KERO Je, kweli nchi yetu imeshindwa kujenga barabara za njia nne katika barabara kuu?

KERO Je, kweli nchi yetu imeshindwa kujenga barabara za njia nne katika barabara kuu?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KelvKate

Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
5
Reaction score
6
Naomba nitoe kero yangu.

Tumeona ajali iliyotokea Morogoro iliyosababisha vifo vya ndugu zetu. Hii ni mojawapo tu ya ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini, lakini hali hii inaendelea kujirudia bila mabadiliko makubwa.

Kero yangu kubwa ni hii: Je, kweli nchi yetu imeshindwa kujenga barabara za njia nne katika barabara kuu (main roads) kama Morogoro–Dodoma, Kibaha–Morogoro–Iringa–Mbeya–Tunduma na Songea–Njombe–Makambako?

Mipango ya kuboresha barabara hizi imekuwa ikitajwa kila mwaka katika hotuba za bajeti kuu, huku awamu za uongozi zikibadilishana, lakini utekelezaji wake bado hauonekani kwa kiwango kinachotarajiwa.

Ifike mahali kama nchi tuamue kwa dhati kuboresha miundombinu yetu kwa kujenga barabara za njia nne na kuzifanya kuwa kiwango cha kawaida katika barabara kuu nchini. Hatua hii inaweza kusaidia kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa, badala ya kuendelea kufanya marekebisho ya muda mfupi kwenye barabara za zamani na kutegemea zaidi tochi za barabarani kuwakamata madereva wanaovunja sheria.

Usalama wa barabarani unahitaji mipango ya muda mrefu na uwekezaji wa kutosha katika miundombinu, si hatua za kudhibiti madereva pekee.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom