Gharama kubwa ni kupata eneo/ kiwanja Cha kujenga. Eneo liwe tambarare kupunguza gharama za kuujaza kufusi. Vibali vya ujenzi Unaanzia NEMC Hadi EWURA. Hapo lazima uwe na 10M to 20Million.
Gharama za ujenzi zimegawanyika kulingana na ukubwa wa eneo Eg. Kujaza zege inaweza eneo la pump,
Inaweza fika 10- 15 millioni, inategemea ukubwa wa kituo.
Gharama za Canopy / paa la kisasa linaanzia 30-60millioni, ila yapo ya kawaida unaweza Jenga Kwa 10-18 millioni.
Gharama za kutengeneza matanki ya kuhifadhia Mafuta, Tanki mbili zenye ujazo wa Ltrs 35elfu ukinunua material mwenyewe na kumleta fundi site kwako ni 20millioni.
Pump mbili za Mafuta zenye mikonga miwili / midomo miwili Kila upande mdomo, moja ni 34 millioni Kwa zote.
Generator nzuri ya kuendesha kituo 5-8millioni.
Gharama za kujenga office, vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo wafanyakazi ni 15millioni. Gharama za kuchimba mashimo ya Tanki mawili, kutengeneza mfumo wa kutenganisha Maji na Mafuta, pamoja na kuchimba mfereji wa kupitisha Mafuta 3 millioni.
Gharama za pipe za kutoka kwenye matanki Hadi kwenye pump ni 1.5 millioni. Gharama za kufunga. Mfumo wa umeme ni 3-6millioni.
NB: Hizi ni gharama Kwa kituo standard, ila kama ukiamua kubana kwa maeneo ya vijijini unaweza punguza gharama kidogo.