana wa sasa wanaona kama ndoa ni mchezo hata hwaheshimu zao na za wengine.
 
Hayo ni maelewano binafsi tu lakini sheria mama ina miongozo yake. Wewe unafikiri mwanamke anaelenga mali za mwanaume atakuja moja kwa moja kumwambia mwanaume kwamba anataka mali zake?

Feminism ndio iliyovuliga taasisi ya ndoa, imepachika miongozo ambayo haiendani na taasisi ya ndoa. Tuchague kimoja kipi cha muhimu kati ya feminism na ndoa.

Kama feminism ni muhimu basi taasisi ya ndoa iondolewe au ifanyiwe marekebisho kuendana na feminism, na kama ndoa ni muhimu basi tuachane na feminism au tuifanyie marekebisho iingie kwenye mfumo wa ndoa bila kuvuluga misingi yake.

Lakini feminism kwa namna inavyoenezwa na inavyotendeka kwenye jamii, tukitaka kuiingiza kwenye ndoa ni lazima mambo yavulugige.

We can't have feminist society without abolishing the marriage institute
Lakini feminism siyo adui wa ndoa. Ina maana ya kumpa mwanamke nafasi ya kuchagua maisha anayoyataka, siyo kumzuia kuolewa au kutaka familia. Tatizo si feminism, bali ni watu kushindwa kuelewana kuhusu matarajio yao kabla ya kuingia kwenye ndoa.
 
Siri ya kupenda ni tofaut na Hali ya kuishi na mtu.
Ndyo maana Kuna mahusiano yanadumu zaid ya miaka 4 ila wakiona tuuh ndoa inavunjika ndan ya mwaka
Kuni Siri katka kuchagua mke au mume
Lakini si kweli kwamba ndoa zote zinavunjika kwa sababu watu walichagua vibaya. Wakati mwingine mazingira na hali za maisha hubadilika baada ya ndoa, na watu wanashindwa kuzoeana na mabadiliko hayo. Swali ni: Je, kuna namna ya kuhakikisha kwamba wanandoa wanajitayarisha kwa changamoto zinazokuja baada ya ndoa?
 
Lakini feminism siyo adui wa ndoa. Ina maana ya kumpa mwanamke nafasi ya kuchagua maisha anayoyataka, siyo kumzuia kuolewa au kutaka familia. Tatizo si feminism, bali ni watu kushindwa kuelewana kuhusu matarajio yao kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Umeelewa ninachokiongea? Feminism kama feminism sio tatizo, ndoa kama ndoa sio tatizo. Tatizo ni kuyachanganya hayo mawili kwa pamoja kwa sababu constractive blocks zake zinapingana.
 
Bwanamkubwa ukiona ndoa ipo na inaendelea ujue mwanaume amekubali yaishe.Chunguza ndoa nyingi wanaume hawakai kwenye nyumba zao zaidi ya masaa ya kulala pekee tena hiyo inakuwa ni usiku wa saa tano kwenda mbele.
Lakini si ndoa zote ziko hivi. Kuna wanaume wanaopenda kutumia muda nyumbani na wake zao. Sio kila mwanaume anakubali yaishe, wengine wanashirikiana na wake zao kuunda ndoa yenye furaha. Labda tatizo si ndoa yenyewe, bali jinsi watu wanavyoichukulia.
 
Umeelewa ninachokiongea? Feminism kama feminism sio tatizo, ndoa kama ndoa sio tatizo. Tatizo ni kuyachanganya hayo mawili kwa pamoja kwa sababu constractive blocks zake zinapingana.
Lakini feminism siyo kuharibu ndoa, ni kuleta usawa wa haki kwa jinsia zote. Tatizo si feminism wala ndoa, bali ni watu kushindwa kuelewana kuhusu majukumu yao mapya. Ikiwa wanandoa wanakubaliana kuhusu namna ya kuendesha ndoa yao, feminism haiwezi kuwa tatizo.
 
Back
Top Bottom