Je, kwenye Biashara hizi uendeshaji na faida vinapatikanaje?

Je, kwenye Biashara hizi uendeshaji na faida vinapatikanaje?

Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga . Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi,
Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC , Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.
Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fikka 10- 15mullioni, inategemea ukubwa wa kituo,
Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18millioni.
Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni ,
Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo Moja ni 34millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni,
Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni.
Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta , pamoja na kuchimba mfeteji wa kupitisha Mafuta 3millioni
Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5nillioni.
Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.
NB: hizi ni gharama Kwa kituo standard , ila kama ukiamua kubana Kwa maeneo ya vinijini unaweza punguza gharama kidogo

Be blessed
 
Bei za kununulia Mafuta Depot Kwa wauzaji wa jumla bandari ya Dar es salaam
Petrol Kwa Ltrs Moja Tshs 2952.48 na
Disiel Kwa Ltrs Moja Tshs 2946.09.
Hizo ndio Bei rasmi bila punguzo , ukiongea nao wanakupa punguzo.
Ukitaka kujua Faida Kwa Ltrs Moja unachukua Bei ya kuuzia kwenye vituo vya mtani kwako una toa na hiyo Bei ya kununulia kutoka Kwa wauzaji wa Jumla.
NB; Kuna issue za usafirishaji ambazo huwa kama ifuatavyo kupeleka Mafuta Mwanza gharama zake ni Tshs 100-120 Kwa Ltrs na Mbeya na Tunduma Bei ni hiyo hiyo . Ndio maana Bei Zina tofautiana Kila mkoa ama Kanda Kwa sababu ya issue za usafiri. EWURA wanatoa Bei mpya Kila jumatano ya mwanzo wa Mwezi, wao hitoa Bei elekezi Kwa Nchi nzima
Nitarudi tena hapa
 
Sheli faida inakuaga ni sh 100 kila lita moja Ila mzunguko wake ni mkubwa Sana hivyo ni biashara yenye returning kubwa Sana.
Mzee sh 100 kwa lita moja ya mafuta ni hela kubwa sana navyojua mimi kwa lita moja faida huwa ni sh 20,30 mpka 50.

So unakuta mtu analita za mafuta lita laki 5+ au zaidi ukipigia hizo sent kwa lita hizo unaelewa
 
Leo tuziangalie hizi biashara tupeane mawili matatu kwenye angle hii ya

Uwekezaji, kwamba mtaji wa kiasi gani unahitajika ili kufaidi faida kubwa

Uendeshwaji wake

Faida zinapatikanaje

Biashara hizo ni

Sheli ya mafuta

Kampuni ya MADINI

Karibuni kwa michango.
Ila kama una mtaji wa chini ya 250m sikushauri ufanye biashara ya mafuta bro
 
Mzee sh 100 kwa lita moja ya mafuta ni hela kubwa sana navyojua mimi kwa lita moja faida huwa ni sh 20,30 mpka 50.

So unakuta mtu analita za mafuta lita laki 5+ au zaidi ukipigia hizo sent kwa lita hizo unaelewa
Lita laki 5 zinaeza isha ndani ya mda gani kwa Station iliyokua maeneo ya town..???
 
Mzee sh 100 kwa lita moja ya mafuta ni hela kubwa sana navyojua mimi kwa lita moja faida huwa ni sh 20,30 mpka 50.

So unakuta mtu analita za mafuta lita laki 5+ au zaidi ukipigia hizo sent kwa lita hizo unaelewa
Calculation za Faida ni rahisi sana kujuwa , unaangalia Bei elekezi ya vituo vya mafuta una toa na Bei elekezi ya wauzaji jumla, una toa gharama za usafiri, discount uliopewa Kwa wauzaji wa jumla na wewe unatumia kwenye kupunguza gharama ndogo ndogo.
Faida Kwa Ltrs sio chini ya Tshs 100.
 
Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga. Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi. Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.

Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg. Kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fika 10- 15 millioni, inategemea ukubwa wa kituo.

Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18 millioni.

Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni.

Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo, moja ni 34 millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni.

Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni. Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta, pamoja na kuchimba mfereji wa kupitisha Mafuta 3 millioni.

Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5 millioni. Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.

NB: Hizi ni gharama Kwa kituo standard, ila kama ukiamua kubana kwa maeneo ya vijijini unaweza punguza gharama kidogo.
Mkuu ule mpango waliokuwa nao BP kipindi fulani wa kuingia partnership na wamiliki wa maeneo wao wanajenga kituo bado upo ?
 
Ila kama una mtaji wa chini ya 250m sikushauri ufanye biashara ya mafuta bro
Wote walionza hakuna aliye anzia na mtaji wa mabillioni, wore Kuna sehemu walianzia.
Leo Hii Kuna baadhi ya maeneo ukiwa na 150millioni unaanza biashara. Vizuri tu, Tena ndani ya mwaka Moja unafikia break even point.
Hizi biashara zitahitaji kwanza uwe mjanja unaelewa Industry inahitaji kitu Gani Kwa Hilo eneo lako, then ndio mtaji unafuata..
Kuna njia nyingi sana za kupunguza gharama Kwa vituo vya vijijini , ukatumia less than 100M.
Tuwe wepesi kujifunza vitu Kwa undani, jitahidi kufanya feasibility study tumia muda na gharama kujifunza biashara inayohitaji uwekezaji mkubwa, ila Ukienda kicha kichwa. Utapigwa Kila eneo Hadi uone chamoto
 
Mzee sh 100 kwa lita moja ya mafuta ni hela kubwa sana navyojua mimi kwa lita moja faida huwa ni sh 20,30 mpka 50.

So unakuta mtu analita za mafuta lita laki 5+ au zaidi ukipigia hizo sent kwa lita hizo unaelewa
Kwa wale waliopo Dar es salaam mnaweza kufanya Hii hesabu mkatusadia vizuri
Mkuu ule mpango waliokuwa nao BP kipindi fulani wa kuingia partnership na wamiliki wa maeneo wao wanajenga kituo bado upo ?
BP walikuja kyuzwa na Sasa inaitwa PUMA, nimeona Oryx / Total amechukuwa vituo vingi vya Oil com mikoani.

Na wao wakicgukuwa wanampa mtu aendeshe ila sharti lazima ununue Mafuta kwao ya jumla na Faida wao wanachukuwa sehemu kubwa, wewe unakuwa kama mfanyakazi wao, Kwa mtaji wako.
Kwenye Faida wanatoa gharama zao za ujenzi plus Faida mnagawana
 
Back
Top Bottom