Je, Magic Mushrooms ni halali hapa Tanzania?

Status
Not open for further replies.
Janii ni nyokoooo.....nnadhani watu wengi wanaokosea kwenye jani ni wake wanaotafuta ile stimu ya ukungu...kwa uvutaji ule unaweza ukawa unapiga hata sita mpaka 10 per day....ukisikiliza mziki unausikia kwenye angle nzuri...kula sana na mambo kadha wa kadha...mtu wa aina hii anauwezo wa kuvuta bangi kila siku mpaka siku atakayoamua kuigeukia heroin.....wengine wanakuwaga mateja kabisa...
Kuna hii bangi inayokupeleka kwenye hallucination na mara nyingi huchangiwa na namna unavyotaka kujitafuta na kujielewa wewe mwenyewe...ukiipeleka kujiaminisha maisha ambayo hayapo kwenye jamii trust me utaishia huko....ukiipeleka vizuri itakufundisha namna ya kuishi na watu vizuri....Kuelewa uwepo wa Mungu maana kuna hali utakuwa unaipitia ya kuhisi kabisa uwepo wake na ukimueleza kuhusu ni kwa namna gani ungependa akusaidie kwenye maisha yako.....utafanya mema mengi...Ego itashuka...hutakuwa judgemental kwenye maisha yanamhusu mtu zaidi utapenda kuelewa zaidi kilichompelekea yeye kuingia kwenye hio hali....Lakini kipindi unakutana na hii hallucination broooo ni nyoko kuna muda nilikuwa ninahisi nnakuwa kichaa.....maisha yako unayoyaishi unakuwa unayaangalia kama movie...kuna kipindi utahisi unakufa ile hali ikikukuta utaandika mpaka wosia utapiga simu kuaga....nnakumbuka .hali mbaya zaidi niliyowahi kuipitia ni ya kuhisi nnaingia kwenye version mpya ya maisha... akili inatengeneza segment utoto ujana uzazi uzee kwa hiyo kama ulikuwa unajihisi wewe ni kijana kwenye sober life utaona kama ndio unaingia kwenye kuwa mzazi....unajuta kwa yale mabaya yote uliyoyafanya na kile kitu kinakufanya unakuwa weak sana.by that time..jamii ilikuwa inaelekeza hivi wewe unaenda hivi...kuna mtu ulimkosea maybe......so siwezi kusema bangi ni nzuri kwasababu sio kila mtu huwa anafaulu kwenye kujitafuta....
 
Kuelezea hivi vitu i mean experience wanayokutana nayo watu kipindi wanakutana hallucination ni ngumu its like unakuwa na mind nyingine ambayo ni intelligent na advanced kuzidi ile unayoitumia kila siku kwenye maisha...na ni kama vile huwa ina take over na kuanza kukufundisha how to live....hivi sio sawa, pita hapa, fanya hivi, usifanye hivi, ambayo sijawahi kuielewa ni pale nnapopitiaga ile hali ya kuhisi kama vile kuna mazungumzo unafanya na Mungu ukisha notice tuu ile hali...utaongea kwa muda pale tuu utakapoanza kufikiria cha kuongea, ile connection huwa inakatika....huwa nnahisi nimetumia hata lisaa...kumbe ukiurudisha ule muda kwenye dunia yetu sidhani kama hata dakika mbili huwa ninamaliza.haitokei unapokuwa na mtu huwa ni jeshi la mtu mmoja
 
Hauwez kufanya kila mtu ajue mkuu , kama soul ya mtu sio wakati wake wa kuamka atabaki tu hivyo hivyo.
 
Mkuu huu ni ukwel 200%
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Yaani! Kwa bahati mbaya " kutoa hawa wanaopitia humu kupata experience kabla hawajatumia " wengi tumetumia tukia hatujui maana halisi ya meditation, hivyo tulikua tuna enda enda tu, Mungu muweza kuna tulio mudu kui control na kuna walio feli na wengine kuangukia kwenye Heroin nadhani hiyo heroin ndio janga halisi
 
Dawa sio meditation hizo, dawa ni kumpokea Yesu moyoni mwako, ukiokoka utajazwa Roho Mtakatifu, utapata maono na mafunuo kutoka kwa Mungu wa kweli, utapata uzima wa milele.
Yesu mwenyewe alikua anafanya meditation unafikir alikua anajitenga milimani kufanyaje? Sala za wakatholic za rozali ni aina ya mantra meditation , hakuna din isiyo na kipengele cha meditation japo kwa uchache.
 
Dah Hii Kitu Jamani sitaki kukumbuka Maana kila nikikumbuka naona kama ni Jana imenitokea kumbe ni kama miaka 10 ilopita...

Sasa nisikilize nikupe Experience yangu kuhusu Hii Magic mushroom ambayo sijawahi kuisema popote kwa sababu zangu binafsi..

Ilikuwa mwezi wa 12 Mwaka 2011 Nikitoka kwenye mishe mishe Nikapoteza Baadhi ya pesa ambazo sikujua nimeziweka wapi na zilikuwa pesa za Muhimu sana Kuna watu niliwahisi wamechukua Ila wakagoma sasa kwa wakti huo siku na uwezo wa kupata hizo pesa...Kila nikijaribu kuwaza mwezi wa kwanza 2012 zinatakiwa hizo pesa na kwa muda huo nisingeweza kuzpata kwa wik8 mbili zilizobaki...

Sasa nikamshirikisha Rafiki yangu Mmoja akaniambia mbona hilo jambo Dogo Twende Maramba (Tanga) kwa fulani tukaangalie...

Sasa me nikajua tukifika Atafanya mambo yake na atasema anazo nani na atafanya dawa Ya kuzileta (Maana mimi sikiwahi kabla kwenda kwa mganga)..

Bhna jamaa si akaja na maji kwenye Chupa ya Kilimanjaro Ndani yana kama vitu vyeupe vimechangnywa akaniuliza "umekula"

Nikamwambia sijala akasema vizuri akamimina kwenye kikombe yale maji mchanganyiko na vitu vyeupe akaniambia kunywa bila kufikiria radha nikanywa yote..

Akaniambia nikae juani ili dawa ifanye kazi Guyz "Mushroom halucination we zisikie tu"

Hakuna matukio niliacha kuyaona mengine sikuwahinhata kuyajua na nilipowauliza wahusika niliowaona kwenye matukio hayo walikuabli kweli yalitokea...

Japo sikuafanikiwa kumuona mwizi wangu wlaa aliyechukua wala tukio la hela ila kuna baadhi ya matukio ya mbele niliyaona (Ambayo baadae nilikuja kuyashuhudia in reality ila niliyaona kwenye ile hallucinative )...
Baadaye nilipokuja kuchunguza nilijua kuwa walinipa Mushroom..

Guyz msijaribu kabisa maana ukiangalia ukutani utaona hallucinatiom ukifba macho utaona vild vile ni hatari sana msijatibu hii kitu....
Naungana na wale wanaosema unaweza ukachizi kwa sababu unaona Vitu in reality na sio kuwaza unaona kitu kama unaangalia Movie....

Namalizia kwa Kusema KAMA WEWE NI MFANYAJI WA MEDITATION NA TAYARI UOGA KWAKO UMEONDOKA UNAWEZA UKAJARIBU HII KITU...

LAKINI KAMA WWE SI MFANYAJI WA MEDITATION NA UNA UOGA WA ASILI USIJARIBU KABISA HII KITU WALA HATA KUISOGELEA NI HATARI SANA
 
Huu ni ukweli kwa 100%
 
Au Nabii daudi anaita "Bonde la uvuli wa mauti" kwenye Zaburi 23
 
Huu uongo kabisaa,huyu samaki namla sana Tena mtamu balaa ila sipati hizo hallucinations. Tena wapo aina mbili wanaofanana wanaitwa kibua mbono
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ€£πŸ€£ Mzee huyo sio kibua wala mbono wala hata Sio Samaki changu 🀣🀣🀣
 
Watu tumepewa uwezo wa kuona bila hata hayo madude...

Hichi nilichoona juzi ndicho kinaniwazisha...

Mungu wangu nisaidie..

Naona kama maono...

Mwendazake akiwa kaja kuchukua majina ya waliomdedisha...

Jamani, ni kama nimemuona sehemu ya watu wengi ni kama sokoni, ila ghafla nikamuona akitoka nje ya mlango wa soko akawa anaondoka, ila nikaona amerudi na alipofikia mlango, pembeni kulikuwa na msalaba upo nje juu ya kitu, ndani yake kuna majina ya waliomdedisha nikaona anauchukua msalaba..

NB: Si mara moja naona yanayohusu Mwendazake...
Rabbon
 
Si pekeako, wengi wanaona.

Zipo Roho ambazo hutangatanga, ni zile Hasa ambazo maisha yalikatiliwa kabla ya muda wake. Ni zipo kudai kisasi.

Tusubiri.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…