Je, Mafia Kisiwani kuna barabara za lami?

Je, Mafia Kisiwani kuna barabara za lami?

Mkuu kilwa na liwale umefika lini??
kilwa rami kila mahali kivinje masoko lami tupu hadi mitaani sijui kilwa ipi waongelea

Liwale kuna rami pia ila haiunganishi wilaya kama kilwa na ruangwa au nachingwea
Kilwa lami ipo ya kutoka Nangurukuru mpaka Kivinje na masoko ila sio lami za kuunganisha mitaa, Liwale lami ipo mjini kati ila mitaani kwa raia hamna na ya kuunganisha wilaya hamna bora hata Mafia ukiacha hiyo ya msaada wa mwamerika kuna lami mitaani hasa kuanzia kkkt kichangachui mpaka beach kwa wavua dagaa kitu ambacho wilaya nyingi nchini lami za mitaa japo miwili hamna.
 
Kilwa lami ipo ya kutoka nangurukuru mpaka kivinje na masoko ila sio lami za kuunganisha mitaa, liwale lami ipo mjini kati ila mitaani kwa raia hamna na ya kuunganisha wilaya hamna bora hata mafia ukiacha hiyo a msaada wa mwamerika kuna lami mitaani hasa kuanzia kkkt kichangachui mpaka beach kwa wavua dagaa kitu ambacho wilaya nyingi nchini lami za mitaa japo miwili hamna

Tuoneshe
 
Hongereni kwa advancement, vipi usafiri meli zipo au bado ni lile dude la Msimbat
Kuna meli bora kabisa kama kilimanjaro ya kwenda Zenji unacheki mpaka movie pia kuna meli ya Jeshi hiyo ina huduma bora balaa, unasafiri kama upo mamtoni, huwezi linganisha na visiwa vingine kama Songosongo huko ni kupanda majahazi tu mkifika mnashukuru.
 
Wenye maswali kuhusu Mafia uliza hapa ujibiwe, niko Mafia kikazi.

Usafiri kuna meli Mv songosongo inamilikiwa na Jeshi ina uwezo wa kubeba abiria 200+. Kuna kivuko Mv Nyamisati kinamilikiwa na Serikali kinabeba abiria 200 na mizigo tani 100.

Barabara ya lami ipo kutoka bandarini hadi Utende, kuna nyingine inawekwa lami sasa.
 
wenye maswali kuhusu mafia uliza hapa ujibiwe, niko mafia kikazi.

Usafiri kuna meli Mv songosongo inamilikiwa na jeshi ina uwezo wa kubeba abiria 200+. Kuna kivuko Mv Nyamisati kinamilikiwa na serikali kinabeba abiria 200 na mizigo tani 100.

Barabara ya lami ipo kutoka bandarini hadi utende, kuna nyingine inawekwa lami sasa.

Uko Mafia sehemu gani??
 
Unatokea wapi? Kama dsm panda bus pale mbagala mwandege za kwenda nyamisati ukifika hapo utakuta meli iko tayari kukuvusha ukale bata na wazungu kibao ndo msimu wao kuanzia januari mpaka april tunakula nao supu ya pweza
Oh asante kunikumbusha ni Nyamisati siyo Msimbati, inapiga trip ngapi kwa siku Mkuu nikitoka Dar nifike saa ngapi pale
 
Back
Top Bottom