Je, kwenye Biashara hizi uendeshaji na faida vinapatikanaje?

Hiyo ni loyalty card wanaita, mteja anapo jaza Mafuta Kila siku mfano hiace, coaster, tipper, Malori Wana record kwenye kitabu Kila siku then mwisho wa Mwezi Wana jumlisha total Ltrs ulizojaza Kwa mwezi wanazidisha mara hiyo 50 ama 30 kupata hiyo bonus.
 
Nimejifunza kitu hapo. Kumbe wastani ili kituo kikamilike kabisa ni 200,000,000.
 
Anatoa kwenye faida yake au anakuminya kwenye lita unazonunua. Mfano badala ya Sh ef 2700 kupata lita 1, yeye anakupa lita 0.9?
Yeye anapo enda kununua Kwa wauzaji wa jumla huwa Wanapewa. Bonus / discount then na wao huwa wanairudiaha Kwa wateja wao , hiyo piya wanapunguza kwenye sehemu ya profit.
 
Kuna mtu aliniambia wauza mafuta wanalipwa laki 2 nilibisha.kumbe kweli.
Na wale wanaobetisha pale caunta mshahara bei gani?
 
Yeye anapo enda kununua Kwa wauzaji wa jumla huwa Wanapewa. Bonus / discount then na wao huwa wanairudiaha Kwa wateja wao , hiyo piya wanapunguza kwenye sehemu ya profit.
Nimekupata. Security wise ikoje?. Siku hizi sisikii habari za vituo kuvamiwa kama zamani. I don't believe kuwa kila baada ya saa 1 wana bank mzigo.
 
Nimekupata. Security wise ikoje?. Siku hizi sisikii habari za vituo kuvamiwa kama zamani. I don't believe kuwa kila baada ya saa 1 wana bank mzigo.
Issue za kuvamiwa zinatengenezwa na wafanyakazi wa ndani wanauza ramani ya Kwa majambazi mfano pump attendant anavyopekea Hela na kuuza Mafuta wanaona wameuza kiasi Gani Wana kadiria mauzo then wanawatafuta watu wa kazi wamaluze mchezo.
Solution;-
Kusisitiza malipo through Lipa Number, Kuwa na POS mashine mtu akija anatumia kulipia na fedha zote kwenda Bank direct .
Kuwa na sheria Kali kuhusu Hela anazoruhusiwa pump attendant kuwa nazo nje. Inatakiwa mauzo Kila yakizidi laki mbili waende kwenye chombo Cha kutumbukiza fedha ( huwa kunakuwa na shimo / tunduukutani linakwenda direct kwenye sefu ndani ya strong room) Hilo Shimo/Tundu linatengenezwa Kwa pipe inakuwa na Kona nyingi na slopi Kali za kuterezesha hela
 
Tumechangia vya kutosha Hii thread, Sasa naomba tufike hitimisho, Kwa mwenye location eneo la kijijini ama makao makuu ya Wilaya,
Kifupi mwenye eneo ambalo anaweza kujenga Kituo Cha Mafuta.
Kama mwana JF yoyote yule mwenye Capital ya kuanzia 70/90millioni akiwa na eneo tayari , nipo tayari kumuonyesha njia nyepesi ya kujenga Kituo Cha Mafuta Kwa huo mtaji.
Nitamsadia Kila kitu Bure bila malipo, Kila siku tunajadili mada nyingi bila mrejesho.
NB ;- Kwa maeneo ya wilayani na vijijini Nina uwezo wa kumsadia mtu mwenye mtaji wa kyanzia 70/90Millioni kujenga Kituo Cha Mafuta.
 
Thanks a lot brother, nitakutafuta I promise you .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…