Je, kwenye ulimwengu hali ya utupu inawezekana?

Je, kwenye ulimwengu hali ya utupu inawezekana?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Hello peoples..

Hebu tujisaule hapa kwa kuchanganya maarifa juu ya UTUPU kwenye ulimwengu, swali la msingi ni kuwezekana kwa hali ya utupu, namaanisha hivi mpaka sasa binadamu na teknolojia yake bado hajaweza kufikia hatua ya Kutengeneza utupu (vacuum), kwa asilimia mia!.

Ataweza kutoa hewa lkn sio atom!, na sidhani kama sasa tuna teknolojia yakutoa atom zote kwenye space!, maana jambo la kushangaza walipofanya jaribio la kuunda utupu kuna atom zilijitokeza pasipo kufahamika zilipotoka!.
Na binafsi ndio maana nikiulizwa ni kitu gani cha ajabu kwenye huu ulimwengu basi sisiti kukuambia kuwa space ndio inaajabu kushinda vitu vyote!.

Mada yangu haichokozi kuhusu uwezo wa binadamu kwenye Kutengeneza utupu (vacuum), mada yangu inajikita zaidi kama ulimwengu unaruhusu hali ya utupu kuweza kufanyika!, hapa namaanisha utupu ambao ni asilimia mia moja!.

Lakini pamoja na hayo ninapata mashaka ikiwa ipo hivi, kama ulimwengu unaweza kuruhusu utupu dukuduku langu ni nahisi kuwa, Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa kikawa ni kitu hatari ikiwa binadamu akiweza Kutengeneza na namashaka ndio inaweza ikawa siraha kubwa kushinda siraha zote ambazo umewahi kuzifikiria!.

Vilevile ikiwa ulimwengu hauwezi kuruhusu utupu basi ulimwengu ni ombwe ambalo limekamilika hakuna kinaweza kutoka wala kuingia, namaanisha na mipaka yake haiwezi kuharibika huku sheria zake zikiwa nizakujitegemea haziwezi kwenda nje yani alpha na omega!..
msiniulize kwanini nafikiria hivi bado nami sijapata jibu kwanini nafikiria hivi kwasasa!.

Hivyo mdau wewe nini mawazo yako, je unafikiri ulimwengu unaweza kuruhusu ama hauwezi kuruhusu utupu...
 
We cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of mysteries we are trying to solve.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, uchunguzi, udadisi na majaribio zaidi.
 
We cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of mysteries we are trying to solve.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, uchunguzi, udadisi na majaribio zaidi.
Ama sisi ndo wanufaika wa nature!
 
true vaccum kumanisha hakuna hata matter kwenye ulimwengu, si itakuwa ni chaos, hakutakuwa na sound, air, light, heat, hata gravity pia sidhani kama itakuwepo kwa hiyo kama hakuna hivyo.
sijui itakuwaje🤔🤔🤔
 
true vaccum kumanisha hakuna hata matter kwenye ulimwengu, si itakuwa ni chaos, hakutakuwa na sound, air, light, heat, hata gravity pia sidhani kama itakuwepo kwa hiyo kama hakuna hivyo.
sijui itakuwaje🤔🤔🤔
haha! ni ngumu hata kuimagine utupu wa space upoje!
 
Vacuum(utupu) ni neno linalotokana na neno la kigiriki vacuus(adjective),neuter vacuus likiwa na maana ya "vacant au void" kwa maana ya utupu.

Vacuum(utupu) ni nini?
Vacuum(utupu)> ni hali pasipo kitu,nafasi pasipo maada. Yaani nafasi tupu ambapo hakuna kitu chochote,hakuna maada,hakuna hewa,hakuna gesi.

Ili tutengeneze vacuum(utupu) inabidi tuondoe kila kitu(maada,air,gas n.k) pasiwepo na kitu.

Je binadamu anaweza kutengene a perfect vacuum jibu ni hapana. Kwasababu quantum theory ina dictate kwamba energy fluactuations inayojulikana kama virtual particles constantly huwa zin pop in and out of existance,hata kwenye empty space.
 
Back
Top Bottom