Je, mabeberu wataruhusu tupate katiba mpya itakayogusa Maslahi yao?

Je, mabeberu wataruhusu tupate katiba mpya itakayogusa Maslahi yao?

Hawana maslahi ya Hila kama unavyotaka kuweka, ama Mwigulu anavyoiweka. Chochote watakacho wanaweza kukipata kwa mikataba halali. Lakini kutaka kuonyesha wao ndio wanaamua katiba yetu iweje, huo ni upotoshaji usio na tija.

Sijasema wao ndio wanaamua iweje.
Ila wanaweza kuinfluence kwa njia mbalimbali
 
Hawana muda huo boss kwa sasa. Kwa sasa wametuachia wachina wao ndio wamejikita zaidi huku Africa kwa sasa. Ni aidha unapotosha, ama umechotwa na propaganda za kizee za ccm.

😆😆😊😀
Kwamba nchi imeishiwa vitu vya maana. Sio?
 
Anhaa!
Itakuwa wewe ni miongoni mwa watu mnaoamini tupo huru sivyo?
Tupo huru ndiyo, sema ni vile tu waafrika tukifeli basi tunatafuta wa kumpa lawama kuwa ni mabeberu wanatuonea wivu!!

Mbona Ethiopia ilijenga bwawa la umeme kubwa zaidi Afrika licha ya vitisho vya Misri na "mabeberu"? Umeona wamepoteza lolote au "kushughulikiwa"?

Hatujiamini tu, ila hakuna beberu atakupinga kutengeneza katiba mpya nzuri kuhusu maslahi yao hayo yanajadiliwa mezani kibiashara zaidi kwa kampuni zao kueleza mazingira wanayotaka na serikali kueleza misimamo yao ndiyo negotiations hufanyika ila sio kama hivi mnavyodai kuwa hawataki tupate katiba mpya.

Kama ingekua hivyo tusingeona Commonwealth au EU zikipinga matukio ya uchaguzi 2025 ama kushauri iwepo katiba mpya na tume huru ya chaguzi.
 
Haina vya kutakwa na wazungu hadi wafanye hila kwenye katiba ya wananchi.
Huwa tunapenda kujipa umuhimu sana. Yaani nchi ambayo ni omba omba na karibu 40% ya bajeti inategemea mikopo ya wazungu eti watuonee wivu?

Hii mentality mbovu sana ya CCM kujitafutia kinga pale wanapofeli kila kitu
 
..Kuna Katiba ya kwanza baada ya uhuru ambayo tuliandikiwa na Waingereza.

..Katiba hiyo ilikuwa ni ya mfumo wa vyama vingi.

..pia Katiba hiyo ilikuwa inaruhusu mgombea binafsi.

..Pia kuna chaguzi ambazo zilisimamiwa na Wakoloni wa Kiingereza na zilikuwa chaguzi safi hakukuwa na kuenguliwa, au kuibiana kura, au kutangazwa kwa nguvu.

..Wachambuzi, na wanazuoni wa Katiba, kama Deus Kibamba wanaamini Katiba tuliyoandikiwa na Muingereza ilikuwa na mambo mazuri ambayo TANU ilikuja kuyapiga chini.
Sahihi kabisa..

TANU ilizika demokrasia iliyokuwepo hapo awali na kuvibana pia vyama vya wafanyakaz vilivyosimama awali na TANU kwenye harakati za kudai uhuru.
 
Huwa tunapenda kujipa umuhimu sana. Yaani nchi ambayo ni omba omba na karibu 40% ya bajeti inategemea mikopo ya wazungu eti watuonee wivu?

Hii mentality mbovu sana ya CCM kujitafutia kinga pale wanapofeli kila kitu
Kabisa, na huyu mtibel naye anaokota huo utapeli anatuletea humu.
 
Usiwachukie ndugu zako kisa tofauti zenu za kiimani
Mimi naelezaga ukweli ambao mtu yoyote atakaye ukataa lazima yamkute majuto..kwa sababu siku zote wapumbavu ujifunza kwa hasara na maumivu na uchungu ..kwa sababu u practice upumbavu
 
Wewe nyani mweusi nakukata mshahara huu mwezi
Kuamini tu kuwa mudi boy ni mtume tena mtakatifu na uislamu ni dini takatifu ni ujinga kama kuamini muhuni na tapeli mwamposa kuwa naye ni mtume.
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU
 
Wanacho kotika wazungu ni hiki

Sijawahi kuona katiba ya nchi moja inayogusa maslahi ya nchi nyingine.

Mbona Kenya wamebadili yao na haijatuathiri sisi.
 
Back
Top Bottom