Okoth p'Bitek
JF-Expert Member
- Jan 11, 2019
- 1,124
- 1,384
Janii ni nyokoooo.....nnadhani watu wengi wanaokosea kwenye jani ni wake wanaotafuta ile stimu ya ukungu...kwa uvutaji ule unaweza ukawa unapiga hata sita mpaka 10 per day....ukisikiliza mziki unausikia kwenye angle nzuri...kula sana na mambo kadha wa kadha...mtu wa aina hii anauwezo wa kuvuta bangi kila siku mpaka siku atakayoamua kuigeukia heroin.....wengine wanakuwaga mateja kabisa...Kwa experience niliyonayo kwenye hiyo kitu sijui nianze kukuelezea wapi!
Kwanza kabisa: kama umesha toboa 25 na hujawahi tumia kilevi chochote, yani pombe, sigara na ganja, sikushauri uthibutu kuanza kutumia hivyo vitu kabisa wewe endelea kunywa juice za embe na machungwa na maji kwa wingi, hivyo vitu hapo juu usiviwaze kabisa.
Kwanini: mwili na akili yako hua havipokei effect zake kwa haraka, hua vinaenda vikijifunza taratibu hivyo ni ishu kuvi control mapema, hivyo mbali na kulewa baada ya kutumia wewe ndio unalewa kuzidi kutaka kuvitumia, utataka ujaribu kila linalowezekana ili uone matokeo yake na hapa ndipo watu tunapo poteana, wengine hua hawaridhiki na walivyotumia au walivyozoea tumia au walivyo kwisha tumia na kuendelea kujaribu vigeni zaidi kwao ndio hudondokea kwenye UNGA AKA NGADA na mpaka hapo biashara inakua imefika mwisho.
Hivyo mpaka kufikia kuvimudu hivyo vitu kwanza unatakiwa uwe na kichwa kizuri ( kwa neema ya Mungu na jinsi alivyo kuumba [emoji72] ) pia uweze kuhimili mihemko means uweze kuendesha akili zako sio kila amri inayotoka kichwani mwako uwe unaitekeleza, unapoona imetosha maana yake imetosha na sio " ngoja niongeze kidogo ", unapoona hiki hakiwezekani au ni hatari ukae kujiua ni hakiwezekani na ni hatari kweli sio " ngoja nijaribu nione "
Pia mwili na akili yako vikubaliane sio mwili hautaki alafu akili inakulazimisha au akili haitaki mwili unakulazimisha, ukisema unatumia maana yake unatumia na ukikataa maana yake usitumie kifupi vinahitaji nidhamu, ukiwa mfujaji navyo vitakufuja!
Bahati mbaya huwezi pata hiyo nidhamu mapema hua inachukua muda mpaka uvizoee ndio maana nikakwambia kama umetoboa 25 usivifikirie mf: ganja nimeitumia mfululizo ( matumizi ya kawaida ya kila siku asubuhi, sometimes mchana, na usiku na usiku ndio ilikua sherehe[emoji16]) kwa miaka kama 9 au kumi tangu gari limewaka form two[emoji2960]. Ndio nikaanza kubadili utaratibu wa matumizi na aina za matumizi lakini nilikua siwezi kufanya chochote kama sijapasha pia haikua rahisi ilini gharimu ila kwakua niliidhamiria akili na mwili vilikubali nika stop ghafla baada ya attempt kadhaa za kuacha kikawaida kushindikana ( kama kupunguza dose, kuruka siku moja moja na nyinginezo ), niliumwa hatari mpaka kulazwa hosp na hata nimetoka hosp hali haikua nzuri homa si homa, no kula no nini, ila shangaa dawa ikawa ni hiyo hiyo ganja tena, nimetoka hosp kufika home nikajichekecha nikaenda kuipuliza nilipona hapo hapo na ndio ikawa mwisho kuitumia mfululizo[emoji854] hivyo unapata picha ukiianza ulevi na 25 itakavyo kugharimu, huto pata muda wa ku turn_over
Kwa story hiyo fupi kulingana na swali lako, sio ganja pekee! Kilevi cha aina yoyote mpaka ukijue na kukidhibiti kinakuhutaji muda na lazima kikugharimu kwanza ndio uweze kuki control. Sijui nitakua nimekujibu!!?
Kuna hii bangi inayokupeleka kwenye hallucination na mara nyingi huchangiwa na namna unavyotaka kujitafuta na kujielewa wewe mwenyewe...ukiipeleka kujiaminisha maisha ambayo hayapo kwenye jamii trust me utaishia huko....ukiipeleka vizuri itakufundisha namna ya kuishi na watu vizuri....Kuelewa uwepo wa Mungu maana kuna hali utakuwa unaipitia ya kuhisi kabisa uwepo wake na ukimueleza kuhusu ni kwa namna gani ungependa akusaidie kwenye maisha yako.....utafanya mema mengi...Ego itashuka...hutakuwa judgemental kwenye maisha yanamhusu mtu zaidi utapenda kuelewa zaidi kilichompelekea yeye kuingia kwenye hio hali....Lakini kipindi unakutana na hii hallucination broooo ni nyoko kuna muda nilikuwa ninahisi nnakuwa kichaa.....maisha yako unayoyaishi unakuwa unayaangalia kama movie...kuna kipindi utahisi unakufa ile hali ikikukuta utaandika mpaka wosia utapiga simu kuaga....nnakumbuka .hali mbaya zaidi niliyowahi kuipitia ni ya kuhisi nnaingia kwenye version mpya ya maisha... akili inatengeneza segment utoto ujana uzazi uzee kwa hiyo kama ulikuwa unajihisi wewe ni kijana kwenye sober life utaona kama ndio unaingia kwenye kuwa mzazi....unajuta kwa yale mabaya yote uliyoyafanya na kile kitu kinakufanya unakuwa weak sana.by that time..jamii ilikuwa inaelekeza hivi wewe unaenda hivi...kuna mtu ulimkosea maybe......so siwezi kusema bangi ni nzuri kwasababu sio kila mtu huwa anafaulu kwenye kujitafuta....